Marekani waandamana kupinga matumizi holela ya silaha

Marekani waandamana kupinga matumizi holela ya silaha

Nondoh

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Posts
298
Reaction score
478
Leo yamefanyika maandamano makubwa nchini Marekani yakiongozwa na vijana wadogo kupinga matumizi ya holela ya silaha huku wakitaka sheria kali ziwekwe juu ya umiliki holela wa silaha.

Ikumbukwe kuwa moja ya sera za rais wa Marekani Donald Trump ni kupambana kuhakikisha sheria ya sasa ya umiliki wa silaha haibadilishwi na hili lilikuwa miongoni agenda yake kipindi cha kampeni ya urais. Na kwa kudhihirisha hili muda wa maandamano ametumia kwenda kucheza gofu.

Rais wa zamani wa Marekani yeye ametumia mtandao wa tweeter kupongeza vijana huku akiwasihi kelele peke yake bila vitendo hazina maana hata wangepiga zaidi ya mara milioni
Screenshot_20180325-013643.jpg
IMG_20180325_013629.jpg
 
Mamilioni wameandamana katika maandamano ya amani. Manjagu yalikuwepo lakini hayakuua mtu, kumtia mtu kilema, kumpiga mtama au hata kufyatua bomu la machozi. Walichokifanya ni kuhakikisha tu usalama wa walioandamana.

Kiongozi wa malaika akiiona hii picha presha itapanda.
 
Kwetu watu wakiandamana kuitaka tume itende haki bunduki za kivita zinaelekezwa hadi kwenye mabasi ya abiria, na marais wetu wastaafu wameufyata tu!
 
Nyani Monkey yeye yupo misitu ya idodomya anapasha viungo kwaajiri ya Muungano wa Tanzania
 
Kwani kwenye nchi ya dictator uchwara haya yanaruhusiwa?.

Pressure inapanda, frustrations zinaongezeka
 
Rais wa zamani wa Marekani yeye ametumia mtandao wa tweeter kupongeza vijana huku akiwasihi kelele peke yake bila vitendo hazina maana hata wangepiga zaidi ya mara milioni

Ikumbukwe kuwa moja ya sera za rais wa Marekani Donald Trump ni kupambana kuhakikisha sheria ya sasa ya umiliki wa silaha haibadilishwi na hili lilikuwa miongoni agenda yake kipindi cha kampeni ya urais. Na kwa kudhihirisha hili muda wa maandamano ametumia kwenda kucheza gofu.
 
"Waambieni waandamane watakwenda kuwasimulia hao waliowatuma "[emoji26][emoji26]
 
Vipi hakuna risasi ya polisi hapo iliyo kata kona hewani na kwenda kutua moja kwa moja kwenye nyama ya muandamaji
 
Naona hii tafsir yako mstari wa mwisho kama sio hivi au mimi ndio sijui kiikristo.... lol
 
hivi hizo sheria wakati wa obama hakuona umuhimu wa kuzibadilisha? au hazikuwepo? au ndio unafiki wenyewe
 
Back
Top Bottom