Mashabiki wa Manchester United wanaamini kwenye ushirikina?

Ladder 49

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
7,416
18,856
Wakuu Habari zenu?

Wamenishangaza hawa mashabiki wa Manchester United,Yaani leo kabla ya mechi yao na Liverpool walikuwa wanamini watashinda hiyo mechi,nikawa najiuliza hawa kunanguvu tofauti wanaitegemea na kucheza uwanjani pale peupe tuone?

Ukifatilia kwenye thread zote za timu za ulaya mashabiki wanazungumzia mapungufu na malalamiko ya timu zao(Manchester United ikiwepo) isipokuwa Liverpool maana Liverpool mechi 7 mfululizo sasa hawajaruhusu timu yao kuguswa wavu,hawana malalamiko yoyote kwenye timu yao. Zaidi ya kushangilia tu timu yao.

hiki kipindi cha January na December ni kigumu sana lakini wao sio tu kushinda mechi bali wavu wao hakuna kuguswa mechi 7 mfululizo zilizopita sasa.unaweza kusema ni rahisi ila sio rahisi.liverpool wanauwezo wa hali ya juu sana.kama rahisi mbona timu yako imeshindwa?

Sasa nikawa nashangaa mashabiki wa Manchester United ujasiri walikuwa wanautoa wapi wakuamini watawafunga Liverpool pale anfield maana Liverpool mara ya mwisho kufungwa pale leo zimefika siku 1000 kabla ya mechi na Manchester United ,mechi 51 hawaja poteza pale anfield kabla ya mechi na Manchester United,kimahesabu Liverpool hawajafungwa anfield msimu wa tatu sasa yaani miaka 3 iliyopita ndio walifungwa.na mpira wanaocheza unaonekana kabisa hawa wanauweza sana sio kidogo.

Sasa nashangaa Manchester United ilivyokuwa mbovu Hivi eti mashabiki wanaamini watawafunga Liverpool ambayo msimu uliopita ilifungwa mechi moja tu kwenye ligi na kikosi chao kimebaki kile kile sasa hivi pressure ya ubingwa aiwasumbui wao kila mechi ni fainali tu.wanaamini kushinda kila mechi ndio uchukue ubingwa.

Kuna mashabiki wa Manchester United licha ya kuzidiwa point 30 na Liverpool bado watakuambia eti watachukua ubingwa najiuliza hawa wanaamini kwenye ushirikina?

Liverpool kwa sasa wamerekebisha makosa yao waliofanya msimu uliopita wa kufungwa mechi moja kwenye ligi nakukosa ubingwa. Sasa hivi wanachokifanya ushindi kwanza ukitaka kiatu mo salah subiria msimu ujao cha kwanza kushinda kila mechi.

Mashabiki wa Manchester United wanaamini kwenye ushirikina? Maana kwa kikosi bora cha Liverpool hiki wanaamini watawafunga kweli?

Maana kila kitu wamezidiwa na Liverpool kuanzia golini mpaka forward asilimia kubwa kikosi cha Liverpool ndio kinaunda kikosi cha dunia kwa sasa wamedhihirisha na wanadhihirisha hilo kwa kushinda kila mechi hapo epl msimu wa 2019/2020.

Mashabiki wa Manchester United mmenishangaza sana kuamini mtamfunga Liverpool iliyokuwa bora sana kwa sasa (kwa wale wanao angalia mechi za Liverpool wanaelewa),mashabiki wa Manchester United waache kuishi kwa mazoea.

mpaka nimekuwa na maswali hawa washabiki wa Manchester United kuna nguvu ya ziada wanaitegemea kushinda mechi uwanjani Tofauti na wachezaji wao kucheza pale uwanjani?

Ni hayo tu wakuu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sasa usipojiamini kuna mtu atakwambia timu yako inashinda hata kama ukweli unajulikana timu fulani iko poa hivi unaujua mpira kweli wewe?

Nina wasiwasi kama ungekuwa kocha unaweza kugoma kupeleka timu uwanjani kisa mpinzani yuko safi
 
👹👺👹👺👹👺👹👺👹👺👹👺👹👺👹👺👹📣📣📣
Hao ndio mashetani wekundu wa Manchester United.
Timu ambayo inajinasibu kuwa na vinasaba vya mashetani.
Wachawi nao wana nasaba na shetani
 
Umeandika ujumbe mrefu lakin pumba tu.Katika mechi zote unazozijua liverpool kwenye ligi hizo point 2 alizodondosha kwa man u tu.Hizo timu zote unazoona ziko powa nimepewa kichapo tena cha mbwa koko.Liver jana wametufunga magoli ya technical lakin kwa mpira wa uwanjani hakuna kitu.Kuanzia pass hadi kila kitu hasa kipindi cha pili Liver wamecheza hovyo sana.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom