Mashangingi ya CHADEMA!!

Kweli nyani haoni kundule, sasa wakuu wa mkoa na wilaya kwani nao hawaendi vijijini?
 

mdau swala uliloliongelea ni muhimu..sema nasikia kisa cha serikali kununua sana ma land cruiser vx ni kutokana na mashrti ya mikopo na misaada tunayopewa na japan inatubana baadhi ya pesa irudi kule kutengeneza soko la magari yao
 
HILI LA CHIKU ABWAO NI MTUMBA (NI KAMA $30,000)



HILI LA MAREHEMU REGIA MTEMA (KAMA LA CHIKU ILA RANGI TOFAUTI)



HAYA YA SERIKALI NDIO V8 YA TZS 200,000,000


Hizo bei zako ni za wapi? Tupe jina la kampuni waliponunua hayo magari kwa hizo bei mkuu.
 

usilete porojo zako mama!
 
Dr Slaa na Josephine wakiwa Arusha wanapewa posho ya malazi sh. 250,000/- kila mmoja wakati wanalala chumba kimoja

Nani anawalipa? Wewe huwezi kuelewa kazi anayofanya Dr Slaa na Umuhimu wake..

JK analipwa kiasi gani?
 
kwa kweli mimi ni mwanachadema damu lakini kuna mahali hata nyie wachangiaji wenzangu tuwe tunaongea ukweli,KUHUSU KUTUMIA MAGARI YA KIFAHARI VIONGOZI CHADEMA HIYO TABIA WANAYO,kwa wale wanaofuatilia siasa za ndani kumbukeni siku ujumbe wa chadema ulioenda ikulu kuwasiliana na rais,haraka haraka niliona vx kali sio tu vx ili ina ubora wa kipekee wa wale viongozi,VX aliyokuwa kapanda mbowe sio ya kitoto hata mil 80 sidhani kama utaweza kuipata ,pili wabunge wengi wa chadema wana magari ya kifahari ingawa kuna wachache sana wanayakawaida,ANGALIA GARI YA REGIA MTEMA ALIYOPATANAYO AJALI,mtoto ana miezi kadhaa bungeni anatembelea vx tena viti maalum ,wakati baba yake hapo tabata tunamjua,KWELI KWA HILI VIONGOZI WA CHADEMA BADILIKIE TUMIENI RAV 4 NI GARI NZURI ,NGUMU,INAENDA BARABARA ZOTE MIL 20 TU INATOSHA BADALA LA HAYO YA MIL 80
 
Mie utata wangu upo kwenye huo mkopo wa M90; Swali langu la msingi ni kwamba,
Kulingana na utaratibu wa utoaji mikopo huambatana na Riba ktk mchakato wake wa malipo sasa Je ni Riba kiasi gani wabunge hawa wana lipa kufuatia mkopo huo wa m90?
(b)Kama hakuna Riba, Je wachangiaji wenzangu wanaweza kukubaliana nami kuwa Wabunge wetu nao ni Wanafiki kwa kupinga matumizi mabaya ya pesa za serikali wakati nao ni wafujaji?
(c) Na kama Riba ipo Je makato yake yanashabihiana na kipato akipatacho Mbunge huyo?
 
ka makubwa na madogo yana nafuu.ama kweli ww umenyimwa elimu na ndugu zako magamba hata huelewi nn maana ya serikali na utawala bora,usiweke hoja yoyote ile inayohusu mambo ya chadema maana unaonekana unazidiwa akili na zezeta kama LUSINDE(MB MTERA) ,hawa jamaa wa cdm wana watetea watanzania wote japo wao wanamali zao wala sio lazma eti kwa sasabab wanattea bac wao wawe maskin.ww umezoea na unaona raha kukaa na magamba wanaoficha ukweli wa utajiri wa mtanzania na raslimali zetu.kuanzia leo umeelimika
 
Kazi ipo! Kwahiyo kununua Gari lako binafsi kuwe kuna sera kitaifa?MmmmmH!

Hivi magari yanayotumiwa na CHADEMA ni ya pesa binafsi au ruzuku, Misaada toka kwa SABODO na zile zilizochangishwa kwa bakuli kusaidia kampeni? Nafikiri kama ndizo hizo, basi nazo ni kodi za wananchi au mnasemaje wadau wenzangu?
 

Nasikia uchaguzi wa 2015 watakuwa na madari maalum ya kampeni yenye rangi ya chama? tufahamishane jamani . Nami mdhamini manake sisi hatuna pesa ndiyo maana tunatembeza bakuli wakati wa kampeni.
 

Tusaidiane kutafakari maandishi mekundu hayo jamani, unaweza kuwa umelala lakini mwandishi akakuamsha.
1. Ni kweli thread zinazohusu mambo ya CHADEMA haziruhusiwi humu JF?
2. Viongozi wa CHADEMA wana mali zao, wamezitoa wapi?

"CHADEMA SI CHAMA CHA KIDINI, ILA WATU WAKE NDO WANA UDINI BHANA-MTEI"

 
siasa mchezo wa kombolela...wewe unajificha ikifika zamu yako na wenzako wanajificha wewe unawatafuta...! siasa ni kama wanyama waitwao NYANI.

wanyama hawa huwa hawaoni makalio yao bali kuishia kuyacheka ya wenzao.......! POLITICS IS THE GAME OF DIRTIEST..!
 
Nakumbuka Slaa alitaja zaidi ya mara moja kuwa bei ya gari moja (hayo unayoyapigia kelele) ni zaidi ya shilingi milioni 200, je, kuna gari lolote CDM imelinunua kwa bei hiyo, ili hoja yako ipate uhalali wa kujadilika?

Halafu tofauti ni kuwa haya ya wabunge wanayamantain wenyewe na sio serekali .
 
Naomba nitoe elimu kidogo kwa watu maana unaweza kuanzisha thread hata hujui tofauti ya magari. Kuna tofauti kubwa sana kati ya toyota VX ya kawaida na VX V8. Kwa yule asiyejua magari kabisa VX V8 unaweza kuitambua kwa kuangalia taa zake zimetoka kwa nje kidogo. Hayo ni new model ya VX ambayo yameanza kutengenezwa around 2009 ambayo serikali inanunua mapya kabisa gharama yake ndio haipungui millioni 200 za kitanzania ingawa yapo used from Japan. hayo unayoayaona ambayo si chadema tu wanayo hata wafanyabiashara na wafanyakazi wengi wanayo ni old model chini ya 2004 ambayo mengi yanapatikana kama mitumba na ukitazama kwenye webstie nyingi i.e. www.tradecarview.com utaona bei zake ni ndogo sana hayazidi $ 30,000. nimeattach picha na gharama zake kwa msaada zaidi

Hizi ndo VX za kawaida

[TD="class: box5"][/TD]
[TD="class: box1"]

[h=5] Toyota Land Cruiser [/h]4,700 cc VX-LTD
GH-UZJ100W, Automatic
Hearte International Japan Co., Lt ...
(0)
JAPAN
ID:531973-ATS0001-151896018103040897

[/TD]
[TD="class: box_year"]2002
[/TD]
[TD="class: box2"]62,000 km
[/TD]
[TD="class: box3"]

[/TD]
[TD="class: box4"]Right
[/TD]
[TD="class: box6"]US$24,752
¥1,974,000

[/TD]



VX V8


[TD="class: box5"][/TD]
[TD="class: box1"]

[h=5] Toyota Land Cruiser [/h]4,600 cc CBA-URJ202W, Automatic
Murakami International Japan
JAPAN
ID:1189750-111106072609

[/TD]
[TD="class: box_year"]2011
[/TD]
[TD="class: box2"]5,000 km
[/TD]
[TD="class: box3"]

[/TD]
[TD="class: box4"]Right
[/TD]
[TD="class: box6"]US$119,122
¥9,500,000

[/TD]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…