Masharti mapya bima afya yaanza

Masharti mapya bima afya yaanza

Bravo AI

Senior Member
Joined
Jan 13, 2023
Posts
145
Reaction score
298
Mfuko huo sasa una utaratibu mpya ulioanza jana Machi 13, kundi hilo linalazimika kulipiwa malipo yao kupitia uanachama wa wazazi au walezi wao ambao ni wanachama kupitia vifurushi vya mfuko kulingana na ukubwa wa familia.

Vifurushi hivyo ni vilivyopewa majina ya Najali Afya, Timiza Afya na Wekeza Afya.

Januari mwaka huu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, alisema atasimama kidete kuhakikisha kila Mtanzania anafahamu umuhimu wa kuwekeza na kuweka kipaumbele kwenye afya na hakutakuwa na msamaha wowote.

Waziri Ummy alisema ajenda kuu iliyopo mbele ya sekta hiyo ni huduma bora na Bima ya Afya kwa Wote, ambayo kwa sasa kiwango kinachotazamiwa ni kuwa kati ya Sh. 340,000 hadi 360,000 kwa mwaka, ili kuhudumia watu sita kwa huduma za rufani, kanda na kibingwa.

UTARATIBU MPYA

Meneja Uhusiano wa NHIF, Angela Mziray, jana aliiambia Nipashe iliyotaka kufahamu utaratibu mpya kuhusu huduma hizo, kwamba utaratibu huo ulianza rasmi jana na bei za vifurushi kulingana na familia wachangiaji kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35, ni kuanzia Sh. 192,000 kwa huduma za kifurushi cha Najali Afya; Sh. 384,000 (Wekeza Afya) na Sh. 516,000 kwa Timiza Afya.

Aidha, kifurushi kama hicho yaani mtu mmoja, bila wategemezi, kwa wachangiaji kuanzia umri wa miaka 35 hadi 59 gharama ni Sh. 240,000 kwa huduma za kifurushi cha Najali Afya; Sh. 444,000 (Wekeza Afya) na Sh. 612,000 kwa Timiza Afya.

Kadhalika, vifurushi kwa ajili ya wanandoa pamoja na mtoto mmoja kwa wachangiaji kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35, ni Sh. 504,000 kwa kifurushi cha Najali Afya; Sh. 924,000 (Wekeza Afya) na Sh. 1,272,000 kwa kifurushi cha Timiza Afya.

Pia kifurushi kwa ajili ya wachangiaji kuanzia umri wa miaka 36 hadi 59 wakijumuishwa watoto wawili, gharama ni Sh. 696,000 (Najali Afya); Sh. 1,248,000 (Wekeza Afya); Sh. 1,728,000 (Timiza Afya) kwa mwaka.
 
Sijui Tunaelekea wapi kama Taifa! tokea mama makinda amekuwa mwenyekiti wa bodi ndio shida zoote hizi zimeanza! MAKINDA amekuwa mbunge tokea 1975 sasa atajuaje shida zetu mtu kaishi maisha ya raha

mtanzania maskini anayehangaika kupata mbolea mifuko miwili atawezaje lipa hizi gharama? Rais Samia lione hili
 
Hadi tutakapoipumzisha CCM, bado tupo tupo sana
 
Daah wameweka vifurushi ili wasikatike kwa Wazee wameweka gharama kubwa kama vile hakuna kitu wamechangia kwenye wenye umri mdogo ambao magonjwa ni kwa kiasi kidogo gharama ni ndogo yaani Serikali inaanzisha kitu kama Kampuni sio kutoa huduma ni faida kwa kila wanachoanzisha...
 
Sijui Tunaelekea wapi kama Taifa! tokea mama makinda amekuwa mwenyekiti wa bodi ndio shida zoote hizi zimeanza! MAKINDA amekuwa mbunge tokea 1975 sasa atajuaje shida zetu mtu kaishi maisha ya raha

mtanzania maskini anayehangaika kupata mbolea mifuko miwili atawezaje lipa hizi gharama? Rais Samia lione hili
Kuna haja ya kufanya research kuhusu kipato cha mwananchi mmoja mmoja
 
Hapo uzazi wa mpango hakwambii mtu mwenyewe utajiongeza,shule za vidumu michango kkbao ukienda private school fees juu ukija kwenye afya hakuna tena utelezi wa 50400,lazima ujiunge safe plan lah unataka watoto wengi utakunywa sana miarovela na miarobaini
 
Sijui Tunaelekea wapi kama Taifa! tokea mama makinda amekuwa mwenyekiti wa bodi ndio shida zoote hizi zimeanza! MAKINDA amekuwa mbunge tokea 1975 sasa atajuaje shida zetu mtu kaishi maisha ya raha

mtanzania maskini anayehangaika kupata mbolea mifuko miwili atawezaje lipa hizi gharama? Rais Samia lione hili
Watoto wake wenyewe hawajui shida hizi haumii Kwa lolote
 
Back
Top Bottom