Mambo mengine bwana, tangu lini jamaa hawa wakasema ukweli? Pentagon wangekuwa wakali na weledi katika ulinzi wa nchi yao, mbona Osama alishambulia Jengo la Pentagon na kuharibu kabisa wing moja ya jengo hilo kwa kutumia vijana wa Kisaudia walio kuwa wanaendesha ndege za kubebea abiria - jeshi la Marekani pamoja na zana zao zote wanazo dai zina teknolojia ya hali ya juu kuliko za wenzao lilifanya jitihada gani kukabiriana na mashambulizi hayo yaliyo dumu kwa saa matatu na ushei??
Nchi yenye jeshi kubwa la anga na ndege za kivita lukuki hachilia mbali makombora chungu nzima ya kulinda anga la nchi yao, wanakwenda kuzidiwa kete na kikundi kidogo cha vijana wenye kufahamu weakness za Taifa lenye majigambo na dhalau, Bush alipo pata taarifa ya mashambulizi aliondoka mkuku kutoka shule ya chekechea akaenda kujificha kwenye mahandaki akiambatana na Chenny - woga kama nini sijui, yaani Commander In Chief wa the Only Superpower anakwenda kujichimbia aridhini wakati Majengo/Ofisi zenye unyeti wa pekee in the Land yakishambuliwa kila sehemu!!!
Kama abiria wasingejitoa muhanga kwa kukabiriana ana kwa ana na Waarabu mpaka ndege ikafikia hatua ya kahanguka kabla hajafika Ikulu ya Marekani ingekuwa aibu tupu, ujasiri wa abiria ndio ulinusuru White House hisishambuliwe - Sasa nyinyi mnao amini taarifa za Pentagon mbona hawakuwahi kutoa taarifa kuhusu idadi ya maafisa wa jeshi na raia waliopoteza maisha yao kwenye jengo la PENTAGON baada ya kumshambuliwa na magaidi - mpaka leo wako kimya kabisa, lakini idadi kamili ya Al Shabaab walio uwawa katika mashambulizi ya Drone idadi wanadai wanayo.