Marekani yailaumu Korea kaskazini kwa kusambaza virus cha computer kinacho igharimu dunia

Drax001

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
439
221
Utawala nchini Marekani unasema kuwa Korea Kaskazini ilihusika moja kwa moja na kirusi cha wannaCry kilichoadhiri hospitali, biashara na mabenki kote duniani mapema mwaka huu.
Kirusi hicho kilidaiwa kuvamia zaidi ya kampuni 300,000 kwenye mataifa 150 na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola.

Thomas Bossert ambaye ni msadizi wa Rais Donald Trump, aliyasema haya kupitia jarida la Wall Street Journal.
Hii ndiyo mara ya kwanza Marekani imeilaumu Korea Kaskazimni kwa kirusi hicho.
Bw. Bossert anayemshauri Trump katika masuala ya usalama wa ndani wa nchi alisema kuwa madai hayo ni kutokana na ushahidi uliopo.

Serikali ya Uingereza na kampuni ya kompiuta ya Microsof waliilaumu Korea Kaskazini kwa kirusi hicho.
Mwezi Mei kompiuta zinazotumia Windows zilivamiwa na kirusi hicho na kufungwa ambapo watumiaji walitakiwa kulipa ili kuweza kupata data zao.
 
Maalim shewedy North ni watu hatari sana ndio maana marekani hataki kuwaona ila ndio hivyo amesha chelewa north amesha kwea pipa na kuondoka!!
uzuri ni kuwa NK. hawatumii Windows wantumia Os yao ya Star OS. so inakuwa vigumu kwa USA kumuatack maana yupo vizur na kajiandaa muda mrefu sana!! Usa aatabaki kulalamika tuu pamoja na SK
 
Huyu jamaa kaisha anza vita mda mrreeffuu sanaa
uzuri NK anatumia teknolojia yake hivyo kupambana naye ni kazi sana maana akishambulia Window Os ina maana dunia nzima inaathirika ndo maana anatumia Os yake peke yaake hivyo inabidi adui ajipange kwa makini
 
Doooh watu wanalipa kodi NK bila kupenda
hahahaha wakisema wavilete na huku hivyo virusi pale kwa baba naniliii sijui watakula nini maana wanategemea ka window kao waki kadukua wakakoma kulinga maana sahivi mtaani kwetu hatulali kero mtindo mmoja
 
Back
Top Bottom