Marufuku ya matumizi ya tumbaku duniani

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Leo ni siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani kutokana na athari zake kiafya . katika moshi wa sigara zaidi ya kemikali 400 zimegundulika kuwa na madhara makubwa kiafya, mvutaji mdogo hutumia nusu pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa mwaka. Yafuatayo ni baadhi tu ya maradhi yatokanayo na uvutaji wa tumbaku.

-Magonjwa ya mapafu

-Ugonjwa wa moyo

-Mifupa

-Vidonda vya tumbo

-Kung'oka nywele

Na moshi na kemikali za tumbaku pia hujeruhi sehemu za ndani za masikio.
Maoni yako..!
 
Wanatania tu, mbona bangi wako serious, kama kweli wanapiga marufuku waanzie shambani kisha viwandani ndiyo waje kwetu watumiaji
 
bora pesa lkn wavutaj na wasio wavutaj waendelee kuangamia,hii.dunia yetu ni unafiki tu
 
Back
Top Bottom