PetCash
JF-Expert Member
- Mar 20, 2012
- 1,997
- 1,998
Nawaza, ndoa nyingi tulizo nazo ama zimepangwa au watu wamependana kiukweli. Kwa mfano watu wanamuona uliyempenda haja 'qualify' na wewe wakikulazimisha umuoe/uolewe na wanaomuona ka'qualify' wewe hujampenda (ila kwa vigezo vya kuingilia ndoani anavyo vyote).
-> Ndani ya ndoa na uliyempenda kila mkitoka watu wanawasema na saa nyingine kumuambia mmojawapo,'wewe hukumstahili yule/ndugu yetu'. Sasa, hii huleta stress ndani ya ndoa na saa nyingine kutoelewana. Mwishowe mjumlisho wa mikwaruzano ya mara kwa mara ikaweka ndoa mashakani...
->Ndoa ya kupangwa mikwaruzano huanza kwa ndani, hii nadhani wengi wanaielewa zaidi na mara nyingi huingia mashakani..
Sasa tujadili uzito wa kuwa na vigezo vya kuwa mme/mke kwa kuulinganisha na ule wa kupenda/kupendwa..
mikwaruzo ya kuanzia ndani kwa ulinganisho na ile ya kuanzia nje..
a) najua mtasema oa / olewa na umpendaye ila dunia hii haiko hivyo watu wengi (marafiki zangu wa karibu) wameachwa broken hearted na watu wakaenda oa/olewa na wenye vigezo (uwezo wa kipesa na busara za kulea familia).
b) okay mtasema usisikilize ya watu...ila kumbuka hawa si watu wa kawaida tu! ni viongozi wetu wa kiroho(kidini), ni wazazi waliotuona tunakua na wanajua vitu tunavyohitaji ni marafiki/ndugu wa karibu sana.
Nawasilisha na kufungua rasmi mjadala...