Marufuku kukaa karibu na vituo vya kupiga Kura, inatakiwa kukaa umbali wa mita 100

Do JF siku hizi sijui ni kitengo cha Masaki.... uzi wangu wa IGP: Marufuku kukaa vituo vya kura... haufanani kabisa na huu... zile coments zilizo tolewa ndo zimehamishiwa uzi huu lakini ile main msg ambayo ilikuwa kama inauliza opinio za wadau na polisi kama uamuzi na matamshi ya IGP yapo kisheria umefutwa kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa... do hi ni hatari.... nilikuwa naona wadau wanalalamika sasa ndo nimeelewa.... uzi wangu ulikuwa hauongelei sana suala la 100m ila undani wa matamshi ya IGP na labda anaweza kuja na wazo mbadala baada ya kuona comments za wadau.... hapa sasa kilicho fanyika ni total confusion na ile main part imefutwa.... haya bana.... kama nanyi ni sehem ya kitengo.... tutahamia mwanahalisionline.... boring .....
 
@ Mbeziboy ule uzi wangu umeuchangia sana.... ukitafuta main content ya ule uzi wa IGP: Marufuku kukaa vituo vya kupiga kura (toka gazeti la Tanzania Daima)imefutwa kabisa wakati uzi ule unaunganishwa na huu.... ndo maana naanza ona JF imeanza kuwa kama sehem ya kitengo vile..... kama wale tunao wajua wanacho sema sio wanacho kiamini na sicho wanacho fanya...boring....
 

Hata mie nimeliona hilo mkuu
 

mkuu usilamu sana yawezekana wametuokoa na sheria ya makosa ya kimtandao. au wewe umesha imeza nzima nzima?
 
hapana atumie sheria hii kuhakikisha kuwa kila chama kina weka wakala wa kuhesabu kura anaye aminiwa na chama chake

Mawakala watakuwepo..hilo wala halina mjadala. Issue ni watu wawepo au wasiwepo? Nadhani chimbuko la hii sheria unayoiita pungufu (mimi sidhani ni pungufu) ilitokana na uelewa wa watunga sheria kwamba polisi hawapo wa kutosha kukimbizana na watu mkuu. We fikiria vituo zaidi ya 70,000. Utahitaji polisi wangapi kuanza kukimbiza wananchi na kuhakikisha wamerudi nyumbani? Na pia ukumbuke kila mtanzania ana haki ya kikatiba ya kukusanyika (freedom of assembly). Sheria ilichofanya ni kuweka mazingira yatakayoruhusu wananchi kufaidi hiyo haki yao kwa usalama. Maana ukweli ni kwamba watakusanyika tu.
 
mkuu usilamu sana yawezekana wametuokoa na sheria ya makosa ya kimtandao. au wewe umesha imeza nzima nzima?
Mkuu Kojo.... mjadala wenye tija hata polisi na NEC wanasoma na pia huibua fikra mpya... wanaweza kuona mantiki na kuja na mbadala wa maamuzi yao.... hatuwez kuwa taifa la watu waoga kwa kiasi hicho.... nna uhakika 100% cyber law pale haituhusu na pia hata IGP angeona kilichoko pale ambacho labda kingekuwa bora kwa mama tz.... ila JF siku hizi da....
 

kabla ya kuniuliza hili swali lako, ulitafakari kidogo kuwa kwa nini sikusema watu wasije kupiga kura?
 

so tunao polisi wa kuisimamia hiyo mikusanyiko ya walinda kura wa vyama vyote kila kituo? au mtakubali waongezewe nguvu na JWTZ?
 
so tunao polisi wa kuisimamia hiyo mikusanyiko ya walinda kura wa vyama vyote kila kituo? au mtakubali waongezewe nguvu na JWTZ?

Ha haaa haaa... we Kojo Jwtz hapana.... ila vijijini nadhani watatumia mgambo.... kwa idadi ya vituo 72,000 kama kila kituo ni polisi 2 hao ni polisi 144,000 jeshi letu sidhani kama tuao polisi wengi kiasi hicho....
 
so tunao polisi wa kuisimamia hiyo mikusanyiko ya walinda kura wa vyama vyote kila kituo? au mtakubali waongezewe nguvu na JWTZ?

Ukiwaruhusu wanaotaka kubaki wabaki kwa mpangilio..utahitaji polisi wachache kuliko utakaowahitaji kama unataka kumkimbiza kila mtu aende nyumbani. Historia inaonyesha fujo hua zinaanza pale ambapo watu wanaona haki zao walizopewa kisheria na kikatiba zinanyimwa na vyombo vya usalama. Yani kwa hii kauli ya mangu...wapo ambao hata walikua hawana mpango wa kubaki lakini sasa watabaki "ili kupigania haki zao". Ndio maana mara nyingi inasemekana kwamba chimbuko la fujo ni polisi wenyewe.
 
Hivi watu wote wakikaa kusubiri kura zao maisha yatakuwaje.....ujinga wa mnyika wenu akakae mwenyewe....mnasahau kuwa kuna sheria inazuia mikusanyiko isiyoruhusiwa kisheria..mkionekana kama kikundi mnapigwa

hiyo sheria inazuia mikusanyiko ipo ya kuangalia mpira mita miamoja si eneo la tume hofu ya nini kwa tume kama wanatenda haki,kwanini ni CCM tu ndio wanashabikia watu warudi ma kwao,kwanini tume inapindisha sheria haisemi watu wakae mita mia badala yake inasema waende home.
 
Kumbuka kuna gari 700 za washawasha zimeletwa kutusulubu tu, wakati huo mlo sie kuupata ni shiiida
Magari mia saba vituo elfu sabini na mbili polis elfu arobaini na tano wananchi milion hamsini. Ninyi ndio mnataka kuvuruga Amani. Kila raia anajua wajibu wake wa kupiga kura na kuondoka kituoni lakini kama anaona asubiri matokeo au aone kama haki inatendeka basi anaweza kusubiri zaidi ya mita mia moja kutoka kwenye kituo cha kupigia kura mradi asilete tafrani kwa wanaokwenda kupiga kura. Pia kumbuka vituo vingi viko kwenye makazi ya watu je siku ya uchaguzi wataamishwa wakazi walio karibu na vituo vya kupigia kura?
Naomba viongozi wanaosimamia sheria wasiwe chanzo cha kuharibu uchaguzi wao wawajibike kwa kufuata sheria ama sivyo kuwe na njama za kuahirisha uchaguzi kwa kisingizio cha vurugu vituoni ambazo zitaanzishwa na vyombo vya dora badala ya kulinda usalama.
 

Sheria imerekebishwa. Kusimama ni mita 200 kwa uchaguzi huu.Au kama unaona mita 200 I mbali hauoni u naomba kwenda kukaa nyumbani na kufatilia matokeo kwenye TV. Yenyewe itakua ipo karibu zaidi, kama mita 1 au 2 tu.
 
Mkuu mnatungaje sheria zenye kuingiza watu matatizoni?? Unakumbuka matukio ya makada kubeba kura kwenye hot pot??
 
Sheria imerekebishwa. Kusimama ni mita 200 kwa uchaguzi huu.Au kama unaona mita 200 I mbali hauoni u naomba kwenda kukaa nyumbani na kufatilia matokeo kwenye TV. Yenyewe itakua ipo karibu zaidi, kama mita 1 au 2 tu.
Mkuu, ilirekebishwa lini? Au kwenye zile za dharura?. Alafu kuangalia kwenye tv naona umesahau kuwa,
#hapa giza tu.
 
Ukilaza tunaoung'ang'ania kwa dhahania za kulinda kusubiri kuna siku tutakiri kwamba hatukua sahihi kwa maamuzi hayo,haya na kila mmoja wetu afanye anavyoona inafaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…