Maria Sarungi na Barack Obama ni sawa na Mbingu na Ardhi?!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2016
Posts
1,886
Reaction score
5,623
Awali ya yote nachukua fursa hii kutoa pole kwa familia , Wana - Rorya na Watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na Mzee wetu , Daktari Bingwa wa Mifupa Professor Philemon Mikol Sarungi.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Mengi yamesemwa tayari kuhusu Professor Sarungi na mengi yataendelea kusemwa kuhusu yeye.

Kama Kuna kiongozi Mzalendo, Mwadilifu na Mchapakazi ambaye msiba wake haujatendewa haki na Taifa hili basi ni msiba wa huyu Profesa Nguli wa Mifupa siyo tu Tanzania bali Duniani.

Kipindi cha nyuma ambako ajali za mara kwa mara katika barabara ya Morogoro kati ya Morogoro na Dar es Salaam zilikuwa zikitokea kutokana na ubovu wa Barabara hiyo, ulikuwa hukosi kusoma katika magazeti kuwa ajali mbaya imetokea na majeruhi wamekimbizwa Hospitali ya Tumbi na Profesa Philemon Sarungi , Daktari Bingwa wa Mifupa ameongoza jopo la Madaktari katika kuokoa maisha ya majeruhi hao.
Nadhani wakati huo pia alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Huyo ndiye Profesa Philemon Mikol Sarungi ambaye pamoja na Rais wetu tunayempenda sana Dr.Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mwepesi sana kutoa salamu za pole kwetu Watanzania kufuatia misiba inayotokea kama ya Watangazaji wa radio na television, wachekeshaji,wanamuziki n.k alishindwa kutupa pole sisi Watanzania kwa kuondokewa na Nguli huyu Professor Philemon Mikol Sarungi.

Hakuna sababu yoyote yenye mashiko kwa mtu mwenye akili nzuri inayoweza kuhalalisha kutotolewa salamu za pole na Mheshimiwa Rais wetu kufuatia sisi kuondokewa na Daktari Nguli huyu wa Mifupa.

Profesa Sarungi alishavuka level za kuwa handled kwa "grudges" za familia yake.
Huyu alikuwa ni Hazina ya Taifa hili.
Kama Rais wetu alishauriwa kutotoa salaam za pole basi huo ni moja ya ushauri mbaya aliowahi kupewa na waliotoa wanastahili adhabu.
Kama alijielekeza mwenyewe basi Rais wetu mpendwa alijielekeza vibaya sana!

Na hapa ndipo nasema Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wewe ni " mtu na nusu" na hata nilipokuona tena umekaa na Mhe.Tundu Antipas Lissu Mwenyekiti wa CHADEMA katika msiba wa Profesa Sarungi na nikarudia tena kuangalia ile picha maarufu ukiwa pale Ikulu kama Rais wa JMT umewaalika viongozi wa CHADEMA Ikulu , ukiwa umesimama na Mhesh.Tundu Lissu akikoroga kikombe cha chai na wewe ukimtazama kwa bashasha!
Hakika kwa roho uliyonayo Dr.Jakaya Mrisho Kikwete tunakuombea maisha marefu sana!

Watu wasisahau kwamba Hayati Baba wa Taifa Julius K.Nyerere alifariki akiwa na miaka 77 tu !! Wewe Leo una miaka 75 lakini kwa mwonekano utadhani uko kwenye early 60s!!
Ungekuwa hapo Kenya bado wewe ni hopeful Presidential Candidate!!

Hata nilipomwona mwanao Mhe.Ridhiwani Kikwete kaongoza mazishi ya Professor Philemon Mikol Sarungi nikajua tu huo ni " mkono wako" katika kuficha " aibu" hiyo!
Kwa kweli Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wewe ni " mtu"saaaana na hatusubiri ufe ndo tukusifie, kaa Baba ukijua wewe ni tunu na hazina ya Taifa letu.

Sasa naomba nirudi kwenye kichwa cha makala haya;
Nimefuatilia malumbano, masimango, mabezo kati ya akina Kigogo wa X ( zamani Twitter) , mapungo , Juma Ayo wa Crown media , watu mbalimbali nilioongea nao kufuatia Kifo cha Profesa Philemon Mikol Sarungi na mazingira duni aliyokuwa akiishi kulinganisha na ukubwa wa jina, hadhi,elimu yake na kelele za Maria Sarungi mitandaoni.

Ukweli usio hitaji degree kutoka Harvard ni kwamba ni kweli Professor Philemon Mikol Sarungi ALITELEKEZWA NA WATU WAKE WA KARIBU HASA WANAWE!!
Na hili kwa watu wenye akili linamwondolea kabisa MARIA SARUNGI uhalali wa kuendelea kupiga kelele mitandaoni kwamba anakosoa Serikali na kupigania haki UCHWARA za watu!!
Msemo huu uko wazi kwamba CHARITY BEGINS AT HOME!

Maria Sarungi na ndugu zako mnawezaje kuacha Mtu maarufu kama Professor Philemon Mikol Sarungi akafia katika mazingira duni vile?! SHAME ON YOU!!!

Harakati za Maria Sarungi ni non sense na watu wengi wamempuuza , michango ya rambirambi alizopata pamoja na kutumia nguvu kubwa ni ushahidi tosha ( hakupata zaidi ya milioni 3 , AIBU!!!)

Kibaya zaidi Maria Sarungi anabishana na watu kama Juma Ayo wa Crown media aliyemwambia kuwa kwa tamaduni za kijaluo na hadhi ya Profesa Philemon Mikol Sarungi hakupaswa kuzikwa Kinondoni Makaburini kitu ambacho ni kweli kabisa!

Kuna Mzee mmoja wa Kijaluo aliwahi kuniambia kwa kijaluo kwamba ," Jaluo mo iki e limbo chalo ng'amo ondiegi ochamo"!
Kwa tafsiri yake kwamba " Mjaluo aliyezikwa makaburini ( makaburi ya halaiki) ni sawa na mtu aliyeliwa na fisi / mafisi".
Kwahiyo Maria Sarungi akae akijua kuwa Profesa Philemon Mikol Sarungi aliyezikwa pale Kinondoni Makaburini kwa tamaduni za Kijaluo ni kama ametupwa na ameliwa na mafisi. It pains but Maria with your mediocre fellows bear that bitter truth!!

Miaka ya mwanzoni mwa 1990 nilifika Dar es Salaam na nikafikia familia fulani ya Kijaluo.Familia hiyo ilikuwa na mtu mmoja akifanya kazi katika Kampuni moja kubwa ya Clearing and Forwarding ikiitwa SAOLIGO HOLDINGS LTD alinisimulia mambo mengi kuhusu Kampuni hiyo.
Nilipomuuliza kuhusu nini maana ya SAOLIGO aliniambia anachojua yeye ni kwamba SAOLIGO ni kifupi cha majina ya watu, na watu anaojua yeye ni wenye SAOLIGO ni Profesa Sarungi, OTIENO Igogo na miamba mingine ya Kijaluo.

Sasa katika msiba huu duni na mazingira duni aliyofia Profesa Sarungi mbona sikuona mikono ya miamba hiyo!?

Miaka ya 2000 nadhani Profesa Sarungi akiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alikuwa akialikwa na Umoja wa Wanafunzi wa Rorya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( MORI Association) nami niliwahi kualikwa nikakutana naye akiwa na huyo mkewe Mzungu ( Mama Maria) Kuna kitu nilijifunza kutoka kwa Profesa Sarungi.
Alikuwa ni mtu mkarimu sana lakini asiyependa sana maingiliano na watu pengine labda sababu ya kuoa mke mzungu!!

Pamoja na kutelekezwa na watoto lakini inavyooneka kutokana na uduni na uchakavu wa mazingira aliyokuwa akiishi Professor Sarungi inaonekana nyumbani kwake hapakuwa na wageni wa mara kwa mara ambao wange detect mapungufu yaliyokuwa yamemzunguka.

Kwa msitu ule ulioko nyumbani kwa Profesa Sarungi kukuta nyoka au hata chatu ni kitu cha kawaida sana!!

Kwa ufupi Profesa Sarungi alifaulu sana katika tiba ya Mifupa ya binadamu lakini alifeli big-time katika mentorship ya watoto hasa Maria Sarungi.

Turudi kwa Barack Obama ambaye naye ni half- cast wa Kijaluo kama alivyo Maria Sarungi.
Barack Obama anasema akiwa mdogo anakumbuka Baba yake (Barack Obama Sr) alimpelekea santuri za muziki wa Kijaluo na mpira wa Basket ( Basketball).
Soma kitabu chake cha Dreams from my Father ambacho kwa Kijaluo ni " Lek ma aa kwom wuoraa" ( Ndoto kutoka kwa Baba yangu).

Kwahiyo Baraka Obama Sr ( Mjaluo Mkenya) alifanya mentorship kwa Barack Obama Jr ( Mjaluo Mmarekani) kiasi ambacho alikuwa akipata ndoto kutoka kwa Baba yake baada ya kufariki. Hivyo Chemistry ya Obama Sr na Obama Jr iko juu sana mpaka kesho!
Professor Sarungi sidhani kama aliwafanyia akina Maria Sarungi mentorship yoyote that's why unaona hawana Chemistry yoyote na Baba yao , watoto wanashindwaje kuja kumzika Baba yao , ujinga mtupu!!

Uko hapo Kenya unashindwa kuja kumzika Baba yako eti unatoa sababu za kipuuuzi eti sijui usalama wako sijui ujinga gani!!?

Maria Sarungi siyo threat na hana umuhimu anaojipa kwa Taifa hili na wala sidhani kama Kuna mtu kwenye system mwenye time naye!

Barack Obama baba yake alifariki akiwa ndo anajoin University na baadaye mwaka 1987 akaja Kogelo - Kisumu Kenya kuhani msiba wa Baba yake.

Anaelezea vizuri sana jinsi dada yake Dr.Auma Obama alivyokwenda kumpokea na kigari chake cha Volkswagen (Kobe) airport.

Alipokuwa Rais wa Marekani Barack Obama alizuru Kenya na ktk kuwashangaza watu Duniani aliruhusu Dada yake ( Half sister) Dr.Auma Obama kupanda naye pamoja ktk gari lake la Rais wa Marekani ( The Beast) na akasema anarudisha fadhila kwa Dada yake kwa hisani aliyofanya kwa kwenda na Volkswagen ( Kobe ) yake kumpokea alipokuja kwa mara ya kwanza Kenya mwaka 1987.

Obama Jr hata alipomwoa mkewe Michelle Robinson Obama alimwalika Baba yake mdogo Said Obama kutoka Kenya kwenda kusimamia Harusi yake kule Marekani.

Kuna Mjaluo mmoja kutoka Kogelo Kenya anasema Barack Obama alipotaka kugombea Useneta wa Illinois - Chicago Marekani alikuja kwanza nyumbani Kenya kutaka Baraka zao na akateta, tena kwa Kijaluo na Bibi yake ( Bibi.Sarah Obama).

Na aliposhinda Urais wa Marekani wakati wa kuapishwa kwake aliwaalika wengi kutoka Kogelo Kenya kwenda Marekani na baadaye aliwafanyia dhifa maalum kwa tamaduni za kijaluo ktk Ikulu ya Marekani ( White House), yaani wanasema kwa Kijaluo kwamba " no rwako gi mo yeng'o ne gi"! Yaani aliwakarimu na kuwachinjia" hapo Ikulu ya Marekani (White House).

Wajaluo hao kupitia msemaji wao ( Kogelo Spokesperson) walimshukuru Barack Obama na kumtania kwamba akija nyumbani ( Kenya,) watamtafutia mke mdogo ( dhako ma tin ) ili amzalie watoto wa Kiume watakao rithi nyumba ya Obama kama Michelle hataki kuzaa tena!

Wajaluo ni watu wakarimu na wapenda utani na majigambo sana!! Ndo maana wao na Wahaya utani wao unoga sana!!

Barack Obama Jr amebeba juu jina la baba yake kutokea Marekani lakini Maria Sarungi na ndugu zake wamezamisha jina la Hayati Profesa Philemon Mikol Sarungi matopeni na kumtupa pale Kinondoni Makaburini!

Baraka Obama Jr amefanya leo Kogelo Kenya kuwa sehemu maalumu ambayo ina msemaji rasmi na itifaki zake.

Leo kama ilivyo Las Vegas Marekani , Kogelo Kenya nayo Wajaluo wanapaita Las Kogelo kutokana na heshima ambayo Barack Obama Jr ameipa sehemu alikozikwa baba yake Barack Obama Sr.

Sidhani kwa akili mbovu ya Maria Sarungi na ndugu zake wana connection yoyote na Utegi!
Maria Sarungi and the likes are disgrace to the Luo Nation!

Profesa Philemon Mikol Sarungi nindi gikwee wuod Wategi e thim mo wiitiye.
 
huku ni kufirisika kwa akili au mawazo.

1- Hela ya rambi rambi - unasema haikufika mil 3 - jee huu ni ukweli kuwa Maria na familia yake walichangiwa mil 3 tu.?

- Mazingira aliyokuwa anaishi sarungi yananyoka - hii na yenyewe kweli ni jambo la kujadili.?

-Sarungi kukwama kimalezi , je amekwamwa wapi au kosa ni Maria sarungi kuongea ukweli ?

katika Uzi wako jambo ulilozungumza la maana ni moja kuwa hakuepewa mazishi ya heshima hiyo ni kweli Ila hayo mambo mengine unaongea tu ilimradi.

Kuhusu watoto kumtelekeza Baba yao je kwa akili yako unaona huu ni ukweli ?

Tukija katika kampuni unayoilalamikia iliyokuwa inafanya Kazi miaka ya early 90 kwa mujibu wako je Una uhakika hiyo kampuni bado ipo hai ?

🤔🤔🤔
 
Binadamu ni wanyama so kuishi na nyoka au fisi siyo Jambo la kushangaza maana watu wengi hasa waafrika wanaishi katika mazingira kama hayo na pia wote tunasubiri kufa na mbele ya kifo watu wote tuko sawa Kwa maana kifo hakiangalii hadhi ya mtu.
 
Miaka hiyo, Serikali ilimuweka Prof. Shaba hospitali ya Tungi kama Daktari Bingwa wa Mifupa kusaidia majeruhi kabla hawajaenda Muhimbili. Huyo Otieno Igogo ni ndugu yake kabisa na Prof. Sarungi. Ni tajiri fulani wa clearing and forwarding!
 
Kwanini anajishuku kuwa atakamatwa?
tuseme ukweli Maria Sarungi ni nini kinamfanya asije nchini?? Kwanini anajishuku kuwa atakamatwa? Na akamatwe kwa makosa gani?

Huwezi kuwa mwanaharakati kama wewe ni muoga. Sawa na mfanya biashara wa utumbo kuigopa nzi
 
Back
Top Bottom