Verse 1
Uko wasiwasi mtu bila nafsi/ umeajiriwa shirika la mtu binafsi.
Sina wasiwasi mtu mwenye nafsi/ sijaajiriwa nimeajiri yangu nafsi.
Poleni mishahara imejaa makato/
Biashara mjini ndo zimejaa mapato.
Poleni ajira itakulinda toa vyeti/
Sihitaji kulindwa mi sio mtoto wa geti.
Tokeni ajira ni mpaka wa akili yako/
Mpaka ufukuzwe kazi ndo ugundue kipaji chako.
Ajira ya mkeo chini ya boss /
We housegirl pekee nchini anakuita boss.
Sivai tai siikatai utamaduni wangu mi ni kuuliza why.
Elimu bongo imekosa plani ya pili/ kosa la pili haufundishwi kuwa tajiri.