kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
IDADI ya taasisi zinazojiingiza kwenye mgogoro wa CCM na Chadema, uliosababisha polisi kuua watu watatu na kuujeruhi 29 mkoani Arusha inazidi kuongezeka, baada ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam (T), kuandaa mkutano utakaoshirikisha jumuiya na taasisi mbalimabili kutoa tamko.
Tayari, hadi sasa taasisi mbalimbali za dini, jamii, uchumi, siasa na viongozi wa vyama na serikali, wamejitokeza na kutoa misimamo yao kuhusu mgogoro huo, huku mitazamo ikikinzana.
Katika matamko hayo wapo waliolaumu polisi kwa kusababisha mauaji hayo, wengine wakilaumu wanasiasa kwa kukiuka amri ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Katibu wa baraza hilo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema mkutano huo utafanyika ukumbi wa Diamond Jublee jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.
"Lengo la mkutano huu ni kuweza kujadili kwa kina mgogoro wa Arusha na kuweza kutoka na msimamo wetu kupitia tamko la pamoja ambalo litasomwa kwa niaba mbele ya waandishi wa habari na washiriki wote," alisema Sheikh Ponda.
Sheikh Ponda, ambaye pia ni Katibu wa Kutetea Haki za Waislaam Tanzania, alisema tayari zaidi ya jumuiya na tasisi 10 za Kiislaam zimethibitisha ushiriki wao.
"Mkutano utazishirikisha taasisi zaidi ya 10 na tayari zimethibitisha ushiriki wao, wadau na washiriki wa mkutano huu watapata fursa ya kuchambua chanzo, mwenendo na athari za mgogoro wa Arusha kwa wenyeji wake na Watanzania kwa upana," alisema.
Alisema suala la Arusha halipaswi kunyamaziwa na kwamba, lazima kwa upande wao watoe tamko ili kuonya na kukemea au kutahadharisha mambo mbalimbali kwa usalama wa taifa.