Marubani wachunguzwa Uchina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marubani wachunguzwa Uchina

Discussion in 'International Forum' started by MasterMind, Sep 7, 2010.

 1. MasterMind

  MasterMind Senior Member

  #1
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Marubani wachunguzwa Uchina

  Uchina imeanza kuwachunguza marubani wake wote wanaohusika katika safari za ndege za abiria, kufuatia madai kwamba zaidi ya marubani mia mbili walitumia vyeti vyenye maelezo ya uwongo, kuhusiana na ujuzi na maarifa yao ya urubani.

  Idara ya safari za ndege iligundua kwamba zaidi ya marubani mia moja waliotoa maelezo ya uwongo walikuwa ni wafanyikazi wa shirika la ndege la Shenzhen, kampuni kuu iliyosimamia shirika la ndege la Henan, ambalo ndege yake ilianguka mwezi uliopita, na kusababisha vifo vya watu arubaini na wawili.

  Zaidi ya watu 54 walinusurika baada ya ndege hiyo kukosea njia.
  Kati ya mwaka 2008 hadi 2009, inaelekea maelezo kuhusiana na historia ya kikazi ya zaidi ya marubani 200 wanaohusika na ndege za abiria ni ya uwongo, na wengi wakitia chumvi juu ya maarifa yao.

  Ripoti hiyo inaelezea kwamba kati ya marubani wanaohusika ni wale waliokuwa wakiendesha ndege za kijeshi, na baadaye kuanza kuendesha ndege za abiria.
  Baada ya kugunduliwa, marubani hao wanakatazwa kufanya kazi, hadi watakapokaguliwa na kutahiniwa tena.

  Sekta ya safari za ndege nchini Uchina imekuwa ikiimarika kwa kasi mno, na kila mwaka mamia ya marubani uhitajika.


  Source: BBC Swahili
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Hivi rubani akiwa ametumia cheti cha kughushi halafu akawa na rekodi bora maradufu ya kurusha ndege zaidi ya rubani mwenye cheti halali, kuna umuhimu wa kumuandama?

  Nafikiri waongeze uangalifu katika kuwapa urubani marubani wapya, na marubani waliopitisha uzoefu fulani waachiwe. Experience is the best teacher, no certificate can make up for hands on experience. Ukifikia uzoefu fulani kazi yako haipimwi kwa cheti chako, inapimwa kwa matokeo ya kazi.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kumbe makanjanja wapo kila nchi!..huh!...
  Ingekuwa ni Tanzania tungeongea hadi kwa lugha za malaika kulaani hii maneno!
  All in all, rubani wa ndege ya Abiria anatakiwa kuwa na kiwango cha juu kabisa cha uelewa katika ngazi za urubani ili apate leseni ya commercial, jambo ambalo wengi linawatesa, na hivyo kutafuta njia za mkato!
   
 4. MasterMind

  MasterMind Senior Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kiranga: experience might be the best teacher, lakini kama mtu anaweza akawa na ujuzi mzuri ambao ni kwa faida ya wengi, kwanini asifuate normal procedures ili kuhakikisha usalama wake na wale anaowabeba, kwa maana kitu chochote ambacho kinahusisha maisha ya wengi ni bora kufuata taratibu halali.

  Credibility ya mtu haiji tu kwa uzuri wa kazi anayofanya, lakini pia to the level of honesty or loyalty to his/her profession.
   
 5. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  China, China

  Marubani makanjanja, maziwa ya watoto feki, bidhaa substandard madukani tele, nk, nk - Tujihadhari na wachina!
   
 6. MasterMind

  MasterMind Senior Member

  #6
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  PakaJimmy: Ni kweli, lakini pia mi naona kinacho sababisha pia ni watu kutokuwa wavumilivu.
  Wingi wa procedures ama urefu wa procedures unamfanya mtu afikirie kwamba ili kurahisisha mambo basi
  afate njia za mkato.....lakini hili si sahihi! mtu lazimwa apimwe kihalali ili ajulikane uwezo wake wa kufaya kazi....si ndio?
   
 7. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Jamani hawa wachina hawa fogery kila sehemu. Mi nilidhani ni kwenye bidhaa tu!
   
 8. Steang

  Steang JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2016
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 343
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Naweza uliza swali bei ya mafuta ya ndege na tofauti ya ptrol au diesel?
   
 9. SirChief

  SirChief JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2016
  Joined: Jun 23, 2014
  Messages: 1,705
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Na hapo ndo huwa watu wengi wanakosea sana..
   
Loading...