MARIJANI RAJABU: Miaka 18 sasa Jabali bado lipo imara

Inasemekana husda ndio iliyomuondoa Safari Trippers inasemekana wazee wengi waliopo pale hawakupenda kung'ara kwa nyota ya Marijani
Alichofanya Marijani hakuchukua wanamuziki alichukua wapenzi wa muziki akawakusanya akawa train baada ya muda akaenda kuperform ktk eneo la wazi kiingilio bure na mojawapo ya kibao kipya alichoporomosha siku hiyo kulikuwa "Mayasa" hapo ndipo jina la "JABARI LA MUZIKI" liliposadifu
Kuhusu wimbo wa "Mama Watoto" inasemekana aliuimba kuakisi ya nyumbani kwao kwani mama yake alifariki muda si mrefu baada ya kuzaliwa kwake hivyo alilelewa muda mrefu na mama wa kambo ambaye alikuwa aki mnyanyasa sana kufikia kiasi cha kumtungia wimbo huo akijifanya ywye kama ndiyo baba akimuasa mkewe
 
1. Mbona inasemekana aliyetunga wimbo wa Georgina siyo Marijani Rajab ila ni Jumanne Uvuruge ila yeye Marijani aliimba tu? Ukweli ni upi? 2. Pia inadaiwa aliyekuwa na uhusiano na Georgina siyo Marijani ila ni rafiki yake aliyekuwa akisoma nae kidato cha pili pale Tambaza na kwamba binti alirudishwa kwao Iringa baada ya kupata ujauzito kutoka kwa huyo rafiki yake na Marijani akiwa kidato cha pili Zanaki Secondary jijini Dar na siyo kwamba alihamishiwa shule ya bweni. Maelezo mengine yanayomhusu huyo Georgina ni kwamba alikuwa mtoto wa kaka yake na waziri Dr. Mahiga na kwamba alifariki na kuzikwa wiki hii jijini Dar.
 
1565074890661.png
 
Dah we mkali mkuu, kwa picha hii uliyoweka ni ushahidi tosha kuwa hamkufahamiana barabarani. Jamaa namkubali sana hasa nnaposikiliza nyimbo za Siwema namba 1 na 2 pamoja na Salama. Apumzike kwa amani.
Yenye No. 1 na No. 2 ni Mzee Saidi, Siwema haina No.1 na No.2
P
 
MARIJANI Rajabu ingawa hatunaye tena hapa duniani, wapenzi wa muziki wa dansi hapa nchini hata nchi za jirani hawatamsahau kamwe.

Alikuwa miongoni mwa wanamuziki waliotoa mchango mkubwa wa maendeleo ya nchi, ikiwamo elimu kupitia tungo za nyimbo zake maridhawa zilizokuwa zikiendana na wakati.
Alifariki dunia Machi 23, 1995 na mwili wake ukazikwa siku iliyofuata Machi 24, 1995 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mungu aiweke roho yake pahala pema peponi. Amina.
Machi 24 mwakani, Marijani Rajabu anatimiza miaka 25 ya kifo chake, mimi nikiwa Mtangazaji Kijana mdogo wa RTD, nilifanya Radio Documentary ya kifo na mazishi yake. Hicho ndicho kilikuwa kipindi changu cha mwisho RTD nikaacha kazi.

Mwakani napanga kumuandimisha kwa namna fulani. Pia nita replay hiyo 25 years old Radio Documentary ya Marijani Rajabu.
P
 
Machi 24 mwakani, Marijani Rajabu anatimiza miaka 25 ya kifo chake, mimi nikiwa Mtangazaji Kijana mdogo wa RTD, nilifanya Radio Documentary ya kifo na mazishi yake. Hicho ndicho kilikuwa kipindi changu cha mwisho RTD nikaacha kazi.

Mwakani napanga kumuandimisha kwa namna fulani. Pia nita replay hiyo 25 years old Radio Documentary ya Marijani Rajabu.
P

Muziki wake ulikuwa murua....RIP. alikuwa mahiri mno
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom