Marmo Abariki Uharamia wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marmo Abariki Uharamia wa CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Albedo, Jun 20, 2010.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Yaani kila inachofanya CCM bwana Marmo anakibariki na kuwa ni Sehemu ya Maisha au Kanuni za Uchaguzi, kaaazi Kweli kweli

  Marmo aruhusu vyama vya siasa kampeni ya nyumba kwa nyumba

  Na Muhibu Said
  19th June 2010

  [​IMG]
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo.

  Serikali imesema vyama vya siasa vinaruhusiwa kufanya kampeni nyumba hadi nyumba na kuorodhesha majina ya watu walioandikishwa, lakini haviruhusiwi kuchukua kadi za wapigakura.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, alisema hayo wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa hotuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya matumizi ya fedha ya ofisi ya Waziri Mkuu na ofisi ya Bunge ya mwaka 2010/11, bungeni jana.

  Wabunge waliochangia eneo hilo, ni pamoja na Dk. Willibrod Slaa (Karatu-Chadema), Mgana Msindai (Iramba Mashariki-CCM), Masoud Abdallah Salim (Mtambile-CUF), Lucy Owenya (Viti Maalum-Chadema) na Ismail Jussa Ladhu (Kuteuliwa na Rais-CUF), ambao baadhi yao waliitaka serikali itoe tamko kukemea viongozi wa CCM kuwafuata wananchi majumbani na kuorodhesha kadi za wapigakura na kuandika namba zake kwenye fomu maalum.

  Waziri Marmo alisema wajumbe wa vyama vyote vya siasa wanaruhusiwa kuwafuata wananchi na kuwahamasisha katika kuwashawishi ili wawapigie kura na kufanya kampeni nyumba hadi nyumba.
  Alisema sheria za uchaguzi hazikatazi vyama kuorodhesha majina ya watu walioandikishwa na kwamba, kinachokatazwa ni kuchukua kadi za wapigakura.

  Kutokana na hali hiyo, alisema iwapo kuna vyama vinavyochukua kadi za wapigakura, taarifa ya suala hilo itolewe ili hatua zinazostahili zichukuliwe.

  Kuhusu madai katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Biharamulo, mkoani Kagera na ule wa Busanda, mkoani Mwanza, uliofanyika mwaka jana, kwamba kadi za wapigakura zilichukuliwa kwa nguvu, alisema taarifa zilipelekwa polisi na baada ya uchunguzi, walibaini kuwa waliolalamikiwa walikuwa wameorodhesha majina tu ya wanachama wao na hawakuchukua kadi yoyote ya mpigakura na kwamba, kwa kuwa kuorodhesha majina siyo kosa, watu hao waliachiwa.

  Alivitaka vyama vya siasa vyenye wajibu wa kuteua wagombea, kuteua wanawake wengi na kwamba serikali itaendelea kuvishauri kuwa kwa sasa lengo la serikali ni kwamba, asilimia 40 ya watakaokuwa wabunge katika Bunge lijalo, ni wanawake.

  Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa kuondolewa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na kuwekwa chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Marmo alisema jambo hilo kwa sasa haliwezekani.

  Alisema Katiba ya nchi imeipa NEC mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani Tanzania Bara, hivyo haina mamlaka ya kusimamia uchaguzi kwa serikali za mitaa.

  Alisema uchaguzi huo unasimamiwa na Halmashauri husika chini ya Tamisemi kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za mitaa namba 7 na 8 za Mwaka 1982 na kwamba, serikali inaamini utaratibu huo unakidhi haja na utaendelea kutumika.

  Kuhusu NEC kutoa taarifa zaidi ili kuepusha ubambikiaji wa kesi kwa viongozi wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi, alisema kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi sura ya 343, imepewa mamlaka ya kuandaa maadili ya uchaguzi baada ya kushauriana na vyama vya siasa na serikali.

  Waziri Marmo alisema hivi sasa NEC iko katika mchakato wa kuandaa maadili hayo na kwamba, pamoja na mambo mengine, maadili yanakataza ubambikiaji wa kesi wakati wa uchaguzi.

  Alisema maadili hayo yakishakamilika, itatangazwa kwa wadau wote ili yaweze kufahamika na kwamba, vyama vyote vya siasa, serikali ikiwamo, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na NEC, watawajibika kutekeleza maadili hayo kwa baadaye.

  Kuhusu serikali kukemea lugha chafu wakati wa uchaguzi, alisema inakatazwa na sheria za uchaguzi na kwamba, serikali itachukua hatua kwa atakayekiuka maadili hayo.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi huyu mzee ana akili kweli au?mi simuelewi kabisa
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huyu Mzee ameamua kuifanya Wizara yake kuwa moja kati ya Kamati za Ushindi za CCM, sioni Mantiki ya kwa nini watu waorodheshe wapiga kura ili iweje, ili iwafamu then iweje sasa na wakati kura ni Siri ya mtu

  Hapa Mtu Mzima Marmo amechesha kweupe, Yaani amejivua Nguo na kujionesha ni vipi alivyo mtupu hata katika Mambo ya Kutumia Common sense, yaani hii nchi watu wamekuwa wanatafuta Majibu Marahisi kwa Matatizo Mazito, yaani ukishindwa Kumdhibiti mtu basi una bariki Matendo yake, ni sawa na Ewura wanashindwa kuwadhibiti wachanganyaji wa Mafuta wao sukuhisho la Raisi ni Kupandisha Kodi ya Mafuta ya Taa pasipo kuangalia athari zake kwa Wananchi ambao hata magari hawapandi
   
 4. M

  Malunde JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Bado hakuna demokrasia ya kweli katika nchii, kwa miaka mingi na sehemu nyingi(ukiachilia mbali maeneo machache) watu wamekuwa wanachanguliwa viongozi na si wao kuchagua viongozi.Hii inaanzia ndani ya vyama na hata kwa wapiga kura wote kwa ujumla.Kuruhusu wagombea waorodheshe wapiga kura ni kuwaondolea uhuru wao wa kupiga kura.Kampeni zitakuwa za vitisho hasa vijijini. Chama fulani kinaweza sema "tunaorodha yenu wote, na ole wenu msipotupigia kura". Ninavyowafahamu watu mfano wa kule kwetu watasema "Nduhu tabu"( No problem) tutakupga kura, kwa sababu hawataki matitizo na mtu na yale ya kwao yamekuwa sehemu yao.

  Hii ni sumu inayoendeleaza mauaji ya demokrasia; nani anaweza kuwatapisha watu wa vijijini sumu hii
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  NEC ( National Electoral Committee) = NEC ( CCM National Executive Council)
   
 6. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sioni tatizo lolote hapa, strategically ni muhimu kwa vyama vya siasa kuwajua wapiga kura watarajiwa ili kuepuka kupoteza muda mwingi kwa watu ambao hawatapiga kura.
   
 7. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Nyie hapo juu mimi ndiyo ninawashangaa kama akili mnazo. Marmo anachosema ni kuwa wakati wa kampeni wewe ukiwa mgombea hakuna ubaya kuwafahamu wapiga kura wa eneo lako. Hii inakusaidia kimkakati hata kufanya permutation ya iwapo utashinda au la. Haya mambo hata CHADEMA na CCM walifanya kama kule Karatu kwenye chaguzi zilizopita. Wagombea wanaweza hata wakafahamu katika kila kaya nani anawaunga mkono au nani hawaungi. Sasa nyinyi mnashangaa nini.
   
Loading...