Marekani yalaani kufutwa kwa matokeo Zanzibar

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
21,246
34,196
Marekani imelaani hatua ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais pamoja na wajumbe wa bunge la wawakilishi visiwani humo.

Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa ubalozi huo nchini Tanzania, Marekani ilisema imeshtushwa na hatua hiyo na kutoa wito tume hiyo iondoe tamko hilo. Zec imeahidi kutangaza tarehe mpya ya marudio ya uchaguzi huo.

Katika kufutilia mbali matokeo ya urais wa Zanzibar, tume ya uchaguzi ya Zanzibar-ZEC ilisema shughuli nzima ya upigaji kura visiwani iligubikwa na kasoro nyingi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha amesema baadhi ya makamishna wa tume hiyo, badala ya kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa kikatiba "wamekuwa ni wawakilishi wa vyama vyao".
"Kumegundulika kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa baadhi ya vituo hasa Pemba vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura wa kituo husika."

Amesema hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba "baadhi ya wapiga kura hawakwenda kuchukua vitambulisho vyao vya kupigia kura". Kadhalika, amesema kura hazikupata ulinzi mzuri hususan kisiwani Pemba ambako amesema kuwa baadhi ya mawakala wa baadhi ya vya vyama vya siasa katika kisiwa hicho walifukuzwa.

Hata hivyo, taarifa ya ubalozi wa Marekani inasema kufutilia mbali matokeo hayo kunasitisha mchakato wa uchaguzi uliofanyika vizuri na kwa amani.

Aidha Taarifa hiyo inasema kuwa hatua hiyo ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar inakwenda kinyume kabisa na tathmini ya waangalizi wa uchaguzi kutoka ubalozi wa Marekani, jumuiya ya ulaya, jumuiya ya madola na jumui ya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki.

Marekani yasikitishwa na tamko la ZEC kufuta uchaguzi Z?€™bar - Uchaguzi Tanzania | Mwananchi

Marekani yalaani kufutwa kwa matokeo Zanzibar - BBC Swahili
 
Ngoja tupate viongozi waliongia kwa wizi wa kura alafu wadai eti wanashughulikia ufisadi!
 
nimegundua cdm na cuf wana differ...
cuf hawataki yafutwe sababu uchaguzi ulikuwa ok...ila matokeo sivyo...
cdm kama wamefuraia ufutwe vile??!! maybe watafaidika uchaguzi ukirudiwa...though sijui how?
 
nimegundua cdm na cuf wana differ...
cuf hawataki yafutwe sababu uchaguzi ulikuwa ok...ila matokeo sivyo...
cdm kama wamefuraia ufutwe vile??!! maybe watafaidika uchaguzi ukirudiwa...though sijui how?

mkuu hii ni kauli ya USA sijaelewa unataka kumaanisha nini hapa!!
 
Mambo ya Tanzania watuachie Watanzania wenyewe

Kweli kabisa mkuu kitu cha kwanza ni kuomba serikali yetu tukufu chini ya mh JPM kukataa kabisa misaada yao na hata wakitubembeleza tugome kabisa ikiwezekana tususie ziara zote za Amerika hadi wakome
 
Kweli kabisa mkuu kitu cha kwanza ni kuomba serikali yetu tukufu chini ya mh JPM kukataa kabisa misaada yao na hata wakitubembeleza tugome kabisa ikiwezekana tususie ziara zote za Amerika hadi wakome

Acha kuota, amka jua lisha chomoza!!
 
Kweli kabisa mkuu kitu cha kwanza ni kuomba serikali yetu tukufu chini ya mh JPM kukataa kabisa misaada yao na hata wakitubembeleza tugome kabisa ikiwezekana tususie ziara zote za Amerika hadi wakome
Kama mpaka mapumb.u na busha rais wenu anaenda kutibiwa kwao wewe kapuku mjinga usiejielewa unapata wapi jeuri ya kuwanunia hao jamaa. vingine shirikisha ubongo kabla ya kuandika pumba na uharo wa namna hii
 
Nadhani hujamuelewa huyu jamaa. Hii ilikuwa ni reply kwa mpuuzi aliyetaka watuachie Tanzania yetu wenyewe huku akujisahaulisha bakuli tunalotembeza huko mbele
 
Back
Top Bottom