PreGE2025 Mary Joseph: Kuwa CCM siyo kigezo cha kuvunja sheria

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Mara, Mary Joseph amewataka vijana kuacha kujihusisha na vitendo vinavyochafua picha ya umoja huo, badala yake wawe sehemu ya ulinzi wa amani na mshikamano.

Mary ametoa kauli hiyo leo Machi 24, 2025 alipokuwa akizungumza na vijana katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara, baada ya kuhitimisha ziara yake ya kusikiliza za na kuzitafutia ufumbuzi kero za mbalimbali zilizopo mkoani humo.

“Hatuna sababu ya kudanganya kutiana moyo na kukichafua chama kuwa vijana wa Chama Cha Mapinduzi haitupi upendeleo wowote wa kuvunja sheria, kwenda kinyume na taratibu.

“Muhimu tuwe na utaratibu wa kuzingatia sheria bila shuruti kama umeonewa hapo tunaweza kusimama pamoja na kutafuta ufafanuzi, tofauti na hapo tufuate sheria,”amesema Mary.
.
Amefafanua kuwa inawezekana kuna jambo kijana wa CCM anafanya kwa nia njema au kwa kutojua, mwingine akalifanya kwa nia ovu akasingizia ni vijana wa chama hicho kwa sababu walishawahi kulifanya hakuna pa kukwepea.

“Tusiwe mfano mbaya, tuwe mfano wa kuigwa.”
Your browser is not able to display this video.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…