Kumbe ni habari za rekodi!! Hoja inaanza hivi
1. Mashabiki wa Simba kuishangilia Al Ahyl
2. Mashabiki wa Yanga wananza vurugu
3. Yanga wanafunga goli
4. Viti vinarushwa.
Kama ni bakora hapa utawachapa wa kundi gani na kuacha lipi?
Haya nimetii. Japo kabla yagoli unaona waziwazi waliokuwa wanafanya vurugu ni akina nani.
Mkuu usiongee nahharia. Kama kweli wewe ni mwanamichezo na ulikuwapo uwanjani basi unapaswa kukemea ushenzi uliofanyika.
Asili ya vurugu: Mashabiki wa UBT walipoamua kukaa nyuma ya goli upande wa screen. Lengo kuu lilikuwa kuumiliki uwanja dhidi ya waarabu ili kuzima kelele zao za ushangiliaji. Hii pia ilikuwa sahihi kwa vile eneo hilo lilikuwa wazi tu. Hizi ni mbinu za kimchezo.
Wahuni wa soka (soccer hooligans) waliovalia sare nyekundu na nyeupe hawakuipenda hali hiyo. Hivyo rabsha zikaanza hata kabla ya mechi kwa wahuni hao kujaribu kuwaondoa mashabiki wa Yanga kwa madai kuwa hilo ni eneo lao la kukaa. Yanga wakagoma, viti vikaanza kurushwa hata kabla mechi haijaanza (timu zilikuwa zikipiga jalamba). Ukweli ni kuwa viti viling'olewa upande wa jukwaa la wekundu na kurushwa kwa mashabiki wa Yanga. Katika hatua ya kushangaza, FFU waliingilia kati na kuanza kuwatandika virungu mashabiki wa Yanga, wakiwataka warudi mpaka eneo lao (nusu ya uwanja). Hali hii ilisababisha manung'uniko kwa vile hii haikuwa mechi baina ya Simba na Yanga. Pia kitendo hiki kilitafsiriwa kuwa ni njama za polisi wetu kuwasaidia wageni ambao huzinyanyasa timu zetuziwapo huko.
Kufuatia malalamiko mengi, Luis Sendeu alimvaa Wambura Boniphace kutaka ufafanuzi kisa cha mwenyeji kunyanyasika nyumbani, na kama hi imechi ni baina ya Yanga na Simba. Ndipo afisa wa juu wa polisi alipowaamuru polisi wasio na uzalendo wawaruhusu yYanga kukaa kwenye viti vilivyo wazi bila vurugu. Yanga wakarudi tena na kuweka bendera zao kwa amani.
Mashabiki wa upande wa pili hawakuridhika na hatua hio, lakini polisi walisimama imara kudhibiti rabsha zoa.
Kasheshe kubwa lilikuja pale goli lilopofungwa. Wakali wa UBT waliokjwa jirani kabisa na wamisri koko wllishangilia kwa furaaaha. hii iliwakera makoko hao, ndipo wakaanza ile tabia chafu walioizoea ya kurusha viti. Hali ilkkuwa mbaya kiasi kwamba wekundu wenye busara aalianza kuwadhibiti wenzao wasiendelee na ushenzi huo.
Maoni:
Yanga akiwa mwenyeji alikuwa na haki zote za kujipangia mbinu za ushindi. Hii hutokea hata kwa timu zingine ambapo wageni hupewa idadi fulani tu ya tiketi.
Pia huu haukuwa mchezo baina ya Simba na Yanga, hivyo hakuna timu yenye hati miliki ya eeeo la kukaa uwanjani. ni upuuzi mkubwa. kuthibitisha hilo, benchi la akiba la Yanga lilikuwa upande unaofahamika kutumiwa na Simba, wala wamisrikoko hawakulalamika.
Kifupi Simba mmetia aibu sana.