Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Edwin Mtei, Apr 26, 2011.

 1. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika mjadala unaoendelea wa marekebesho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna malalamiko na lawama zinazoanzia Zanzibar kwamba mpangilio na utaratibu wa sasa umemshusha hadhi Rais wa Zanzibar na kumfanya Waziri wa kawaida tu ktk Cabinet ya Muungano. Malalamiko hayo yanaonyesha kutoridhika na utaratibu unaotambulika kikatiba kwamba mgombea wa kiti cha u-Rais akitokea Bara kuna mgombea mwenza atakayekuwa Mzanzibari, na wakishinda ndiye atakuwa Makamu wa Rais kama Makubaliano ya Muungano yalivyotamka awali mwaka wa 1964.

  Lalamiko lingine ni kwamba kumekuwa na ma-Rais wanne wa JMT, lakini ni Rais mmoja tu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, aliyetokea Zanzibar. Licha ya kwamba Orodha ya Makubaliano ya 1964, hayakutamka hivyo, hawa Wazanzibari wanataka kuwe na zamu ya kupokezana uongozi mkuu wa JMT. Hawaridhiki na utaratibu wa kuwa na Mgombea mwenza ambao unahakikisha kwamba kama kiongozi mkuu akitokea Bara, makamu wake ni lazima atokee Zanzibar; na akitokea Zanzibar, makamu wake ni lazima atokee Bara.

  Ni vizuri ifafanuliwe kwamba utaratibu wa kuwa na mgombea mwenza wa kiti cha u-Rais, sio tu unahakikisha Watanzania wote wanajumuishwa katika kumchagua Mkuu wa nchi yao pamoja na makamu wake, bali pia unaondoa uwezekano wa Makamu wa Rais kuwa ni mteule Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, kwa vile Bunge la JMT halidhibiti mashughuli ya Baraza hilo.

  Aidha ieleweke kwamba katika mazingira ya vyama vingi vya siasa, inawezekana kabisa kwa chama cha siasa kinachoshinda ktk Uchaguzi wa Rais wa JMT, kisiwe kimeshinda pia na kupata u-Rais wa Zanzibar. Rais wa Zanzibar akiwa ni wa Chama kinachopingana kisiasa na kile kilichoshinda u-Rais wa JMT, haitawezekana yeye awe ni makamu wa Rais wa Mkuu wa nchi. Kwa utaratibu wa sasa, mgombea mwenza Mzanzibari wa chama kishindi atakuwa ni Makamu wa Rais licha ya kwamba chama chake hakitakuwa kimeshinda na kuchukua Serikali ya Zanzibar. Rais wa Zanzibar akiwa tu ni Waziri wa kawaida anayehudhuria vikao vya Cabinet ya JMT kama Katiba ya sasa inavyosisitiza, hakutakuwa na matatizo.

  Waumini wa demokrasia ya kweli wanaona kwamba mpangilio na utaratibu unaohakikisha kwamba sehemu ya Jamhuri ya Muungano ambayo jumla ya wakazi wake ni chini ya asilimia 5 ya Watanzania wote kuwa na uhakika (yaani Guarantee) ya kutoa Mkuu wa nchi au Makamu wake kila wakati, ni kujitolea tosha ili kuendeleza na kudumisha huo Muungano. Katika nchi ambazo ni muungano wa dhati, hakuna taratibu za kuhakikisha sehemu fulani inashiriki katika uongozi, isipokuwa kuna uhakika wa haki sawa kwa kila raia na uongozi unatokana na uwezo binafsi anaouonyesha mgombea. Matarajio yangu ni kwamba tutakapofikia lengo kuu la kuwa na Serikali moja ya JMTiliyochaguliwa bila kuwa na rushwa au ufisadi basi demokrasia ya kweli itakuwa imefikiwa.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Hivi ni marekebisho ya katiba au ni uandikwaji wa katiba mpya?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280

  Mzee hapo umenena! Sisi Watanganyika kwa kweli tumejitolea na kuwapa haki zetu zooote hawa jamaa zetu lakini hawaridhiki!! Leo nilikuwa naangalia protocal ya kuingia kwenye sherehe za muungano nikagundua kuna viongozi wakuu wengi sana ambao ni Wazanzibar na wanatambuliwa na JMT: Makomo wa Rais wa JMT, Rais wa Zanzibar, Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar wote hao wanatambuliwa na JMT kiplotocal. Leo kulikuwa na viongozi wakuu watano, bara tulikuwa na Rais Kikwete tu!!
   
 4. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  inashangaza sana kuona Mzanzibar anavyolalamikia muungano. wanafikiri itafika wakati watapewa kila kitu bure. ki ukweli bara ndiyo tunabeba mzigo wa wa Zanzibar na tunawavumilia sanaa kama ndugu zetu ila hawana shukran hata kidogo
   
 5. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Uandikwaji upya wa Katiba ambao Chadema tunaupigania hauimanishi kwamba hakutakuwa na ibara zitakazohusikana na mambo ambayo nimegusia ktk mada yangu. Kwa mfano ni lazima tuhusike na jinsi ya kuteua wagombea u-Rais na jinsi ya kuhakikisha Rais akitokea upande mmoja wa Jamhuri, Makamu wake atokee upande mwingine. Mambo haya yametajwa ktk Katiba ya sasa, kwa hiyo tukiyaandika upya yatakuwa ni maboresho.
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mzee. Mtei
  Mbona mnatuchanganya?
  Sera ya serikali tatu Tz, wewe hukubaliani nayo.Nijuavyo hii ndio sera ya Chadema au vipi?

  Sasa hili la matarajio la serikali moja vipi? Matarajio haya yalianza lini?

  CHADEMA wamezungumza serikali tatu, au ndio kamba za uchaguzi tu?Ahadi hewa kama za CCM?

  Halafu kwa nini jina Tanganyika mlilifuta au kuacha kulitumia?(hapa namaanisha ninyi wazee,sisi vijana bado tunaihitaji Tanganyika yetu na tunasema Tanganyika)
  Mimi sizungumzii serikali ya Tanganyika hapa...nazungumzia sehemu iliyoitwa Tanganyika.

  Ni wazi kama matarajio ya serikali moja yatatimia basi serikali ya Zanzibar itapotea au vipi?,je jina la sehemu inayoitwa Zanzibar itafutwa pia au itakuwepo sehemu inayoitwa Zanzibar?

  Natoa mfano wa UK kwa Muungano wao ndio wamepata UK au United Kingdom of Great Britain. Lakini kuna England ambayo haina serikali yake, Wales, Scotland na Northern Ireland...jina England ambalo tunaweza kulilinganisha na Tanganyika halikufa, halijaachwa kutumiwa wala kufutwa...sasa sisi tuliifuta serikali ya Tanganyika sawa ,lakini kulikuwa na ulazima kuliuwa jina la sehemu pia?

  Halafu hii Katiba ni Katiba ya Muungano au vipi? Muungano hauna wanachama, wabia?Kama wapo ni wepi?
  Sasa kama lengo ni kuboresha katiba,kiutaratibu sio wabia au wanachama wa Muungano ndio wanatakiwa ndio waiboreshe katiba hiyo?

  Mimi naona ninyi wanasiasa mnatuchanganya kwa "unafiki" wenu. Hamuelezi vitu in black and white.


  Mnatoa kauli,mnafanya mambo na maamuzi kama vile mna agenda za siri.
  Au ndio uzee tena?
   
 7. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katiba yoyote itakayoandikwa ni lazima ionyeshe wazi wazi Serikali ya Zanzibar na mbia wake Serikali ya Tanganyika. Serikali ya Muungano iundwe kwa kuzingatia sovereignty ya kila upande na hili ndilo litakalokuwa suluhisho pekee as far as Zanzibaris are concerned.

  Vyenginevyo, kila mmoja kivyake.

  Bahati nzuri Zanzibar ina Serikali yake, ni kazi ya Tanganyika kuifufua nchi yao wanayoipenda.

  Hakuna jambo zuri kama freedom and self determination.
   
Loading...