frank nyantu2
JF-Expert Member
- Jun 26, 2016
- 298
- 162
We umenena na unafatilia acha wengine wajuajiMambo ya mkataba yapo kwenye tume nyingine.
We umenena na unafatilia acha wengine wajuajiMambo ya mkataba yapo kwenye tume nyingine.
Hawa wazungu sio wajinga wabebe mikontena iliyojaa michanga wakajaze huko kwao!!Ndugu yangu niseme tu kwa kifupi hili swala mkuu anadhani ndiyo sehemu utakayompa ujiko wa kisiasa lakini kwenye hili kuna possibilty kubwa tumeingia mkenge na hakuna haja kuwabatiza watu kuwa ni madalali au vyovyote vile, pia kwa bahati mbaya sana hayo ndiyo maono ya mkuu wetu.
Lakini lingine naona watu wengi wala hawataki kuhangaisha akili zao ili hata kujua gharama za uzalishaji wa huo mchanga zikoje utadhani huo mchanga ulikuwa kwenye government store kisha Accacia wamekuja na kuuiba tu bila kutumbukiza mtaji wowote wa kiuzalishaji.
Bado nashauri jambo hili linataka busara ya hali ya juu sana kudeal nalo kuliko mihemko iliyopo hivi sasa.
Ya ni kweli kabisa nimesoma tena post yako na ni sawa kabisa. Mpaka sasa hivi natafakari namna walivyoihandle issue nzima nashindwa kuwaelewa. Time will tell.Nakubaliana na wewe kabisa kwa figures akizopewa raisi zinapotosha umma kabisa. Ndiyo maana nasema hata kama ni kwa takribani miaka ishirini tunaibiwa ni kiasi kidogo tu ambacho ni mharaba. Ukisoma vizuri nilichoandika utagundua kuwa mimi na wewe tunakubaliana hata kama hesabu nimekosea kiasi.
Mfumo wa uongozi aliouweka Mkuu wetu wa awamu hii ndio utakaoliingiza taifa hili pabaya. Mkuu amejitahidi na amefanikiwa kuweka mfumo wa watu kuwaona wote wanao-challenge mawazo yake ni wezi, wapiga deal, mafisadi, wala rushwa au wamepewa chochote kile wamkosoe. Huu utaratibu ni mbaya na naona taratibu unaanza kulitafuna taifa.
Sasa hivi ukiongea tofauti na mawazo ya Rais au Serikali yako basi wewe utaonekana ni moja ya watu hao niliowataja hapo juu. Kuna vitu vingi tu sasa hivi Mh. Mkuu anachemka lakini watu (wataalam) wanapiga kimya kwa kuogopa kuonekana hawaitaki mema nchi hii au wamepewa hela (wamehongwa). Hii ni mbaya sana kwa taifa. Ku-challenge (kuhoji) maamuzi au mawazo ya Rais (au Serikali) sio usaliti kwa nchi, ni njia nzuri ya kufanikisha mambo yaende, hatuwezi kufanana mawazo au mitazamo na akiona mnafanana kwenye kila jambo basi ujue anguko lenu limekaribia.
Kwenye taarifa ya jana kuna vitu vimepotoshwa/vimekuzwa lakini watu hawawezi kuviongelea kwa kuogopa kama nilivyosema hapo juu. Mkulu anaposema kwa makontena yale 277 serikali ilkuwa inapoteza mapato kati ya Bil 676 na Trilion 1.147 ya dhahabu sio sahihi.
Hizi ni true value (thamani halisi) ya dhahabu iliyopo kwenye makontena ambayo ikiuzwa, serikali kupitia TRA itachukua kodi/tozo/mrahaba wa 4% kwa sheria ya sasa hivi. Kwahiyo hiyo hela yote sio ya kwetu, sisi tuna % tu ya hela hiyo iliyotajwa. Tatizo lililopo ni kuwa kulingana na taarifa ya tume, thamani halisi ya dhahabu ni ndogo kuliko iliyotajwa hapo mwanzoni. Sasa hili tumelikuza na kuwaaminisha watanzania tumeibiwa kati ya Bil na Trilion wakati si kweli, chetu pale ni 4% ya true value (Bil 676 to Tril 1.147).
Ni kama kwenye biashara zingine tu za uzalishaji, utazalisha soda utauza zile soda, baada ya mauzo halisi ya soda zile kwa thamani sahihi ya soda, ile hela iliyopatikana (gross revenue) itapigwa % kadhaa kama kodi/tozo na mzalishaji atabaki na chake baada ya kodi/tozo (net revenue).
Sasa jana tumeaminishwa ile gross revenue baada ya kuuza zile dhahabu ni yetu yote. Hili tulikosea jana na kuleta taharuki kubwa ya kuonesha kuwa tunaibiwa sana. Ni kweli tunaibiwa lakini tuepuke kukuza mambo.
Haya yote chanzo MZEE BEN NKAPAFunga migodi yote hakuna kuchimba chochote na hao wawekezaji waondoke wote!!
Hatuwezi kuchezea nchi na rasilimali zake kama mchezo wa paka na panya.
Hatuwezi kutawaliwa au koloni la wawekezaji kwasababu ya mikataba ya kinyonyaji ya madini!
Wacha tu mkuu migodi ifungwe tuone haya mataahira yatafanya nini? Juzi yamekabidhiwa mgodi wa TULAWAKA yamekula hasara mpaka yamefunga pamoja na kuachiwa mitambo na kila kitu, yameshindwa kuuendesha huo mgodi!!ukizingatia Dec buzwagi inafungwa.
Acha kuongopea serikali. Kwenye ukweli tuseme ukweli, kwenye uongo tukatae, lakini Tulawaka hawajala hasara,ni ishu tofauti. Fatilia ili ujueWacha tu mkuu migodi ifungwe tuone haya mataahira yatafanya nini? Juzi yamekabidhiwa mgodi wa TULAWAKA yamekula hasara mpaka yamefunga pamoja na kuachiwa mitambo na kila kitu, yameshindwa kuuendesha huo mgodi!!
Hata ikifungwa sisi ni mataahira hatuwezi kuyachimba. Unakumbuka mgodi wa Tulawaka yaliachiwa kila kitu lakini yameshindwa kuuendesha. Pia wakiondoka wewe hiyo dhahabu yako utauzia wapi? Wenzetu ndo wameshika mpini sisi tumeng'ang'ania makali haki ya nani tutaacha vidole pale!! Hapa kikubwa na kinachotakiwa ni kurudi mezani na kujadili upya hii mikataba angalau iwe pasu kwa pasu!! Yote haya ni matokeo ya mataahira ya CCM tuliyoyapeleka bungeni!!Funga migodi yote hakuna kuchimba chochote na hao wawekezaji waondoke wote!!
Hatuwezi kuchezea nchi na rasilimali zake kama mchezo wa paka na panya.
Hatuwezi kutawaliwa au koloni la wawekezaji kwasababu ya mikataba ya kinyonyaji ya madini!
Unafikri unapoendesha mradi bila faida hiyo ni nini? Siyo kula hasara huko? Ndugu zako walikuwa wanatumia gharama kubwa kuzalisha kuliko mapato ndo maana wameamua kufunga, fuatilia uone ilikuwaje!!Acha kuongopea serikali. Kwenye ukweli tuseme ukweli, kwenye uongo tukatae, lakini Tulawaka hawajala hasara,ni ishu tofauti. Fatilia ili ujue
Tulawaka/stamigold inasikitisha sana.Wacha tu mkuu migodi ifungwe tuone haya mataahira yatafanya nini? Juzi yamekabidhiwa mgodi wa TULAWAKA yamekula hasara mpaka yamefunga pamoja na kuachiwa mitambo na kila kitu, yameshindwa kuuendesha huo mgodi!!
Umesema vema sana mkuuNdugu yangu niseme tu kwa kifupi hili swala mkuu anadhani ndiyo sehemu utakayompa ujiko wa kisiasa lakini kwenye hili kuna possibilty kubwa tumeingia mkenge na hakuna haja kuwabatiza watu kuwa ni madalali au vyovyote vile, pia kwa bahati mbaya sana hayo ndiyo maono ya mkuu wetu.
Lakini lingine naona watu wengi wala hawataki kuhangaisha akili zao ili hata kujua gharama za uzalishaji wa huo mchanga zikoje utadhani huo mchanga ulikuwa kwenye government store kisha Accacia wamekuja na kuuiba tu bila kutumbukiza mtaji wowote wa kiuzalishaji.
Bado nashauri jambo hili linataka busara ya hali ya juu sana kudeal nalo kuliko mihemko iliyopo hivi sasa.
Mleta mada sidhani kama kuna mtu anaweza kukuelewa labda wachache "vichwa".
Hayo madini mengine yapo ila yeye amejikita kwenye biashara moja ya gold na labda copper kidogo ndio maana mgodi unaitwa labda turawaka gold mine sio turawaka gold,uranium,polonium,nickel mine.ni sawasawa wewe uwe unauziwa chapati kwa shilingi mia mbili halafu baadae muuzaji akudai eti mbona kwenye chapati kuna unga wa ngano,mafuta,chumvi hujalipia?Ilikuwa inalipwa % ya madini ambayo yalikuwa under estimated na baadhi yake hayakuhususishwa kwenye % hizo. Mfano wewe unalipa TRA kodi ya biashara ya unga wa sembe na mtaji wa laki mbili. Na katika biashara uliyokadiriwa unalipa % kwa biashara uliyoisajiri, lakini ukawa unauza unga, Mchele, Ngano, na Mafuta ya kula na biashara ni ya mtaji wa 5millions. Sasa ukishikwa na TRA unaweza ukauliza swali lako hilo la kuwa eti huwa silipi kodi!!?? Unalipa ila unacholipa sicho ulichotakiwa kukilipa.
Mbona huo utetezi wenu bado haujaweza kuonesha kwanini waorodheshe kwa kiwango kidogo na kutooredhesha kabisa aina zingine za madini?yaani kwa hoja zenu sioni uhusiano gharama za uzalishaji na kuweka vielelezo vya kilaghai ,ina maana gharama zikiwa juu unacompesate kwa kufanya ghilba dhidi ya serikali?Hawa wametuibia kupitia mikataba ya kipuuzi tuliosaini na hapa ndio watatubana.
Alafu taarifa ile ya kamati ilijikita kueleza tu thamani ya yale madini bila kueleza actual cost of production ambayo makampuni yanaingia katika uchimbaji,strorage, usafirsha na gharama ya ku-process mchanga huu uko nje ya nchi.
Augustine Moshi
Kamati ilifanya kazi yake ya kuonyesha true value ya dhahabu iliyoko ndani ya makinika, lkn ulisikia vizur JPM alovyokuwa anaongea baada ya kukabidhiwa report?? Yeye ndio aliyedanganya umma kwa kusema hiyo hela yote Bil 676 to Tril 1.147 tumeibiwa na hao wenye migodi kwa kushirikiana na wapiga deal na kuleta taharuki kwa kukuza figure tuliyotakiwa kulipwa. Sisi yetu pale ni 4% ya hiyo hela aliyoitaja kwa ujinga wetu wa kusign mikataba mibovu. Sasa jana et tumeaminishwa kwa yale makontena 277 tumeibiwa kati ya bil 676 na Tril 1.147
Ukipiga hesabu ya 4% (ujinga wetu wa mikataba hovyo) chetu pale ni kati ya Bil 19 na Bil 45. Umeona hiyo tofauti hapo??? Hiyo sasa ndio hela nying sana tunayopoteza kuliko hiyo difference between the actual value ya kamati na declared value kabla ya kamati. Sasa hapo mwenye akili ataona tatizo liko wap na waptunapoteza mapato mengi. Mapato mengi yanapotea kwa huu ujinga wa mikataba tuliyosainiana nao inayotupa 4%. Ndo mana tunalia kila siku na kusema turekebishe mikataba yetu (ingawa sio rahis km tunavyofkria, mana tulishasign ana nao kwa ujuha wetu) au tuweke utaratibu flan ambao uyawezesha tusign mikataba yenye tija kwa taifa. Tusipojirekebisha kwny mikataba yetu,,tutaendelea kusign mikatabaya hovyo mpk Yesu anarud. Tuweke itaratibu mzuri so that we can getthe best out of our signed contracts with those Investors (mabepari).
Ovyoooooooo.utafiti hupingwa kwa utafti.lete ba wewe utafti wako.usituletee ngonjera na maigizo hapa.na pia nakuomba usijifiche.jitokeze hadharani kw kupinga kinachafanywa na serikali.HAPA KUNA MAKUNDI MAWILI TUU.(1) KUNA WANAOPINGA UFISADI NA KUPIGANIA MASIRAHI YA NCHI.(2) KUNA MAFISADI NA VIBARAKA WA MAFISADI.WANAOTETEA UFISADI NA KUWAPINGA WANAOPINGA UFISADI.HIVYO JITOKEZE WEWE UKO UPANDE UPI!!!???SECOND JULY
Mbona huo utetezi wenu bado haujaweza kuonesha kwanini waorodheshe kwa kiwango kidogo na kutooredhesha kabisa aina zingine za madini?yaani kwa hoja zenu sioni uhusiano gharama za uzalishaji na kuweka vielelezo vya kilaghai ,ina maana gharama zikiwa juu unacompesate kwa kufanya ghilba dhidi ya serikali?
Tupisheni tuendelee kuwachenjua hawa watu!
Point yangu ni kuhusu underdeclaration. Huo ndio wizi. Mkuu kataja thamani ya madini kwa fedha. Kwani amesema hiyo ndiyo asilimia yetu?
Uko sahihi unaposema tumeafiki mikataba mibovu. Namwombea Mungu mkuu ili apate nguvu ya kuwashughulikia akina Kafumu, Chenge na Kazirimagi. Wametuliza sana.
Ni ajabu kuna watu wanasema tusingefanya hivi eti kwa sababu ACACIA watakwenda mahakamani. Yaani ukamate mwizi kisha uogope kumthibiti kwa kuogopa mahakama?
Tunao ushahidi wa kisayansi kwamba ACACIA walivunja mkataba. Tuwashitaki kwa underdeclaration.
Siku nyingi tumekuwa tukijiuliza inawezekanaje nchi kama Tanzania na DRC ambazo zina utajiri mkubwa wa maliasili kuwa masikini hivyo? Magufuli katupatia aspect moja ya jibu. May he be blessed.
Naam, wachache "mchwa"Mleta mada sidhani kama kuna mtu anaweza kukuelewa labda wachache "vichwa".