- Source #1
- View Source #1
Wakuu
Je, ni kweli Maria Sarungi amesema CHADEMA imekufa mapema.
Je, ni kweli Maria Sarungi amesema CHADEMA imekufa mapema.
- Tunachokijua
- Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X kufanya uchechemuzi wa masuala mbalimbali.
Madai
Ipo taarifa inayosambazwa mtandaoni iliyotumia utambulisho wa grafiki za Jambo TV na kunukuu ujumbe uliodaiwa kuchapishwa na Maria Sarungi kwenye mtandao wa X kuwa CHADEMA imekufa mapema.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) ulibaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli bali ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani ujumbe ulionukuliwa haujachapishwa na Maria kwenye ukurasa wake wa X.
Vilevile grafiki iliyoyutumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi kwani hayajachapishwa na Millard Ayo kama inavyoonekana.