Malenga Mwanakijiji na Waghani wengine Mnaoliamini Azimio Arusha,
Kwanza nawasabahi kwa Salamu ya Ujamaa na Kujitegemea. Ombi langu kwenu ni kuhusu tenzi na mashairi ya Azimio la Arusha. Tuko katika harakati za kutimiza unabii wa Malenga Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyebashiri kuwa mwisho wa siku tutarejea kwenye maadili ya msingi ya Azimio la Arusha. Sanaa ni njia mojawapo ya kuamsha kizazi hiki cha kifisadi ili kirejee maadili hayo hivyo naomba mtunge tenzi na mashairi ya kuhusu Azimio. Pia kama inawezekana wekeni tenzi na mashairi ya zamani kama yale yaliyohaririwa na Farouk Topan na Grant Kamenju . Mimi naanza kwa kudondoa beti hizi zilizoghaniwa kwa uchungu na mchumba wa Seti Benjamin Mpinga: Shujaa na Shahidi wa Azimio la Arusha:
Seti umeniacha upweke Lini tukae tucheke? Mbona hukuniachia pete Kifo chako kwangu teke.
Safari usiyorudi tena Wapi tutaonana? Mbona hukuniachia pete Faradha ya upendo hakuna.
Seti, Seti, nipe uso wako Nani atatekeleza ahadi zako? Mbona hukuniachia pete Azimio na kaburi lako.
Seti pendo la roho yangu Kifo ni amri ya Mungu? Mbona hukuniachia pete Upweke wanitia uchungu.
Machozi yanatiririka Kweli Seti umekatika? Mbona hukuniachia pete Kamwe ari isiyopimika.
Saa ya kurejea maadili ya msingi ya Azimio la Arusha kwa ari isiyopimika ni hii!
"Hata kidogo. Sikubali kurudi nyuma kama wale vijana wawili waliotuhadaa pale Momella" - Seti Benjamini Mpinga: Shujaa wa Azimio la Arusha masaa machache kabla ya kulifia Azimio
mkuu nilikuwa na'google seti benjamini shujaa wa azimio la arusha nione kama kuna article yeyote inayomhusu nikaangukia kwenye hii thread, nahisi hii thread ingefaa sana jukwaa la historia kuliko huku ambako watu wanahudhuria kwa mwaka mara moja.