Kimbia uje haraka mama ukichelewa utakuta wameshaniua,kuna majambazi wananiwinda hawataki kuyaona mafanikio yangu na roho zinawauma mno njoo haraka nikupe urithi wa mali.
Ukichelewa ndugu zangu watakudhulumu mwisho wa siku watoto wetu watateseka,watakosa elimu bora nawe tayari utakuwa mjane mwenzangu. nilikua Ilula pande za Iringa,si unajua tena kazi ya mumeo ilivyo ngumu.
Nilienda kuripoti tukio la police kuwapiga ndugu zetu waliokuwa wanajiburudisha kwa kilevi baada ya kazi ngumu za shambani wanazofanya,mwenzangu wakiwa hawana hili wala lile ghafla wakavamiwa na police na kuanza kupigwa eti kisa wanakunywa pombe mida ya kazi.
Jamani Tanzania Ilivyo kubwa ni hao tu wanaokunywa pombe mida ya kazi? Nikadokezwa kisa ni kuikataa CCM kwa nguvu zao zote katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita,mwanaume nikaingia kazini kuitoa hiyo habari katika gazeti letu la haki,kumbe nilikuwa nafuatiliwa bila kujuanipo. Nimejificha kwenye msitu wa Biharamuro njoo nikupe urithi kabla hawajani... Absalom Kibanda,kimbia uwahi usichelewe.