Sijui umepiata wapi hii lakini iko shallow sana. Ukitaka kuijua Marxism-Leninism sawasawa, inabidi usome mambo haya ambayo yote yalianzia Ujerumani:
(1) Hegelian Philosophy ya Hegel
(2) Classical Marxism ya Marx
(3) The Communist Manifesto ya Marx na Engels
Hegelian Philosophy ilikuwa proposed na mjerumani Georg Friedrich Hegel ambayo ililenga zaidi maana ya uhuru (Liberty). Classical Marxism ilikuwa proposed na mjerumani mwingine, Karl Marx akisema kuwa maisha ya jamii ni mfululizo wa mapambano baina ya watawala (bourgeoisie) na watawaliwaji (the proletariat). Mapambano hayo yakikomaa yanaifikisha jamii kwenye Ujamaa (Socialism). Baadaye sana Marx akishirikiana na mjerumani mwingine Friedrich Engels walieendeleza ile Classical Marxism kuwa the Communist Manifesto. Mtililiko huo wa mawazo uliingiza vitu vingi sana kama vile Dielectical Materialism, Surplus Value, Base and Superstructure na mengineyo mengi tu. Miaka kama mitano iliyopita tuliwahi kuwa na mjadala mrefu hapa Jamii forum wa kuhusu theories za Karl Marx. Ukisearch utaweza kuipata thread hiyo.
Vladimir Lennin alichofanya ni kuadapt ile Communist Manifesto ya Marx na Engles na kuifanya kuwa dira ya Urusi kwa mara ya kwanza.