Marekani yaweka mtambo wa kulinda Korea Kusini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_94964051_mediaitem94964049.jpg

Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.

Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora, ambao hufahamika kitaalamu kama THAAD, kwa Kiingereza Terminal High Altitude Area Defense, kutokana na wasiwasi wa tishio kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imeendelea kufanyia majaribio makombora.

Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa an utakuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kumekuwepo na taarifa za kutokea kwa makabiliano kati ya wenyeji na polisi eneo panapojengwa mtambo huo, ambalo awali lilikuwa uwanja wa mchezo wa gofu.

Mtambo huo unajengwa katika wilaya ya Seongju

China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.

Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.

THAAD ni nini?
  • Ni teknolojia ya kujilinda ya kutungua makombora ya masafa mafupi na wastani ambayo huyaharibu yanapokaribia kulipuka.
  • Hugonga kombora la kuliharibu
  • Ina uwezo wa kufika umbali wa kilomita 200 na inaweza kurushwa juu hadi kilomita 150 angani
  • Marekani imewahi kuweka mitambo kama hiyo Guam na Hawaii kujilinda dhidi ya uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Chanzo: BBC
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Aje uswahilini tuna mitambo kila ukitaka kumdhuru mtu humuoni.Yani korea ya kusini ingepata ufundi huu kwisha kazi kwani kila Mr kiduku akitaka kuwalipua hawaoni.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Ni propaganda tu hizo fuatilia uwezo wa hiyo mitambo uone ilivyo dhaifu. Ndiyo maana wanasogeza meli za nyukilia ili walipize kisasi pindi miji yao itakapoangamizwa. Mwisho wa marekani umekaribia.
Bahati mbaya unaota mchana FSB fake... Habari za nguvu za taifa LA magharibi na maaduui zake hata hujawah kusoma... Utakufa utaiacha marekani ni superpower
 
Hawa America waoga sana ndio maana kila nchi wameweka base yao ili Iwe rahisi kupiga wenzao na ndio maana wanalazimisha marais na viongozi na demokrasia wanayotaka wao katika nchi zengine
 
Ni propaganda tu hizo fuatilia uwezo wa hiyo mitambo uone ilivyo dhaifu. Ndiyo maana wanasogeza meli za nyukilia ili walipize kisasi pindi miji yao itakapoangamizwa. Mwisho wa marekani umekaribia.
Ww ndio umesema ni dhaifu. America mpaka watumie kitu chao.. means wana uhakika nacho siku zote. America hatumii vitu weak.
THAAD nimeusoma.. uko vizuri... ww sema weakness yake ni against ICBM ... the same weakness ambayo russia wanayo.. japo wao wanadevelop ambayo inaweza ku take out ICBMs
 
Sasa South Korea wameshindwa kuelewana na North Korea wanadhani wataelewana na USA? Labda kama watakubali USA achukue chochote atakachokua anakitaka kutoka kwao vinginevyo wanatumika kama mtaji wa USA kumshambulia North Korea.
 
Endapo NK akirusha kombora la nyuklia hata likitunguliwa halitakuwa na madhara?
Yes.. makombora yanayotoka kwenye mfumo wa THAAD huwa yatoka kwa speed kali sana na kwenda kugonga kwa nguvu mno lile kombora liliyoka kwa adui. Hii inaweza kulisambaratisha kombora la adui likiwa juu.
 
Hii dunia sijui ipoje...
Kwa hiyo mmoja anatishia kumashambulia mwenzake... Mwingine anatuma kikosi... Baada ya hapo mmoja anasisitisha shambulio... Mwingine anakuja na story ya kutengeneza mtambo wa kujikinga kwanza...

Ni kama mchezo wa kitoto... Chora mstari... Vuka wewe.. Vuka wewe kwanza...


Cc: mahondaw
 
Bahati mbaya unaota mchana FSB fake... Habari za nguvu
Tatizo wewe na wenziyo wote wanaofanana na wewe humu mna "addiction" (usugu) ya umaarufu wa marekani na ikishindwa mko tayari kujiua! Fuatilia uwezo na udhaifu wa hiyo mitambo upate elimu badala ya kubaki na huo usugu ulio nao! Kwa uchache tu ukiacha matatizo ya kiufundi kama tu ambavyo gari au ndege hupata hitirafu; mitambo hiyo pia inaripotiwa kuwa haina uwezo wa kupambana na makombora mengi yanayokuja kwa pamoja na pia yale yanayoenda kwa super sonic speed. Kinachoendelea sasa ni psychological warfare na hili ndilo huelewi!Hivi hujiulizi meli na ndege za nyukilia wanazipeleka za nini?! Wanazipeleka ili kama watawamaliza(usa) na usa wawamalize North Korea ili ngoma iwe draw. Nyukilia moja tu kwa New York au Washington ni zaidi ya tsunami! Uchumi usiyumbe hapo?! Na ndiyo huo mwisho wa marekani kiuchumi.China inakuja kuchukua nafasi.
 
Back
Top Bottom