Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Idara ya forodha na uhamiaji ya Marekani(ICE), imezindua ukaguzi wa kushtukiza unaowalenga wahamiaji 2,000 wasio na vibali nchini humo.
Kwa mujibu wa Rais wa nchi hiyo Donald Trump, mpango huo wa kuzikamata familia za wahamiaji hao ni operesheni kubwa itakayofanyika katika miji mikubwa kadhaa ikiwemo Los Angeles, New York, Chicago na Houston. Hata hivyo maafisa katika miji inapolengwa kufanyika operesheni hiyo wamekataa kutoa ushirikiano.
Meya wa New York Bill de Blasio ameandika kupitia mtandao wa Tweeter akisema operesheni hiyo haiendi kama ilivyopangwa na ikulu ya Marekani.
Trump amewahi kunukuliwa mara kadhaa akizitaka mamlaka husika kuchukua hatua zaidi dhidi ya wahamiaji haramu na kuipa kipaumbele hatua hiyo, kuelekea katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.