Masanja: Nimenunua BMW X6 kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,786
Mchekeshaji wa Orijino Komedi na mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji amesema kila anachomiliki amekinunua kwa pesa yake halali huku akishangaa kwanini watu wameshtuka baada ya kuona anamiliki BMW yenye plate namba ya jina lake.

Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Masanja alisema anamiliki magari mengi huku akidai BMW X6 ameinunua kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli.

“Mimi nina magari mengi sana na yote nayachukulia kama chombo cha usafiri cha kunitoa point moja kwenda nyingine,” alisema. “Sasa nashangaa watu wanaongea sana kuhusu mimi kwani gari kitu gani! Hiyo BMW X6 nimenunua kama watu wengine wanavyonunua baiskeli,” alijinadi.

Aliongeza, “Na hata hao TRA kama wananisikia waje hapa Clouds nimekuja nayo ipo hapo chini ili waangalie kama sijailipia.”

Masanja alisema anafanya biashara za aina mbalimbali hivyo kununua gari la thamani siku kitu cha ajabu kwakuwa anaweza kununua kupitia biashara yake moja tu.

BWW.jpg
 
Mjinga sana, maneno yanafaa kutamkwa na Dr. Mengi, Bkharessa na & Gwajima, profesa tibaijuka(BIBI wa pesa ya mboga), chenge,(babu wa vijisenti) na mzee wa msoga na watu wa kaliba hiyo....

Sio yeye. Masanja hana hela ya kununua BMW kama anavyonunua baskeli.

Gari zina charge nyingi sana. Baskeli na gari tofauti sana katika ununuzi, kuanzia kutoa hela benki nk na ikipata ajali anaweza kukesha miaka kuikarabati.

. You never know..Hope alikua anachekesha watu, manake ndo kazi ya ze komedian kama yeye.

Maskini akipata mata** ulia mbwata.
 
Last edited:
Watu watamponda sana ila siku zote ukimshirikisha Mungu, ukiwa na nidhamu na ujafanya kazi kwa bidii mafanikio hayajifichi.
Namkumbuka Masanja wa miaka ile alipokuwa mambo hayo na akina Joti na Mpoki, leo tunaona mafanikio yao
 
Watu watamponda sana ila siku zote ukimshirikisha Mungu, ukiwa na nidhamu na ujafanya kazi kwa bidii mafanikio hayajifichi.
Namkumbuka Masanja wa miaka ile alipokuwa mambo hayo na akina Joti na Mpoki, leo tunaona mafanikio yao
Masanja ndio anayepondea wengine. Nani alimuuliza atutajie kua anaweza kununua Gari. Haituhusu.
Wasanii wa bongo njaa tu. Wengi walijipendekeza kwenye mfumo. Ndio maana wameinuka.
 
Kitu kimesimamia kucha hiko,Masanja unakuwa wa2 baada ya DIAMOND kumiliki BMW X6 TZ kwa upande wa wasanii.Gari iliyoshika nafasi ya 12 duniani mwaka 2015 kwa upande wa magari ya kifahari hongera sana Masanja.
 
Watu watamponda sana ila siku zote ukimshirikisha Mungu, ukiwa na nidhamu na ujafanya kazi kwa bidii mafanikio hayajifichi.
Namkumbuka Masanja wa miaka ile alipokuwa mambo hayo na akina Joti na Mpoki, leo tunaona mafanikio yao
Masanja alishawah kuwa MAMBO HAYO!???ME NIMEMJULIA CHANNEL 5
 
Time will tell. Kama kweli ni mchele au chuya. Tulikwisha ona hapa hapa bongo makampuni makubwa makubwa, au watu matajiri kupindukia. Baada ya mfumo fulani kubadilika kampuni inakufa, tajiri anafilisika bila maelezo. Kama ni mchele tutauona. Kama ni chuya tuziona.
 
Kipind hicho Mpoki anafuga minywele, wembambaaa! Sema Joti hakui aisee tangu namuona ni anazid kukomaa tu. Wameanza kitambo vibaya pamoja na Seki
Nilikua najua kuwa Mpoki na Joti wameanzia Mambo hayo ITV,then Seki,Mpoko,Joti na Masanja wamekutana CHANNEL 5
 
Wote walikuwa itv kipind hicho kasoro wakuvwanga, makregan na yule mwingine nan sijui alieugua
 
Wabongo hata siwaelewi.. Mtu akifulia watu wanamcheka... Akipata mkwanja akanunua 'madude' watu wanahate... Mtu anafanya Interview anaulizwa swali na interviewer, Majibu yake yanaonekana ya kujisifia.. Ah...kumbe ndo maana American rappers wanasema niggaz gon hate you for no reason..either way it goes...
Kwanini watu hawapendi kuona wenzao wanatusua... Wanataka hata mtu ukinunua gari zuri usiseme. Ukisema tu, unajisifu na maneno ya kejeli kibao. Watu wanataka kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa tu ndo waone raha maana ndo wamelelewa kwa kudanganywa na mama zao na viongozi wao pia. Disgusting.
 
Last edited:
Hatuchukii mafanikio yake ila Ana majivuno akiwabeza vijana waliosoma na kukosa ajira.Anakosea majivuno Tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom