Mark Mwandosya akosoa wanasiasa waasi wanaorudi CCM na kupewa madaraka, asema zamani waliorudi wangepita kwenye mafunzo ya itikadi

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Kada wa CCM na Mbunge Mstaafu wa Rungwe Mashariki (Busokelo), Prof. Mark Mwandosya, akiongea na Mwananchi jana tarehe 02.08.2018, alidai hama hama ya wanasiasa inatokana na Vyama kukosa itikadi, dira na sera inayotakiwa na jamii tangu kumalizika kwa Vita Baridi kati ya Nchi za Magharibi na Mashariki.
Mwandosya aliyeingia katika top 3 ya Wagombea urais wa CCM mwaka 2005, alieleza kuwa, kujenga jamii inayotakiwa kunahitaji ufafanuzi wa itikadi na sera za uchumi zinazoambatana na itikadi hiyo, ambapo hapo awali, sera zilijikita kwenye ukabaila (ubepari?) na usoshalisti (ujamaa). Alisema kwa sasa, mfumo wa uchumi unaongozwa na soko, hivyo kinachofanyika ni Vyama kujaribu kupata itikadi kutokana na mfumo badala ya itikadi kuongoza mfumo wa uchumi. Hali hii imesababisha wananchi na wanasiasa kutoona tofauti yoyote kwa Vyama, hali inayosababisha wanasiasa kuhama muda wowote.
Hata hivyo, Mwandosya aliongezea kuwa, "Watu anaowakuta ndani ya Chama husika wanaona "walioasi" wanarudi na kupanda ngazi haraka." Alidai zamani waliohamia CCM, walipewa kwanza mafunzo ya itikadi ili kuwapima.
IMG_5723.JPG

======

Dar es Salaam. Wakati kukiwa na wimbi la wanasiasa kuhama vyama vya siasa na kuhamia vingine, waziri wa zamani katika Serikali za awamu ya tatu na nne, Profesa Mark Mwandosya amesema ‘hamahama’ hiyo inatokana na vyama kukosa itikadi, dira na sera inayotakiwa na jamii.

Profesa Mwandosya ameyasema hayo ikiwa ni siku chache tangu wabunge wawili wa Chadema kujiuzulu nyadhifa na uanachama wao na kuhamia CCM.

Wabunge waliohama ni Julius Kalanga wa Monduli na Mwita Waitara wa Ukonga. Pia wapo madiwani zaidi ya 50 wa CUF, ACT-Wazalendo na Chadema waliohamia chama hicho tawala hivi karibuni wakidai kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

Akizungumza na Mwananchi jana, Profesa Mwandosya alisema hamahama ya vyama inatokana na changamoto inayovikabili vyama vya siasa barani Afrika na nchi zinazoendelea.

Pia alisema kuhama huko kwa wanasiasa kunatokana na vyama kukosa itikadi inayovisimamia, kwa maana ya mwelekeo na dira pamoja na aina ya jamii ambayo nchi husika zingependa kuijenga.

“Akikaa huko (katika chama alichomo), anaamua kurudi na kupokewa kwa shangwe (katika chama cha awali) mithili ya mtoto aliyepotea katika vitabu vitakatifu. Na kwa sababu anakohamia wanatafuta kuongeza namba, basi inaeleweka kwa nini anapokelewa kwa shangwe,” alisema.

Profesa Mwandosya alifafanua kuwa katika mazingira hayo ni vigumu kutoa sababu za msingi za kiitikadi na kiimani za wanasiasa kurudi katika vyama vya awali, bali mara nyingi ni za kibinafsi zaidi.

Alisema kibaya zaidi mwanasiasa anakorudi kuna watu ambao hata katika mazingira aliyoyaeleza wameendelea kubaki na kukitumikia chama anachohamia.

Alisema watu anaowakuta ndani ya chama husika wanaona “walioasi” wanarudi na kupanda ngazi haraka.

“Jambo hilo limekuwa dhahiri sana baada ya mwisho wa vita vya baridi kati ya nchi za Magharibi na za Mashariki,” alisema mwanasiasa huyo aliyewahi kujitosa kuomba kuteuliwa na CCM kugombea urais mwaka 2005.

Profesa Mwandosya alisema kujenga aina ya jamii inayotakiwa kunahitaji ufafanuzi wa itikadi na sera za uchumi zinazoambatana na itikadi hiyo. Alisema awali sera hizo zilijikita katika ukabaila au usoshalisti.

“Na kila nchi zilitafsiri nini maana ya itikadi na sera hizo katika mazingira yake. Lakini ilivyo sasa, mfumo wa kiuchumi unaongozwa kwa misingi ya soko. Kinachofanyika ni kujaribu kupata itikadi kutokana na mfumo wa uchumi badala ya itikadi kuongoza mfumo wa uchumi,” alisema.

“Vyama vimejikuta katika ombwe la tafakuri hiyo kiasi cha kwamba kushika dola kunakuwa ndio msingi wa kuwepo kwa vyama. Kinachotokea ni kwamba wananchi na wenye nchi hawaoni tofauti za vyama kwa misingi niliyoelezea.”

Alieleza kuwa kutokana na sababu hizo viongozi na wanachama wanaweza kuhama wakati wowote kwenda chama chochote.

“Kwani bila misingi ya kiitikadi, imani ya msingi haipo na masilahi yanakuwa kiini cha maamuzi. Katika hali hii mtu anatoka chama kimoja anaenda kingine, tena kwa jeuri kabisa,” alisema.

Aliongeza kuwa, “sina uhakika kwa kuwa wao ni binadamu wataridhika na hali hiyo. Kwa kawaida, hapo zamani wanaorudi kundini wangepita kwanza kwenye mafunzo au madarasa ya itikadi ili kuwapima kwanza.”

Alisisitiza kuwa ombwe lililopo linatokana na changamoto ya kiitikadi inayoendelea na si kwa Tanzania tu, bali nchi nyingi zinazoendelea.

Miongoni mwa wanasiasa waliohama vyama vyao katika siku za karibuni ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu aliyehamia Chadema.

Wengine ni aliyekuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia na wa Siha, Dk Godwin Mollel (Chadema) ambao walihamia CCM, kisha wakateuliwa na chama hicho kugombea tena ubunge katika majimbo hayo na kushinda tena.
 
Mwandosya anza kuwauliza CHAGADEMA walipompokea Lowasa na Sumaye waliwapa mafunzo gani ya kiitikadi hadi wakawapa vyeo hump CHADOMO na wengine wakagombea Urais
Unachanganya sukari na chumvi. CHADEMA haijawahi kushika dola na CCMimeshika dola zaidi ya miaka50 unatakiwa isome mazuri na yenye faida siyo ku kopi kila kitu kutoka CHADEMA.
Kwa hiyo CCM Ian kopi kila kitu kutoka CHADEMA. Mpaka makosa wanaojifanya lazima wa kopi
 
Kinachoangaliwa zaidi ni uwezo wa kuongoza, na si idadi ya siku ngapi umekaa CCM. Na katika kuthibisha hilo watu kama Prof Mkumbo na Bi Anna wamepewa nafasi serikalini huku wakiwa vyama vya upinzani. Hata hao anaosema wachaguliwe wakiwa wameshapewa mafunzo ya chama mbona tumeona wakongwe wa chama wakiwa ndio wa kwanza kwenye kuvurunda.
 
Mwandosya anza kuwauliza CHAGADEMA walipompokea Lowasa na Sumaye waliwapa mafunzo gani ya kiitikadi hadi wakawapa vyeo hump CHADOMO na wengine wakagombea Urais
Mwandosya anaongea haya nadhani kwa kuumia na kuwatetea wana-CCM waliokosa fursa. Hakuna kiongozi angewaacha wanasiasa wazuri na muhimu kama Kafulila na Katambi eti kwa kuwa wametoka Upinzani.
Kama hukuteuliwa na Rais tangu teuzi za RCs, DCs, DEDs, Directors, unataka uteuzi gani tena? Waache wazuri wateuliwa kama ulikuwa mzuri kwa Kikwete siyo guarantee ya kuwa mzuri kwa Magufuli, that's all.
So, Mwandosya ameyasema hayo akiwa na kinyongo moyoni, hiyo ni lazima akubali.
 
Mwandosya anza kuwauliza CHAGADEMA walipompokea Lowasa na Sumaye waliwapa mafunzo gani ya kiitikadi hadi wakawapa vyeo hump CHADOMO na wengine wakagombea Urais
Yeye ameongelea CCM ilikuwa na utaratibu huo, sasa unapomuambia aongelee CDM yeye hajawai kuwa mwanachama wao na itikadi yao haijui. Acha porojo kwenye hoja za wajuvi wa mambo.
 
Mwandosya anza kuwauliza CHAGADEMA walipompokea Lowasa na Sumaye waliwapa mafunzo gani ya kiitikadi hadi wakawapa vyeo hump CHADOMO na wengine wakagombea Urais
Yeyote anayehoji asiyoridhika nayo ndani ya CCM, anaambiwa akaulize CDM... aiseee.... HIVI LINI MTAACHA KUHALALISHA MAKOSA YENU KWA KUTUMIA MAKOSA YA WENGINE?
 
hivi wanachama wa upinzani wameanza lini kurudi chama tawala na kupewa nafasi.Mwandosya anaongea kama ana wivu fulani kwa sababu alijifikiria yeye ndiye alistahili kuwa rais.
Ukweli hakuna chama ambacho sasa hivi kinatoa mafunzo ya itikadi kwa wanachama wake kwani baada ya vyama vingi kuingia kila chama kilitaka kuwa na mtaji wa wanachama wengi lakini kama vyama hivyo vingekuwa vinafundisha itikadi wanachama wao kabla ya mfumo wa vyama vingi kuingia niwazi tusingeona maigizo yanayofanyika sasa hivi lakini cha ajabu Mwandosya hakuliona hilo
 
Uzee saa mingine taabu kweli. Sasa yeye anajuaje kuwa hawa jamaa mafunzo ya ukada na kunyweshwa maji ya bendera hawakuyapata kabla hata ya kuwa wanachama wa vyama wanavyo vihama na kurudi ccm.

Mh Rais kishasema hawa ni vifaru vilivyotekwa vitani bado tu hajamuelewa? Kifaru Kafulila na kifaru Machali tayari viko msatari wa mbele katika uwanja wa mapambano wa kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi hii.

Mwikabe si anaweza kuwa kada kuliko hata huyo Prof?
 
Back
Top Bottom