bluetooth23
JF-Expert Member
- Apr 8, 2013
- 348
- 326
Akiwa jijini Saint Petersburgh, rais wa Russia Vladmir Putin amewaambia warusi waache kutumia google, facebook na twitter katika mawasiliano yao. Ikionekana ni katika kuihofia Marekani, Putin amewaeleza warusi kuwa social networks hizo zinacollet personal data zote duniani na kuzituma makao makuu ya shirika la kijasusi la marekani liitwalo Central Intelligence Agency maarufu kama CIA ambalo linasimamia servers zote za Facebook, Google na Twitter ili kupata data za maadui na mipango yote itakayohusu usalama wa marekani na pia kujua siri za watu wa mataifa mengne. Putin amewataka warusi wote watumie social networks za kirusi katika mawasiliano yao. Pia amependekeza mamlaka za mawasiliano na parliament kutunga sheria ya kupga marufuku matumizi ya Facebook, Twitter na Google nchini humo. China wao siku nyingi walishapiga marufuku mitandao hyo na hivi juzi Uturuki nao wamepga marufuku.