hao ndo wasabato bw ubaguzi nje nje
Hakuna ubaguzi hapo, ngoja nikupe stori fupi tu kuhusu umhimu wa kuoana mkiwa na imani iliyo sawa.
Siku moja jumamosi nikiwa kanisani mwanamke akaja akiwa amevimba kwa hasira, kisa Mme wake kaenda na watoto kanisani. Na hapo mwanzo mwanamme na mwanamke walikuwa wakatoliki wote baadaye ndipo mwanamme akawa msabato. Swali dogo tu.
Inawezekana kabisa huko mbeleni wakishachujana kila mmoja akaanza kudai watoto waliowapata wakaabudu kanisani kwake itakuwaje hapo? maana sasa hivi bado wamefungwa kwa upofu wa mapenzi, shetani akiingilia ndoa. Jaribu kufikiri kidogo kuhusu mfano huu. Na ndio maana mtume paulo aliandika juu ya umhimu wa kuoana mkiwa wa imani moja.
Haijalishi uthamani wa kiti ambacho shetani amekupatia hapa duniani, mwisho wake ni maafa.