Mashahidi wazidi kumkana Hans Macha kwenye kesi

Mashahidi wazidi kumkana Hans Macha kwenye kesi

Joined
Sep 30, 2014
Posts
95
Reaction score
47
KESI ya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Hans Macha inazidi kuchukua sura mpya, baada ya mashahidi aliowaleta mahakamani hapo kutoa ushahidi kuleta vioja. Vioja hivyo vilitolewa na mashahidi hao mbele ya Hakimu Devotha Kisoka, wakati mashahidi walipokuwa wanatoa ushahidi wao mahakamani.

Awali, Macha alitoa ushahidi mahakamani hapo na kudai kuwa Balenga alimuuzia nyumba ya ghorofa tano kwa sh. milioni 20 lilipo Kigogo, mjini Dar es Salaam na hajagushi. "Mheshimiwa Hakimu nimenunua ghorofa hili, huku kukiwa na mawakili wakishuhudiwa na Balenga aliniuzia ghorofa hili yeye mwenyewe,''alidai Macha mahakamani hapo. Hata hivyo, Mkumbi ambaye anadaiwa ni wakili alisimamia mkataba wa mauziano na Macha alimtaja katika ushahidi wake kuwa alishuhudia maudhiano hayo huku yeye akikana kuwa hakushuhudia maudhiano.

Hali hiyo ilitokana na Wakili huyo, kudai mahakamani hapo kuwa hakushuhudia maudhiano yeyote, bali alipigiwa simu na Macha kwa ajili ya kwenda kusaini mkataba huo. "Nilipigiwa simu na mteja wangu(Macha) niende ofisini kwake Mnazi Mmoja kuna mkataba nataka niusaini mkataba huo,''Alidai wakili huyo ndipo wakili wanaomtetea Macha, walipomuuliza Balenga mwenyewe unamjua ukimuona?. Jambo hilo lilimfanya shahidi huyo, kudai ndio ndipo alipoambiwa muonyeshe, ambapo shahidi huyo alimuonyesha mtu mwingine, ambaye ni mwandishi wa habari aliyekuwa anafuatilia kesi hiyo.

Kitendo hicho, kiliamsha cheko mahakamani hapo, huku shahidi akiendelea kubabaika kumtafuta Balenga, ambaye wakati huo naye alikuwa akionekana akicheka huku akitingisha kichwa. Mbali na shahidi huyo, shahidi mwingine ambaye pia ni Wakili wa kujitegemea, Castro Rweikiza naye alidai mahakamani hapo kuwa hakushuhudia maudhiano. "Nilipigiwa simu na Macha niende ofisini kwake, ambapo nilipofika nikakuta mkataba wa uhamishaji miliki, ndipo nikamuuliza mkataba wa mauziano upo wapi?, Macha aliniambia mkataba ameshamaliza,'alidai mahakamani hapo. Wengine waliotoa ushahidi katika kesi hiyo
 
Macha bana anaonekana kama mtu wa madili! Haiba yake inamtambulisha.
 
mfalmeselemani sasa mnatuchanganya hasa ninyi waandishi wa kujitegemea ambao hamuweki source au link hapa: theNkoromo Blog: MKE AKIRI MUMEWE BWANA BALENGA KUMUUZIA NYUMBA MFANYABIASHARA HANS MACHA KUTOKANA NA KULEMEWA NA MADENI YA MAMILIONI YA FEDHA ALIZOKOPAMKE AKIRI MUMEWE BWANA BALENGA KUMUUZIA NYUMBA MFANYABIASHARA HANS MACHA KUTOKANA NA KULEMEWA NA MADENI YA MAMILIONI YA FEDHA ALIZOKOPA

Dec 1, 2014


​
DAR ES SALAAM, Tanzania
MKE wa mlalamikaji katika kesi ya kughushi dhidi ya Mfanyabiashara Hans Macha (pichani), amedai mahakamani kwamba mumewe anadaiwa fedha nyingi na mshtakiwa, alishindwa kulipa akaamua kumuuzia nyumba.

Mke huyo Nurya Ahmad (34),ambaye ni shahidi wa upande wa utetezi, amedai hayo leo Desemba Mosi, katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu,Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, kwa kuongozwa na wakili wa utetezi, Deo Ringia.

Nurya amedai mahakamani hapo kwamba nyumba iliyokuwa ya Balenga iliyopo eneo la Kigogo, Dar es Salaam, iliuzwa kihalali kwa Macha baada ya mumewe (Balenga), kushindwa kulipa deni.

"Nafahamu kwamba mume wangu (Balenga), alikuwa andaiwa na Macha, aliniambia mwenyewe kwamba ni fedha nyingi sana, deni halikuwahi kulipwa hatimaye akaniambia kuwa ameeamua kumuuizia nyumba.

"Alikuwa akikopa kwa kuweka rehani hati za nyumba, madeni mengine yalikuwa yakilipwa, tulikuwa katika ndoa kuanzia mwaka 2001 hadi 2012, sijawahi kuona mume wangu akiwa kichaa," alidai Nurya baada ya kuulizwa kama aliwahi kuona mumewe akiwa kichaa.

Shahidi huyo alihoji mahakamani kwamba hati za nyumba halisi zilifikaje kwa Hans Macha, kama Balenga hakuzipeleka mwenyewe kwake, aliongeza kwamba hajawahi kumsikia mumewe akilalamika
kudhulumiwa nyumba na Macha.

Mfanyabiashara Hans Macha akijitetea alidai kwamba Ramadhani Balenga alishindwa kumlipa deni la Sh. milioni 879 akamuuzia nyumba iyo ya Kigogo.

Alidai Balengo alikuwa akimtegemea kwa kukopa fedha mara kwa mara kwa ajili ya kuingiza makontena ya vifaa vya umeme au elektroniki.

"Aliletwa na wafanyabiashara wenzangu kwa ajili ya kukopa, nilimpa masharti ya kukopa, aliweka dhamana hati ya nyumba yake ya Mabibo, Manzese, Kigogo, Mbezi Beach, mara ya mwisho Balenga nilikuwa namdai jumla ya Sh. milioni 879, wakati huo nilikuwa na hati zake za nyumba nne.

"Balenga alishindwa kulipa akidai kwamba kontena zake zilikamatwa na kufilisiwa na TRA, aliamua kuniuzia nyumba ya Kigogo, Manzese na nimuongezee Sh. milioni 20 ili tumalizane deni lote.

"Nilipofanya hivyo mbele ya wakili nilikuwa nimempa jumla ya Sh. ilioni 899, nilipomkabidhi fedha ya nyongeza Sh. milioni 20 alinikabidhi hati, siku nyingine tulisaini hati ya kuhamisha umiliki,

Balenga alinikabidhi nyaraka zingine ikiwemo michoro, mikataba ya ujenzi, kibali cha ujenzi, miakataba halisi waliyoingia na kampuni ya ujenzi pamoja na risiti mbalimbali," Macha alidai.

"Si kweli kwamba nilighushi, Balengo aliniuzia nyumba baada ya kushindwa kulipa deni, naiomba mahakama iyatupe mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yangu,"alidai Macha.

Shahidi wa tatu, Mohammed Waziri Mohammed ambaye ni mfanyakazi wa Balenga pia alidai mahakamani kwamba mlalamikaji katika kesi hiyo alikuwa akidaiwa na Macha.

Waziri alidai mara kadhaa alikuwa akienda na mlalamikaji kwa Macha kwa ajili ya kukopa fedha. Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho Jumanne, Desemba 2, 2014.

Posted by: Bashir Nkoromo at 12/01/2014
 
mfalmeselemani sasa mnatuchanganya hasa ninyi waandishi wa kujitegemea ambao hamuweki source au link hapa: theNkoromo Blog: MKE AKIRI MUMEWE BWANA BALENGA KUMUUZIA NYUMBA MFANYABIASHARA HANS MACHA KUTOKANA NA KULEMEWA NA MADENI YA MAMILIONI YA FEDHA ALIZOKOPA[h=2]MKE AKIRI MUMEWE BWANA BALENGA KUMUUZIA NYUMBA MFANYABIASHARA HANS MACHA KUTOKANA NA KULEMEWA NA MADENI YA MAMILIONI YA FEDHA ALIZOKOPA[/h] Dec 1, 2014


​
DAR ES SALAAM, Tanzania
MKE wa mlalamikaji katika kesi ya kughushi dhidi ya Mfanyabiashara Hans Macha (pichani), amedai mahakamani kwamba mumewe anadaiwa fedha nyingi na mshtakiwa, alishindwa kulipa akaamua kumuuzia nyumba.

Mke huyo Nurya Ahmad (34),ambaye ni shahidi wa upande wa utetezi, amedai hayo leo Desemba Mosi, katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu,Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, kwa kuongozwa na wakili wa utetezi, Deo Ringia.

Nurya amedai mahakamani hapo kwamba nyumba iliyokuwa ya Balenga iliyopo eneo la Kigogo, Dar es Salaam, iliuzwa kihalali kwa Macha baada ya mumewe (Balenga), kushindwa kulipa deni.

“Nafahamu kwamba mume wangu (Balenga), alikuwa andaiwa na Macha, aliniambia mwenyewe kwamba ni fedha nyingi sana, deni halikuwahi kulipwa hatimaye akaniambia kuwa ameeamua kumuuizia nyumba.

“Alikuwa akikopa kwa kuweka rehani hati za nyumba, madeni mengine yalikuwa yakilipwa, tulikuwa katika ndoa kuanzia mwaka 2001 hadi 2012, sijawahi kuona mume wangu akiwa kichaa,” alidai Nurya baada ya kuulizwa kama aliwahi kuona mumewe akiwa kichaa.

Shahidi huyo alihoji mahakamani kwamba hati za nyumba halisi zilifikaje kwa Hans Macha, kama Balenga hakuzipeleka mwenyewe kwake, aliongeza kwamba hajawahi kumsikia mumewe akilalamika
kudhulumiwa nyumba na Macha.

Mfanyabiashara Hans Macha akijitetea alidai kwamba Ramadhani Balenga alishindwa kumlipa deni la Sh. milioni 879 akamuuzia nyumba iyo ya Kigogo.

Alidai Balengo alikuwa akimtegemea kwa kukopa fedha mara kwa mara kwa ajili ya kuingiza makontena ya vifaa vya umeme au elektroniki.

“Aliletwa na wafanyabiashara wenzangu kwa ajili ya kukopa, nilimpa masharti ya kukopa, aliweka dhamana hati ya nyumba yake ya Mabibo, Manzese, Kigogo, Mbezi Beach, mara ya mwisho Balenga nilikuwa namdai jumla ya Sh. milioni 879, wakati huo nilikuwa na hati zake za nyumba nne.

“Balenga alishindwa kulipa akidai kwamba kontena zake zilikamatwa na kufilisiwa na TRA, aliamua kuniuzia nyumba ya Kigogo, Manzese na nimuongezee Sh. milioni 20 ili tumalizane deni lote.

“Nilipofanya hivyo mbele ya wakili nilikuwa nimempa jumla ya Sh. ilioni 899, nilipomkabidhi fedha ya nyongeza Sh. milioni 20 alinikabidhi hati, siku nyingine tulisaini hati ya kuhamisha umiliki,

Balenga alinikabidhi nyaraka zingine ikiwemo michoro, mikataba ya ujenzi, kibali cha ujenzi, miakataba halisi waliyoingia na kampuni ya ujenzi pamoja na risiti mbalimbali,” Macha alidai.

“Si kweli kwamba nilighushi, Balengo aliniuzia nyumba baada ya kushindwa kulipa deni, naiomba mahakama iyatupe mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yangu,”alidai Macha.

Shahidi wa tatu, Mohammed Waziri Mohammed ambaye ni mfanyakazi wa Balenga pia alidai mahakamani kwamba mlalamikaji katika kesi hiyo alikuwa akidaiwa na Macha.

Waziri alidai mara kadhaa alikuwa akienda na mlalamikaji kwa Macha kwa ajili ya kukopa fedha. Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho Jumanne, Desemba 2, 2014.

Posted by: Bashir Nkoromo at 12/01/2014

Huyu macha kigeugeu mara alikua anamdai,mara alimuuzia,huyu ni tapeli
 
Je uyu ndiye Macha anayesemekana kuwa ni miongoni mwa wachotaji wa ESCROW!!!!!!!!

Ufafanuzi Please.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Dalisalama imejaa wapigaji kiaina kina Escrow wako wa aina nyingi sana.
 
nilipoona balenga nikakumbuka BATENGA. Angekuwa BATENGA huyo Macha angehesabu maumivu tu, tena makali....
 
Maudhiano=kupeana Jaziba
wakati
mauziano=makubalino ya kuamishiana miliki.
Kiswahili bana!
 
Kama hakuuziwa hizo hati za nyumba zilifikaje kwa Bwana Macha??
 
Back
Top Bottom