Wow asante sana huwa nafikiria kulima vitunguuHabari zenu.
Nimewahi kuuliza swali kuhusu mashamba ya kulima Ruvu,nikabahatika kupata maelezo,nikaenda na nimeanza.
Lakini,uzi ulioniongoza nimeutafuta sijauona,ila nimetumia muongozo niliopewa.
Ruvu kwa kweli kama una nia ya kulima ni pazuri,maji yapo ya uhakika,mito ni miwili,Ruvu na Msuya.
Pamoja na hayo lakini kuna changamoto kubwa mbili:
1.Usimamizi unahitajika na kama umeamua,hamia au tafuta mtu wako wa karibu.Wajanja huku ni wengi,tena bora niwaite wahuni.Ukituma hela kwamba kazi utafanyiwa utaishia kulia tu.
2.Upatikanaji wa mashamba:
+255 658 899 195.Kuna mtu siku za nyuma alitoa hii number kwamba atafutwe mwenye nayo,atawapa maelezo.Hakika aliyepost hii number wanashilikiana asilimia mia.
Jamani,mtu kama yule unawezaje kuomba watu,walioacha familia zao,wampelekee pesa,awatapeli?
Nawasihi sana,nimeona mengi.
Kama unataka shamba huko,kuna sehemu mbili.Kuna kilimo cha mpunga,kinafanywa na shirika,huyu anawapeleka watu na kuwauzia mashamba ya watu,mwisho wa siku mnaishia kugombana na hela unapoteza.Anauza shamba lililopandwa mpunga kwa laki 5,na lisiti atakupa.Za kughusho,mwisho wa siku unakumbana na mwenye shamba sasa.Kama umeamua kulima huko,nenda ofisini,gharama za ofisi ni 442,000(pesa ya kukodi shamba kwa mwaka,unalimiwa,unapewa maji,mbegu ya mpunga ni ya kwao unauziwa kiasi kidogo si kama madukani nje,mbolea ni za ruzuku,ukihitaji utapewa kwa gharama nafuu)Ukipita pembeni shauri yako.Labda uonane na mwenye shamba mtajuana wenyewe lakini kupitia mtu mwingine utalia.
Mashamba mengine unakodi kwa watu,na kama utakodi la hivo,hakikisha mnaandikishana kwenye uongozi wa kijiji.Tofauti na hapo,utajua mwenyewe.
Ukihitaji maelezo zaidi,nambie,kama kukusindikiza ntakusindikiza,ugjaramie usafiri.Ila,kama hujajipanga kulima,usiharibu hela yako.
Nimependa namna ulivyowasilisha ujumbe wako. Haina kubembelezana wala kupakana mafuta kinafki, safi sana
Wow asante sana huwa nafikiria kulima vitunguu
Vipi mihogo na mahindi, vinalimwa hapo hapo ?Jiandae,na ukalime kweli(usimamie)sio uambiwe tuma hela kesho tunavuna njoo na gari huku mara ya mwisho watu kufika shamba ni siku ya kumpanda.
Katika swala la kuwekeza huwa sinaga kutumana ili hasara ikitokea nisiwe na wa kumlaumu na faida ikipatikana nijisifie mwenyewe,Jiandae,na ukalime kweli(usimamie)sio uambiwe tuma hela kesho tunavuna njoo na gari huku mara ya mwisho watu kufika shamba ni siku ya kumpanda.
Vipi mihogo na mahindi, vinalimwa hapo hapo ?
Hayo mahindi yanalimwa msimu wa mwezi gani au wanafanya umwagiliaji ?Mihogo sijaona,mahindi yapo yanapandwa kwa wingi.Kwa sababu ya uhakika wa maji,mbogamboga na matunda ndo vinavyolimwa kwa wingi,na mpunga
Hayo mahindi yanalimwa msimu wa mwezi gani au wanafanya umwagiliaji ?
Unaweza kutoa direction labda tunaweza kwenda kutembea huko siku moja mkuu. Unapanda magari ya wapi ?Pale kilimo si cha msimu ndugu.Unajua mito inavyotema,maji yanakaa ardhini mda mrefu,na ardhi ya huku inatwamisha maji,hivyo bado unyevunyevu wa kuosha upo,na pia kwa vile maji yapo,ukihitaji unamwagilia.Kiwe tu kilimo ambacho unahitaji mazao mengi,kwenye eneo dogo.Maji na dawa na mbolea ni mhimu
Unaweza kutoa direction labda tunaweza kwenda kutembea huko siku moja mkuu. Unapanda magari ya wapi ?
Kipawa, DSMNdio,naweza.Ila ningependa unambie utakuja ukitokea pande zipi.
Kipawa, DSM
PoaPanda gari za Mbezi(Mbezi ya Kimara),ukifika Mbezi kuna gari za kwenda Mlandizi.Ukifika nipigie
Ahsante mkuu. Namba ya ofisi?Habari zenu.
Nimewahi kuuliza swali kuhusu mashamba ya kulima Ruvu,nikabahatika kupata maelezo,nikaenda na nimeanza.
Lakini,uzi ulioniongoza nimeutafuta sijauona,ila nimetumia muongozo niliopewa.
Ruvu kwa kweli kama una nia ya kulima ni pazuri,maji yapo ya uhakika,mito ni miwili,Ruvu na Msuya.
Pamoja na hayo lakini kuna changamoto kubwa mbili:
1.Usimamizi unahitajika na kama umeamua,hamia au tafuta mtu wako wa karibu.Wajanja huku ni wengi,tena bora niwaite wahuni.Ukituma hela kwamba kazi utafanyiwa utaishia kulia tu.
2.Upatikanaji wa mashamba:
+255 658 899 195.Kuna mtu siku za nyuma alitoa hii number kwamba atafutwe mwenye nayo,atawapa maelezo.Hakika aliyepost hii number wanashilikiana asilimia mia.
Jamani,mtu kama yule unawezaje kuomba watu,walioacha familia zao,wampelekee pesa,awatapeli?
Nawasihi sana,nimeona mengi.
Kama unataka shamba huko,kuna sehemu mbili.Kuna kilimo cha mpunga,kinafanywa na shirika,huyu anawapeleka watu na kuwauzia mashamba ya watu,mwisho wa siku mnaishia kugombana na hela unapoteza.Anauza shamba lililopandwa mpunga kwa laki 5,na lisiti atakupa.Za kughusho,mwisho wa siku unakumbana na mwenye shamba sasa.Kama umeamua kulima huko,nenda ofisini,gharama za ofisi ni 442,000(pesa ya kukodi shamba kwa mwaka,unalimiwa,unapewa maji,mbegu ya mpunga ni ya kwao unauziwa kiasi kidogo si kama madukani nje,mbolea ni za ruzuku,ukihitaji utapewa kwa gharama nafuu)Ukipita pembeni shauri yako.Labda uonane na mwenye shamba mtajuana wenyewe lakini kupitia mtu mwingine utalia.
Mashamba mengine unakodi kwa watu,na kama utakodi la hivo,hakikisha mnaandikishana kwenye uongozi wa kijiji.Tofauti na hapo,utajua mwenyewe.
Ukihitaji maelezo zaidi,nambie,kama kukusindikiza ntakusindikiza,ugharamie usafiri.Ila,kama hujajipanga kulima,usiharibu hela yako.