Hilo swali ndilo wengine tunajaribu kulijibu kwa kuonyesha mapungufu ya CHADEMA. Tatizo mashabiki wengi wa CHADEMA siasa walianza mwaka 2010 wakati Slaa akiwa mgombea Urais. Wao macho yao yote yako 2015 bila ya kujali baada ya 2015 kwa CHADEMA hii kitatokea nini.jaman mi naombeni mnijuze tu.ina maana chadema haina mapungufu hata kdogo?
Ebu fafanua vizuri wabunge wamekopeshwa na bunge milioni 90 kwa manunuzi ya magari yao sio benki...halafu hapo hapo wabunge wamekopa benki mikopo binafsi na mdhamini wao ni bunge, kuna wengine wamekopa milioni 30 wengine milioni 50 na malipo yao kwenye mikopo yao inatoka na kodi zetu, nikirudi kwenye hoja ya Kigarama, mbunge wa Chadema ambae anatembelea gari la bei ndogo ni John Mnyika, Toyota Vitz.
Ni vema kijadili vitu vya ukweli kuliko kuleta ushabiki usio na tija. Kama kweli mboye kalichukua gari la kiongozi wa upinzani bungeni basi atakuwa amewaadaa wana CDM wenzake. Nasikia mpaka posho wanasaini kuzichukua kimya kimya nyinyi wana CDM wengine mnadanganywa wala hamjielewi. Bado miaka 3 kabla ya uchaguzi mpaka leo hakuna hata halimashauri moja iliyo chini ya CDM inayotoa elimu bure sijui mtawaambia nini wananchi mwaka 2015.
Ni vema kijadili vitu vya ukweli kuliko kuleta ushabiki usio na tija. Kama kweli mboye kalichukua gari la kiongozi wa upinzani bungeni basi atakuwa amewaadaa wana CDM wenzake. Nasikia mpaka posho wanasaini kuzichukua kimya kimya nyinyi wana CDM wengine mnadanganywa wala hamjielewi. Bado miaka 3 kabla ya uchaguzi mpaka leo hakuna hata halimashauri moja iliyo chini ya CDM inayotoa elimu bure sijui mtawaambia nini wananchi mwaka 2015.
Mkuu lazima utakuwa na mtindio wa akili, yaan uwezi fikiri hata kidogo, kwenye 145m kuna 60 ngapi? au kwenye 200m ya vx/Gx v8 kuna 60 ngapi? 3 na kuenelea, hivo ni economical.
Pia hata wakikubali kununua corrola utamambia kwa nn wasinunue pikipiki? na wakinunua pikipiki utambia wana2mia pesa vibaya, kwa nn wasinunue baiskeli na mwendelezo unakuwa hivo.
Hapo kwenye red, hivi kuna mbunge ambaye analipiwa marejesho ya mkopo (loan instalments) kwa fedha za walipa kodi ??
Duh !!, JF kuna kazi kweli kweli.
Nazungumzia "consistency" ya chama kwenye mambo wanayoyapigania wakati wa Kampeni. Kusema akili yangu mbovu hakuondoi ukweli kwamba hata hayo mashangingi ya CHADEMA yananunuliwa na kwa kodi za wananchi. Wewe hujui kuna baadhi ya wabunge kabla ya kuwa wabunge hata Baiskeli walikuwa hawana uwezo wa kununua.
Unajisahaulisha kwamba wabunge wote walipewa mkopo wa shilingi Milioni 90 na ofisi ya Bunge kwa ajili ya kununulia magari yao?
Nisome vizuri au inawezekana umerukia usichokijua...hao ulipo bold posho, mishahara, na viinua mgongo vya wabunge ni kodi zetu, sijui kama unafahamu mbunge akimaliza kipindi chake bunge anapewa zaidi ya milioni 40? Unadhani zinatoka wapi.
Mkuu Acha hadithi za sungura.Kweli watu wagumu kuelewa. Mtu kasema akishika nchi ndio atakataza vx na v8. Leo hajashika bado watu wanashikilia kauli.
Acha kufikiria kwa kutumia ma***** huko vijijini utaenda na Corolla au GX 100?
CHADEMA ilitoa hoja za msingi sana wakati wa Kampeni za Mwaka 2010 na zikakubalika na wananchi wa Tanzania.
Mgombea Urais wakati huo MH: Willbroad Peter Slaa na wagombea wa nafasi za Udiwani na Ubunge walikuwa wanatoa tuhuma kwamba serikali iliyopo madarakani inafuja fedha za wananchi kwa kununua magari ya kifahari aina ya Land Cruiser VX na V8 wakati fedha hizo zingetumika vizuri zingeleta maendeleo kwa wananchi. Katika kukoleza hoja hiyo ikaaminishwa kwamba kama CHADEMA ikishika madaraka basi magari hayo ya kifahari yatauzwa na madala yake yatanunuliwa magari madogo ya bei rahisi.
Slaa alikuwa anasema aina ya magari yanayotumiwa na Wakuu wa Wilaya na Mikoa thamani yake ni sawa sawa na gari moja kujenga Zahanati Nne vijijini. Wanachi waliambiwa kwamba magari hayo yatauzwa na fedha itakayopatikana itatumika kuwekeza kwenye Elimu.
Baada ya uchaguzi wa Mwaka 2010 viongozi wa CHADEMA hawatumii VX au V8 kwa matumizi ya kichama na yao binafsi, au thamani ya magari hayo imeshuka baada ya wao kuanza kuyatumia?
UKIKEREKA SEMA UPENDAVYO!!
Yaani mpaka nakuhurumia jinsi unavyotoa 'hoja'.
Iko hivi:-
Mshahara, posho, viinua mgongo, etc. ni malipo ya kazi ya Ubunge. Hivyo ni kama malipo yoyote ya mishahara ya wafanyakazi wowote wengine.
Hivyo, mpokeaji mshahara ana uhuru wa kutumia mshahara wake vyovyote anavyopenda (bila ya kujali pesa za kulipa mshahara zinatoka wapi), yaani kununua fenicha, kununua gari, kulipia marejesho ya mkopo, etc.
Kwa hiyo, unachosema wewe ni kwamba wabunge hawana uhuru wa kutumia mishahara yao wapendavyo !!! Yaani wakitumia mishahara yao kulipia marejesho ya mikopo, inakuwa issue !!!
Jiulize, wafanyakazi wa serikali huwa wanakopa?? Hivi wakikopa, wanaruhusiwa kutumia mishahara yao kulipia marejesho ya mikopo ??
Kwa wewe, ungesema wasitumie mishahara yao kulipia marejesho ya mikopo maana, hiyo mishahara yao ni pesa zetu za kodi !!!
Mkuu Acha hadithi za sungura.
Sungura(CDM) alisema, mkiniingiza shamba la zabibu( mkinipa Nchi), nikakula zabibu mbichi tu Kama Nina njaa(CDM hatanunua mashangingi).
Leo tu CDM wanakula zabibu za jana( mashangingi yaliyozeeka), wakipata nchi we fikiria mwenyewe itakuwaje,watakula zabibu za jana au za Leo leo?
Another lumpen ploetariat, mtu ambaye hajui kwamba serikali inaendeshwa na taratibu zilizowekwa na kuwa gazetted.hesabu yako imekaaje mimi navyo elewa siku kabla ya jana ni juzi,halafu nashukuru kwa utabiri wako kwamba umetambuwa kuwa wataongoza nchi.... watakuweje ..jibu subiri uone kwani kwa sasa kila mtu ananunuwa kivyake hana masharti yeyote hata akitaka kuwa na helkopta kama ndesa ni juu yake mafuta na spea dereva anakolipaki kila kitu atajuwa mwenyewe....
subiri uone wacha umbea kwa sasa hawajashika nchi