Mashamba pori, kwa tajiri sawa Iia kwa maskini utanyang'anywa

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Nchi hii ina malaki ya maeneo ya kilimo.Sasa ukienda karibu serikali zote za vijijini wakakupa shamba wanakwambia hilo shamba liendelee ndani ya miaka miwili nje ya hapo litachukuliwa apewe mwingine.

Lakini ukipita Bagamoyo hadi Tanga, pita Moro road hadi Mwanza, na kwingineko Tanzania kila pori potential ukiuliza utaambiwa hapo tajiri flani ana hekari 1000, hizo ni za mwanasiasa flani anazo 5000, cha ajabu ni pori tangu enzi za vita vya majimaji. Ila wewe usiye na kitu kila siku unatishiwa kunyang'anywa hata kama huko ndani kabisa unapishana hadi na tembo.

Hii kitu kifanyiwe kazi na kama ni sheria ile kote na kwa wakati.Mfano kuna muwekezaji anashamba heka zaidi ya 20000 mkoa wa pwani ambapo mwanzo ilikuwa mali ya serikali, pori kubwa hata unaweza kukutana na nyayo za simba kwa muda mrefu tu. Wananchi wa hapa kazi na ari mpya walipojaribu kuanza kulima na kuendelea ikaonekana ni uvamizi mkubwa.
 
Back
Top Bottom