Marudio yasiyoisha ya uhakiki wa vyeti, chanzo kikubwa cha upotevu au kuibiwa vyeti

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Salam ndg zangu.

Toka swala la uhakiki lianze, haliishi kabisa.Kila siku uhakiki, hii inasababisha watumishi wa umma kila siku kutembea na vyeti original mkononi ili ikitokea la kutokea,awe navyo.

Sasa vibaka /wahuni/ wataalam wa mjini nao wamekuwa wakiviwinda sana vyeti, hasa wale ambao hawajasoma au wanatafuta vyeti.

Matukio ya watu kuibiwa vyeti yamekuwa mengi sana toka zoezi la uhakiki lianze. Kwann swala hili linarudiwa kila siku?Hakuna coordination ya mifumo ya serikali ili kukamilisha swala hili kwa ambao wameajiriwa?

Mathalani leo hii mtu anapoteza cheti cha kuzaliwa, cha form 4, form 6, Chuo kikuu nk, ni usumbufu mkubwa sana kupata nakala yake. Kama umesoma Ulaya inakuwaje?

Malizeni swala la kuhakiki watu ili vyeti vya watu viwe safe.
 
Back
Top Bottom