Mashambulizi dhidi ya wageni yaaendelea nchini Zambia

Mashambulizi dhidi ya wageni yaaendelea nchini Zambia

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,297
Polisi nchini Zambia wamesema watu wawili wamechomwa moto mjini Lusaka katika vurugu ya ubaguzi wa wenyeji dhidi ya wageni.

Watu Zaidi ya mia mbili na hamsini wamekamatwa baada ya maduka mengi yanayomilikiwa na wanyarwanda kuvamiwa. Uvamizi huo ulitokea baada ya wanyarwanda kushutumiwa kuua watu na kutumia viungo vyao kuvutia wateja.

Padre Charles Chilinda ameiambia BBC kuwa kanisa lake linafanya jitihada zote ili kuweza kuwasaidia wahanga ambao wamekwenda kuomba hifadhi kanisani.

"Kitu ambacho tunaweza kuwapa ni kwamba watakuwa na usalama wa kutosha kuwa hapo,tutaenda kuwaangalia na kuwaeleza kuwa hawa sio wazambia ambao wanagombana nao.hali hii haikubaliki, kila mtu aliyepo katika ardhi ya Zambia analindwa na katiba ya Zambia. Ni jukumu letu kudumisha Amani na tushirikiane katika kulitokomeza hili"

Chanzo: BBC
 
gettyimages-522422774.jpg
 
Tatizo kubwa linalowasumbuwa ni wivu na tamaa. Lusaka maduka makubwa ya jumla 60% yanamilikiwa na wanyarwanda ongezea maduka ya wafanyabiashara kutoka India, Pakistani, Tanzania au Lebanon. Unakuta maduka machache yalio baki ndio yanayomilikiwa na wazawa wa Zambia. Wa Zambia waache ubaguzi wafanye kazi siku ikitokea wanyarwanda wakafukuzwa Zambia itakua kama Tanzania iamue kuwafukuza wahindi wote. Uchumi wa taifa utatetereka sana.
 
Mkuu cha kujiuliza hapa, mbona unasema mjini Lusaka kuna wafanya biashara kutoka Tanzania, India, Pakistan nk hao mbona hawavamiwi why pickon Rwandese - kuna tatizo si bure.

Halafu hili la kusema Wazambia ni wavivu sikubaliani nalo, mbona miaka ya nyuma maduka mengi mjini Lusaka yalikuwa yanamilikiwa na Wazambia, Wazungu na Wahidi/Lebanon mbona hatukuwahi kusikia yamevamiwa na Wazambia - bila ya ku resolve underlying problem baina ya Wazambia na Wanyarwanda mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi - hayo ni maoni yangu.
 
Wazambia ni wavivu waliowaamsha ni Wagenihasa katika kile kipindi cha kamwala market iliyokua na Watanzania na wakongo wengi wakaleta fitina wakawaondoa Wageni katika lile soko ikabidi Watanzania Wakiunge na kuomba Eneo Commesa ndio mpaka sasa wapo pale wazambia wanamuogopa sana Mhindi kuriko maelezo hawawezi fanya kitu kwao au wasomali walijaa Mandevu na maeneo mengine...
 
still wamelala kodi kwa Wazambia ipo chini sana kwa bidhaa nyingi toka nje tofauti na Nchi zingine...wanaoongoza kwa uvivu ni South Africa..Zambia ikifuatiwa na Botswana..
 
Wabongo bana, yaani mijitu mnaona ni sawa uovu unaotendeka Zambia eti kwasababu inawatendekea Wanyrwanda pekee yake. Miafrika tuna laana, bora hata Wazungu wanegtukalia na kutunyoosha kwa miaka zaidi. Naona bado tunaendelea ku-evolve.

Iwaingie akilini kwamba hawa Wazambia walipora hadi maduka ya wazawa, yaani Wazambia wenzao....
 
Kaka Zambia wapo wafanyabiashara wengi na sio wanyarwanda peke yao,ila hilo limewatokea wafanya biashara wa kinyarwanda baada ya kushutumiwa kuwaua watu(wazambia) na kufanya viungo vyao kama kivutio cha biashara zao.
Sasa kama kweli ndo iko hivo we ulitaka wazambia wafanyeje labda ili kupoza machungu yao.
 
Hukumu ya halaiki sio haki, ninaamini Zambia kuna mfumo wa sheria na katiba.
Kuanza kuwasaka Wanyarwanda na kuwaua na kupora mali yao haifai kabisa halafu mbovu zaidi nyie watu wa Nyerere mnashabikia, yaani hayati Kabarange akifufuka leo ataomba afe tena ili asiishi kushuhudia Watanzania wa leo.
 
sio wanyarwanda tuu ukijichanganya hata Mtz wao wakitaka kukupora wanatumia mbinu hiyo izo sehemu ni hatari sana yanapotokea matukio kama hayo hata kupita mimi nilihisi haya yanaweza kutokea maana Trafki wao wanawanyanyasa sana madereva wa Kitanzania wa truck...ni chuki tuu imejengeka ya kipuuzi..
 
Back
Top Bottom