Martha Gwau awafunda Wakinamama na Mabinti wa Shule Siku ya Wanawake Duniani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,074
998
MBUNGE MHE. MARTHA GWAU AWAFUNDA WAKINAMAMA NA MABINTI WA SHULE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Mhe. Martha Gwau, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Singida alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliofika shule ya Sekondari Ilongero kuzungumza na kusikiliza midahalo miwili ya mabinti wa shule pamoja mdahalo wa wazazi, midahalo yote ililenga kukomboa kizazi chetu kutoka kwenye makuzi yasiyofaa na ukatili kwa watoto wetu.

Mbunge huyo ambaye ndiye aliyekuwa mgeni ramsi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa Ilongero Singida vijijini.

Mbunge huyo aliwasihi sana wazazi kutokuwa sehemu ya kuficha watu wanaoharibu watoto wetu vilevile kuwa askari namba moja wa kuwalinda watoto na kuwapa malezi mema yatakayowaandaa kuwa raia wema kwa taifa, vilevile aliwataka wakina mama wachangamkie fursa mbalimbali za serikali lakini wajitahidi sana kutunza uaminifu

Mwisho, aliishukuru na kuipongeza halmashauri chini ya mkurugenzi wao Bi. Esther Chaula kwa maandalizi mazuri ya maadhimisho hayo.

Imetolewa na;
Ofisi ya Mbunge Viti Maalum Mkoa Singida

#MarthaGwauKazini
#KaziIendelee

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…