Masauni awataka wanafunzi kuulinda Muungano

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671
0a8b56bc-3427-474b-95b2-6aefebb295e1.jpg

Unguja. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewataka wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Zanzibar kuwa mstari wa mbele kulinda, kuuenzi na kuutetea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kuendeleza amani, umoja na mshikamano wa Taifa.

Akizungumza wakati akifungua kongamano kuhusu Muungano kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), leo Februari 19, 2026, Masauni amesema vijana ni nguvu kazi na ni tumaini la taifa, hivyo wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha urithi wa amani na upendo ulioasisiwa na waasisi wa Taifa unaendelea kudumu.

Amesema kongamano hilo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa Aprili 23, 2024 wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais, ambapo alisisitiza umuhimu wa kutoa elimu ya Muungano kwa makundi mbalimbali ya jamii, hususan vijana.
7b0ee002-d15f-4a9a-997c-701ae7499b4f.jpg

“Idadi kubwa ya Watanzania ni vijana waliozaliwa baada ya Muungano, hivyo ni muhimu wapate uelewa mpana kuhusu historia, misingi na manufaa yake ili wawe mabalozi wazuri wa kuulinda,” amesema Masauni.

Masauni amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na waasisi wa Taifa letu Julius Nyerere na Abed Amani Karume, umeendelea kudumu kwa zaidi ya miaka 61, ukiwa nguzo ya amani na utulivu nchini.

“Uzalendo si maneno pekee bali ni matendo. Vijana mnapaswa kusuluhisha migogoro kwa mazungumzo, kuheshimu maoni tofauti, kupinga rushwa, kulipa kodi kwa uaminifu na kulinda rasilimali za taifa,” amesisitiza.

“Serikali iko tayari kushirikiana na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini kuhakikisha Muungano unaendelea kuwa msingi wa kudumisha amani, utulivu na maendeleo kwa kizazi cha sasa na kijacho,” amesema.
d57c009a-cc34-4127-9ab3-e4e8b6767eec.jpg

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Suleiman Masoud Makame amesema kongamano hilo limewezesha kupata maarifa na uelewa zaidi kuhusu upekee wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

“Tukiwa na uelewa pana kuhusu wajibu kama vijana wa taifa, na kwamba nmakwenda kutumia maarifa na uzoefu mlioupata katika kuendeleza misingi ya Muungano ya Amani, Utulivu na mshikamano,” amesema Makame.

Amesema kongamano hilo litasaidia kuongeza uelewa kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu kuasisiwa kwa Muungano, changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wake, pamoja na malengo na dira ya kuudumisha na kuuenzi kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Naye, Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Juma Omar Nkwede amesema kongamano hilo limekuja wakati sahihi kwao kwa kuwapa elimu ya historia kuhusu taifa.
da30b2d0-78c3-4639-a77b-dae6d4e6d358.jpg

Amesema elimu waliyoipta imezidi kuwa msingi imara juu ya kuendelea kutetea Muungano kwa kujua misingi ambayo imewekwa na waasisi kwa maslahi mapana ya nchini kwa vizazi vya sasa na vijavyo.Top of Form
 
View attachment 3546088
Unguja. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewataka wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Zanzibar kuwa mstari wa mbele kulinda, kuuenzi na kuutetea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kuendeleza amani, umoja na mshikamano wa Taifa.

Akizungumza wakati akifungua kongamano kuhusu Muungano kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), leo Februari 19, 2026, Masauni amesema vijana ni nguvu kazi na ni tumaini la taifa, hivyo wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha urithi wa amani na upendo ulioasisiwa na waasisi wa Taifa unaendelea kudumu.

Amesema kongamano hilo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa Aprili 23, 2024 wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais, ambapo alisisitiza umuhimu wa kutoa elimu ya Muungano kwa makundi mbalimbali ya jamii, hususan vijana.
View attachment 3546089

“Idadi kubwa ya Watanzania ni vijana waliozaliwa baada ya Muungano, hivyo ni muhimu wapate uelewa mpana kuhusu historia, misingi na manufaa yake ili wawe mabalozi wazuri wa kuulinda,” amesema Masauni.

Masauni amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na waasisi wa Taifa letu Julius Nyerere na Abed Amani Karume, umeendelea kudumu kwa zaidi ya miaka 61, ukiwa nguzo ya amani na utulivu nchini.

“Uzalendo si maneno pekee bali ni matendo. Vijana mnapaswa kusuluhisha migogoro kwa mazungumzo, kuheshimu maoni tofauti, kupinga rushwa, kulipa kodi kwa uaminifu na kulinda rasilimali za taifa,” amesisitiza.

“Serikali iko tayari kushirikiana na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini kuhakikisha Muungano unaendelea kuwa msingi wa kudumisha amani, utulivu na maendeleo kwa kizazi cha sasa na kijacho,” amesema.
View attachment 3546090
Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Suleiman Masoud Makame amesema kongamano hilo limewezesha kupata maarifa na uelewa zaidi kuhusu upekee wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

“Tukiwa na uelewa pana kuhusu wajibu kama vijana wa taifa, na kwamba nmakwenda kutumia maarifa na uzoefu mlioupata katika kuendeleza misingi ya Muungano ya Amani, Utulivu na mshikamano,” amesema Makame.

Amesema kongamano hilo litasaidia kuongeza uelewa kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu kuasisiwa kwa Muungano, changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wake, pamoja na malengo na dira ya kuudumisha na kuuenzi kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Naye, Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Juma Omar Nkwede amesema kongamano hilo limekuja wakati sahihi kwao kwa kuwapa elimu ya historia kuhusu taifa.
View attachment 3546091

Amesema elimu waliyoipta imezidi kuwa msingi imara juu ya kuendelea kutetea Muungano kwa kujua misingi ambayo imewekwa na waasisi kwa maslahi mapana ya nchini kwa vizazi vya sasa na vijavyo.Top of Form
Yaani anata Wazanzibari ndiyo walinde muungano? So does this translates kwamba wao ndiyo wenye uwezo wa kuulinda na siku wakitaka kuuvunja wanauvunja?
Watanganyika majority hatuutaki kabisa, hao parasites wakae kivyao kwanza then ndiyo walete proposal iwekwe hadharani ndipo kupigwe kura kama majority ya raia wanakubali au la.
We ain't equally yoked.
 
Hao wasomi wa vyuo vikuu zanzibar hamna kitu vichwani wamebebwa bebwa ili mradi vyuo vyao vipate wanavyuo na ajabu wote wakishamaliza masomo yao urojo watakuja kupewa ajira huku bara huku vijana wetu compitent wakikosa fursa hizo, huu muungano ni takataka kabisa!!.
 
Back
Top Bottom