Mashamba ya kulima Ruvu

kutoka dar es salaam hadi Ruvu kwenye hayo mashamba kuna umbali gani ?wanajamviii!
 
Niliona umegusia sana mpunga ndio maana nikauliza. Na nyanya ni sehem gani zinakubali??

Na mashamba yake lazima ukodi kwenye chama?? Bei shi ngapi?

Chama ni mpunga tu. maeneo ya jirani ndo mazao mengine yanalimwa.
Bei inategemea na mtu,wapo wanaoomba laki hadi laki mbili kwa mwaka. Wengine wanakodisha kwa msimu,unalima,ukivunaunakabidhi shamba
 
Mkuu, kuna mashamba ya kulima mbogamboga mm nahitaji
Pia naomba namba Zako

iPhone 6s
 
Jamani nahitaji shamba kibaha au Ruvu kwa ajili ya ufugaji?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Habari mtoa mada.Mie nipo Mapinga bagamoyo nipo interested na kilimo hicho cha umwagiliaji na mara nyingi nimekuwa nikijiuliza namna ya kupata shamba mto Ruvu.

Hofu yangu kubwa imekuwa ni utapeli wa watu wa bagamoyo maana vilio vya waliotapeliwa ni vingi. Je naweza kupata shamba la umwagiliaji msimu huu lengo langu ni mahindi niuze mabichi kabla ya Dec.
 

Utapata mbona? Wanaolia wengi walienda kwenye mpunga,na hapo kama unahitaji ndo kuna ka ugumu,maana wengine anakueleka kwenye shamba la mtu.Na kama mtu uliepania kulima,ukiona deal la maana lazima uingie,ila kuna haja ya kuwa makini. Wengine pia ni walionunua ardhi,hao nao inahitaji kwanza mazungumzo hasa na wazee wa kijiji maana asilikia kubwa wanayaelewa sana maeneo hayo.

Sasa wewe kwa kukodi na kufanya shughuli zako,mbona rahisi?!
 
Mkuu mavuno gunia ngapi wastani kama umefata taratibu vizuri na return inakuaje baada ya kuuza pia kuna gharama zingine zozote nje ya iyo 442,000 adi kuvuna?....

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hayo maeneo ni CHAURU?

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Dunia imebadilika kila kona, hakuna uaminifu sasa lakini baadhi ya watu wa mkoa wa Pwani wengi sana hasa Maeneo ya Wilaya za Kibaha na Bagamoyo ni watapeli na hawaogopi kudhulumu mtu. Wanauza mashamba mara mbilimbili au ambayo sio ya kwao.

Hawa watu hawataki kufanya kazi ila wanataka pesa ya kuongeza wanawake. Maeneo ya Ruvu kuna utapeli sana huwezi tuma pesa kwa mtu akafanya mlivyo ahidiana bila kupiga panga, hawajali kama huo mradi utakufa. Kama alivyosema mleta mada ukitaka kulima basi uende ukasimamie kuanzia siku unalima kwa trekta, kupanda, hadi unavuna.

Ukisema utume pesa umeumia. Kilimo kinahitaji pesa na ufuatiliaji wa karibu sana.
 
Mkuu mavuno gunia ngapi wastani kama umefata taratibu vizuri na return inakuaje baada ya kuuza pia kuna gharama zingine zozote nje ya iyo 442,000 adi kuvuna?....

Post sent using JamiiForums mobile app

Ni matunzo yako mkuu,ndo maana nikasema kama una hela ya kuungaunga bora ujipange kwanza.Ukihudumia shamba lako vizuri,unaweza pata hadi 80.Nasikia aliwahi kupata mtu 92.Ukihudumia vibaya,hukosi 20.

Gharama nyingine zipo.Kuvuna,wanatumia machine,na siku hiyo hiyo unasafirisha mpunga wako. Kuvuna ni laki 3.Kutumia vibarua wa kawaida,itachukuwa mda na gharama zinatofautiana kama 50 elfu tu.Ila hawa itachukuwa hadi siku 3
 
Mkuu hayo maeneo ni CHAURU?

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app

Maeneo yapi unayoyazungumzia mkuu? Kama ni kilimo cha mpunga,ndio,ni CHAURU,kama ni matunda na mbogamboga,havilimwi CHAURU
 
Pia nilisikia kuna maghala ya kijiji sijui ni chama ukivuna unaweza kulipia na kutunza uko mpunga wako adi utakapo taka kuuza...ili limekaaje mkuu??

Post sent using JamiiForums mobile app
 

Wa kwanza niliewambia na kutoa number zake za simu,tayari keshakamatwa,na kama unavosema wengine ni wajinga.Katapeli,hela kaenda kuongezea mke wa pili.Kama humu yupo aliyewahi kutapeliwa nae(Anaitwa Abdalla Saidi Ndandike)maarufu kama Dulla,na ana ushahidi wa kupeana nae hela,ajitokeze kituo cha Polisi MLANDIZI akamuone,wamalizane.Ila atamlipa nini!Manaa leo anakabidhi hati za nyumba na viwanja.

Wengine wapuuzi tu,wanapenda hela za bure,na wanajua hapo kwenye mpunga msimu wa kulima ndo na wao msimu wa hela unaanza.Ila huyu,amewaliza watu aise!
 
Pia nilisikia kuna maghala ya kijiji sijui ni chama ukivuna unaweza kulipia na kutunza uko mpunga wako adi utakapo taka kuuza...ili limekaaje mkuu??

Post sent using JamiiForums mobile app

Mkuu,siwavunji moyo hapa nawaonjesha tu changamoto za huku,na mwenye swali asisite kuniuliza,ili siku yakikukuta ukumbuke.Ghala lipo na ni la chama.Hivyo,ukivuna unaweza kutunza mpunga wako mpaka utakapoamua kuuza.

Gharama za kutunza,nilisikia ni 2,000 kwa siku(japo uhakika sina,mpaka niulize),ila nimesikia kipindi furani hao hao tunaowasema walivunja na kuiba mpunga wa watu.Sasa mpaka mwizi atafutwe,kesi iende,ulipwe ni leo?

Mi naonaga tu uuzie shamba hapo,wanaonunua wanaanika wenyewe,au utafute sehemu kijijini uupeleke uombe hifadhi uwe unaanika mwenyewe,ukimaliza toa shukrani zao,safirisha,uza au koboa mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…