Marekani yaiondoa Sudan katika orodha ya wafadhili wa ugaidi

Marekani yaiondoa Sudan katika orodha ya wafadhili wa ugaidi

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842

Shambulio la kigaidi
​


Marekani imeiondoa rasmi Sudana katika orodha ya wafadhili waugaidi, kwa mujibu wa ubalozi wake mjini Khartoum.

"Muda wa ilani ya siku 45 iliyowasilishwa kwa bunge la Congress umepita na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ametia saini arifa ya kuiondoa Sudan katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi kuanzia leo (Desemba 14), ambayo itachapishwa katika sajili ya serikali," Ubalozi wa Marekani umeandika katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Rais wa Marekani Donald Trump mnamo mwezi Oktoba alisema kwamba Sudan itaondolewa katika orodha hiyo baada ya kulipa fidia ya $335m kwa waathiriwa na familia ya shambulio la bomu la al-Qaeda mwaka 1998 dhidi ya ubalozi wa Marekani Afrika.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok alijibu kwa kusema fedha hizo zimetumwa.
Sudan iliorodheshwa mwaka1993 wakati kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden alipoishi nchini humo kama mgeni wa serikali. Nchini zingine zilizojumuishwa katika orodha ya kufadhili ugaidi ni Iran, Korea Kaskazini na Syria.
 
Hiyo fidia watalipwa raia wa USA tu waliokuwa kwenye hizo balozi wakati wa shambulio au mpaka raia wa Kenya na Tz walioathirika na hayo mashambulizi wakati wakiwa kwenye hizo balozi?
 
Hiyo fidia watalipwa raia wa USA tu waliokuwa kwenye hizo balozi wakati wa shambulio au mpaka raia wa Kenya na Tz walioathirika na hayo mashambulizi wakati wakiwa kwenye hizo balozi?
Pesa iko US, wengine mtakufa kivyenu
 
Hiyo fidia watalipwa raia wa USA tu waliokuwa kwenye hizo balozi wakati wa shambulio au mpaka raia wa Kenya na Tz walioathirika na hayo mashambulizi wakati wakiwa kwenye hizo balozi?
... hoja ya ajabu kabisa! Fedha azihangaikie Marekani; zimetoka; mnadai na ninyi mlipwe! Mnakuwa kama TRA? Wanavuna wasipopanda; wanachukua hadi mitaji ya watu.
 
Wanaounga mkono ugaidi ndio wajue kwamba ugaidi haulipi, sasa ona hiyo hela ndefu imewatoka huku wananchi wa Sudan wakibaki kuchoma mahindi. Bure kabisa.
 
Ukiwa super power Raha Sana. Yaani unaamua tu Nani aonekane shetani na Nani aonekane malaika
 
Back
Top Bottom