Marekani yatoa msaada wa silaha waaasi huko Syria

Marekani yatoa msaada wa silaha waaasi huko Syria

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
21,786
Reaction score
35,747
Juzi juzi tulisikia Russia akiwashambulia waasi wanaompinga assad bila kuwasahau ISIS!!! Leo asubuhi USA wamewapa silaha waasi je hii inamaanisha nini???

Jeshi la Marekani limetoa zaidi ya tani 45 za silaha kwa waasi wanaopambana na wanamgambo wa Islamic State (IS) kaskazini mashariki mwa Syria.


Jeshi hilo liliangusha shehena ya vifaa katika jimbo la Hassakeh, Msemaji wa wizara ya ulinzi wa Marekani ameeleza.

Shehena hizo zimeripotiwa kuhusisha silaha ndogo ndogo,kubwa na maguruneti.


Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya Marekani kuacha mpango wa gharama ya dola za marekani milioni mia tano wa kuwafundisha maelfu ya waasi kupambana na IS

Badala yake imeelezwa kuwa fedha hizo zitatumika kugharimia silaha ambazo zitakuwa zinahitajika kwa makamanda wa makundi ya waasi ambao wako katika maeneo ya mapambano.

CC Dotworld FaizaFoxy Bavaria RUCCI

Marekani yatoa silaha kwa waasi Syria - BBC Swahili
 
Last edited by a moderator:
Russia ianze kutungua hivyo vindege vya US vinavyotumika kuwapa waasi silaha.
 
Naunga mkono America. IS nao ni binadamu? Jamani iweni na haya!
 
Hii inamaanisha kuwa vita rasmi kati ya urusi na wamarekani (wazungu wanaita proxy war) imeanza.. Pia ni uwanja wa majaribio ya silaha mpya zinazoingia sokoni.. Marekani itawapa silaha waasi kuwaumiza zaidi warusi kama vile makombora ya kudungilia ndege na kubomoa vifaru.. Watawapa pia taarifa muhimu za movement za majeshi ya Syria na warusi (intel toka satellite na drones) etc.. Hapa tujiandae kwa mapigano ya mda mrefu especially now that wachina na wa iran wanasemekana kuingia kwenye theater
 
Jamaa wapuuzi sana kila sehemu wanataka kuvuruga amani iliyopo
 
Baada ya kushtukiwa kuwa IS ndio mmarekani,sasa wameanzisha group jingine linaitwa #FreeSyria hawa ndio chanzo cha kila vurugu Middle east na kwingine duniani
 
Angalau sasa tutaona Balance na wakitaka wapeleke wanjeshi
 
Hao wasiria ndio wapuuzi,wanakubali vipi kurubuniwa ili waiharibu nchi yao?
 
Back
Top Bottom