Mashairi ya Wimbo Lunchtime wa Marehemu Gabriel Omollo na nasaha zake kwa jamii ya sasa

Fyafyafya

Member
Nov 30, 2017
53
187
sasa ni lunchtime
tufunge makazi
twende kwa chakula
tuje tena saa nane

wengine wanakwenda
kulala uwanjani
kumbe ni shida ndugu
njaa inamwumiza

wengine wanakunywa
soda na keki
huku roho yote
kwa chapati na ng’ombe

na wengine nao wazunguka maduka
huku wakijidai
wanafanya window shopping

kufika mwisho wa mwezi
uwanja thire mundu
ukiona anayelala
pia asiye na kazi

wamekwenda wote
kula hotelini
wengine kwa biriani
wengine kuku na wali

watu wa Industrial Area
watoroka maharagwe
waenda hotelini
kwa chapati na ng’ombe

na wengine nao
wale mishahara juu
siku hiyo wote
kwa hoteli za wazungu

kumbe shida ndio hufanya
mtu kulala chini ya miti
kumbe shida ndio hufanya
mtu kung’ang’ana na maharagwe
kumbe shida ndio hufanya
mtu kuonekana kama mtoto
nimeelewa eeh, nimeelewa oh
nimejua kumbe ni shida oh
nimeelewa eeh, nimeelewa oh
nimejua kumbe ni shida oh

kumbe shida ndio hufanya
mtu kulala chini ya miti
kumbe shida ndio hufanya
mtu kung’ang’ana na maharagwe
kumbe shida ndio hufanya
mtu kuonekana kama mtoto
nimeelewa eeh, nimeelewa oh
nimejua kumbe ni shida oh
nimeelewa eeh, nimeelewa oh
nimejua kumbe ni shida oh

Huu ni miongoni mwa nyimbo nyingi ambazo hazichuji na ujumbe wake unagusa kila mtu. Wimbo wa karne hiyo ila bado unamashiko enzi hizi.

Huu wimbo unamaanisha kuwa Pesa ni Kila kitu. Huna Pesa basi utakuwa wa maisha ya chini yaani fukara na taabu tu.

Katika wimbo huu; Mrehemu Gabriel Omollo anatwambia kuwa watu huishi maisha ya chini ila si kwa matwakwa yao au wanavyopenda wao ila ni hali duni ya maisha. Katika ubeti usemao

"wengine wanakunywa
soda na keki
huku roho yote
kwa chapati na ng’ombe"

Maana yake nini: Nikwamba watu wanakula chakula duni pasipo raha ya moyo. Wanakula tu ilimladi tumbe lijae tu na kesho ifike au siku iishe. wanakula chakula hicho duni huku mioyo yao ikifikiria nyama; wali; samaki; matunda n.k. Sasa wafanyeje, hamna namna!

"Pia katika ubeti wa pii

wengine wanakwenda
kulala uwanjani
kumbe ni shida ndugu
njaa inamwumiza"
Hapa anajaribu kutuonesha na kutudhihirishia ule msemo wa sasa wa " Kupambana na hali yako" Kwamba kila mtu na maisha yake. Anasema kuwa kuna watu wabapitisha mchana deshi; yaani mchana hawali chakula kutokana na kipato duni au ukali wa bajeti. Nahapo haijarishi kazi gani unayoifanya ila wewe mchana huli chakula.

Ndio; hata leo tunaona watanzania wengi wakiw hali chai hasubuhi na wengine wakiwa hawali mchana. Yaani wanasema kupiga pasi ndefu.

Ubeti wa tatu anasema:

"na wengine nao wazunguka maduka
huku wakijidai
wanafanya window shopping"

Haswaaa! Hii ndo ile defense mechanism ya ule usemi usemao:" Mtembea bure si sawa na mkaa bure." Watu ambao hawana kitu huwa wazururaji sana. Mtu ambae hana mbele wala nyuma huwa mjuaji wa kila mtaa ndani ya mji anamoishi. Tena atajifanya kuwa anajuwa historia ya kila tajiri hapo mtaani kwao au wa sehemu anayaokaa maana hana kazi; hana shughuli yoyote.

Kwa mfano jijini Dar es salaam; si kitu kigeni kukuta mtu akizurura mwenge nzima kwa mguu; mara yupo Mlimani city na anakatiza maeneo ya saveyi chuo kikuu hadi ubungo; anaenda mara sinza; tandale ; huyo manzese; magomeni na baadae akaishia Mburahati. Hapo anakuwa akitembea kwa mguu ilitu siku iishe na pengine anaweza kutana na zari la menthali kama waseavyo mtembea bure si sawa na mkaaa bure.

Beti hizi:

"kufika mwisho wa mwezi
uwanja thire mundu
ukiona anayelala
pia asiye na kazi

wamekwenda wote
kula hotelini
wengine kwa biriani
wengine kuku na wali

watu wa Industrial Area
watoroka maharagwe
waenda hotelini
kwa chapati na ng’ombe

na wengine nao
wale mishahara juu
siku hiyo wote
kwa hoteli za wazungu"

Mtunzi; marehemu Gabrel Omollo alijaribu kutuonesha kuwa watu hasa wafanyakazi huishi maisha ya furaha kama ta paeadiso ndani ya wiki ya kwanza mshahara umetoka.

Kwamba; Mshahara ukitoka tu ndo watu huansa kula vizuri. wale wa kushindia maharagwe na kulalia kisanvu/ Mbaazi sasa utakuta wamepika samaki; nyama. Kila siku ilikuwa ni ugali; basi kwa siku huzi za mshahara utakuta wakila wali.

Siku za mishahara ndo watu hunywa hata ka soda wengine bia. Wale wa chipsi mayai; chipsi kuku utawaona ndani ya wiki hii ya mshahara.

Sasa wiki ya pili hadi ya tatu na ya nne hapo ndo kiama sasa. Watu wanaanza kuishi kwa msoto; wanageukia tena Maharagwe na ugali. wengine utasikia wakikwambia :" Mimi nakula ugali wa Dona maana ndo unavirutubisho sembe hamna! Sasa hapo utamkuta yeye ni nguna mchana na jioni. Anapiga dona hilo! Swali je ; nikweli ni hiari yake kula huo ugali? Au vyuma vimekaza! Anaukata?
Mtu huyo huyo akisikia ka sms M pesa kwenye simu yake. Mara paaa elfu 20. hapo hapo network inahama. Inasoma maili 70. Ataenda dukaninkwa mangi kuchukuwa kilo mchele na samaki wa 2000 au myama!!

Gabriel Omollo anatuambia kuwa; Mshahara ukitoka ndo watu husuza mioyo yao kwa kula vitu vizuuri ambavyo walikuwa wakivitamaani pindi hawana pesa japo kuwa hiyo furaha ni ya muda kidogo tu.


"kumbe shida ndio hufanya
mtu kulala chini ya miti
kumbe shida ndio hufanya
mtu kung’ang’ana na maharagwe
kumbe shida ndio hufanya
mtu kuonekana kama mtoto
nimeelewa eeh, nimeelewa oh
nimejua kumbe ni shida oh
nimeelewa eeh, nimeelewa oh
nimejua kumbe ni shida oh"

My take:
Ndugu yangu unaenisoma; unaishi maisha ulojipangia na ni standard?

Maisha yako hubadirika pindi tu upatapo hela?

Unasoend bila kuweka akiba ya kesho?

Unajutuma ili kesho uje kuishi maisha mazuri?

Je unajua kuwa kijana wa leo ndo mzee wa kesho?
 
Huu wimbo nilianza kuusikia kabla sijaanza ata primary,but now nina watoto wapo shule but wimbo uko vile vile,cha ajabu wimbo wa "zali la mentary" wa mh mbunge uneshakufa na kuoza wakati hauna ata miaka15!
 
Back
Top Bottom