Marekani kuziwekea vikwazo Urusi, Iran na Korea Kaskazini

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
_97080741_63298142-86d2-4ece-bd94-ad8bf88a6a92.jpg
​

Baraza la wawakilishi la Marekani limepiga kura kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini.

Urusi inaadhibiwa kutokana na kudaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa Marekani huku Korea Kaskazini na Iran wao wakiadhibiwa kufuatia majaribio ya makombora.

Muswada huo unatarajiwa kupitia kwa baraza la seneti kabla ya kupelekwa kwa Rais Trump ili audhinishe na kuwa sheria kamili.

_97080744_45e19fa6-5ce5-48a2-a1a9-db278086b58c.jpg
​

Akizungumza katika baraza hilo wawakilishi David Ciciline kutoka chama Democratic amesema hatua kamili zinahitajika kuiwajibisha Urusi.

Amesema hawawezi kuruhusu dola nyingine kuingilia uchaguzi wao japokuwa Rais wao anapinga kuihusisha Urusi na uchaguzi uliopita.

Naye Ted Poe kutoka chama cha Republican amesisitiza kuwa muswada unaihusisha Korea kaskazini pia.

_97080746_4cd2172a-885f-437a-a5f4-838c4a850ceb.jpg
​

Mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya kimataifa ya bunge la Urusi Duma , Leonid Slutsky amesema hatua hizo mpya zitazorotesha uhusiano baina ya Urusi na Marekani.

Chanzo: BBC Swahili
 
Marekani anawawekea vikwazo korea na iran kama nani
 
Hahaaaa! Huyu jamaa anarukaruka tu N korea tangu nazaliwa nimekuta ana vikwazo tayari mpaka leo hii wanadunda Iran taangu namaliza shule miaka 1979 baada ya mapinduzi ya SHAH ikawekewa vikwazo mpaka leo hii RUSSIA huyu ni mbabe mwenzie kila akiwekewa vikwazo lazima maumivu wayasikilizie ULAYA na washirika wao mimi naona vikwazo kwa nchi kama hizo ni kupoteza muda tu haswa kwa Kiduku alishakubuhu
 
Hakuna nchi duniani inayoweza kustahimili vikwazo. Angalia Russia inavyolalamikia vikwazo na hiyo ndiyo chanzo cha wao kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Kitendo cha Wairan kushangilia usiku kucha pale walipoondolewa vikwazo na Marekani, ni uthibitisho tosha wa jinsi gani haya mataifa yanavyoumia pale yanapowekewa vikwazo.

Mbinyo wa vikwazo ndo chanzo cha umasikini wa Korea Kz, kama isingekuwa vikwazo, nchi hii ingekuwa ngoma droo na mwenzake wa kusini, au hata kuizidi.

Hivyo kusema eti vikwazo havitikisi haya mataifa ni uongo uliyofuzu. Hakuna nchi inafurahia vikwazo. Haya mataifa bila vikwazo yangekuwa mbali sana.
 
Kuna nchi kama n korea vikwazo kwake ni sawa na samaki kumtoa majini halafu unamtupia majini vikwazo vimedumu kwa zaidi ya miongo sita lakini ulishawahi kusikia wanalia njaa au maradhi sisi huku pamoja na kujitawala kote lakini bado tunaishi kwenye lindi la umasikini ujinga na maradhi yaliyotopea
 
Marekani wanahangaika mno hapa duniani...

Hivi nani anafanya biashara na marekani bado,kila kitu ni china sikuhizi,
ufalme wa marekani siku zake zinahesabika,
uchumi umekufa,unapumlia mashine ili hawaishi kukuruka waonekane bado wamo,
 
Hakuna nchi duniani inayoweza kustahimili vikwazo. Angalia Russia inavyolalamikia vikwazo na hiyo ndiyo chanzo cha wao kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Kitendo cha Wairan kushangilia usiku kucha pale walipoondolewa vikwazo na Marekani, ni uthibitisho tosha wa jinsi gani haya mataifa yanavyoumia pale yanapowekewa vikwazo.

Mbinyo wa vikwazo ndo chanzo cha umasikini wa Korea Kz, kama isingekuwa vikwazo, nchi hii ingekuwa ngoma droo na mwenzake wa kusini, au hata kuizidi.

Hivyo kusema eti vikwazo havitikisi haya mataifa ni uongo uliyofuzu. Hakuna nchi inafurahia vikwazo. Haya mataifa bila vikwazo yangekuwa mbali sana.

North Korea mwaka zaidi ya 20 huu wanawekewaga vikwazo tu hadi sasa hivi wameshakuwa manunda.

Russia wanalalamika vikwazo wakati huo huo hao Marekeni wanaenda kununua Engine za roketi kwao
Wakati huo huo Ulaya wanatumia gas ya Urusi
Wakati huo huo Ulaya wanatumia sehemu ya mafuta ya Urusi na bidhaa nyingi.

Ukitaka uone jinsi vikwazo vilivyo na athari tuwekewe sisi huku ambao hatuna tunaloliweza, hapo ndo tutaomba poo, ila Russia umuwekee vikwazo vya maana sidhani kama EU watamuunga mkono huyo Marekani.
 
Marekani wanahangaika mno hapa duniani...

Hivi nani anafanya biashara na marekani bado,kila kitu ni china sikuhizi,
ufalme wa marekani siku zake zinahesabika,
uchumi umekufa,unapumlia mashine ili hawaishi kukuruka waonekane bado wamo,
Kwanini Urusi analalama sasa na kuomba poo kwa Trump?
 
Marekani wanahangaika mno hapa duniani...

Hivi nani anafanya biashara na marekani bado,kila kitu ni china sikuhizi,
ufalme wa marekani siku zake zinahesabika,
uchumi umekufa,unapumlia mashine ili hawaishi kukuruka waonekane bado wamo,
Umetafakari kwa makini lakini kabla ya kuja na hii comment?. Hebu tueleze China ina technologia gani kubwa ambayo inaipa sifa ya kuipokonya marekani utawala wa biashara duniani? Nadhani, japo inawezekana China bado ana safari ya miongo au hata karne kadhaa kuweza kusimama height moja na US.

Zamani kabla yetu yalikuwepo mataifa yaliyoitiisha dunia kila idara. Ilikuwepo babeli, uyunani na rumi. Kwa wakati wetu mbabe wetu ni US hakuna wa kumtunishia misuli. US kwa sasa hivi ndo nchi yenye uchumi mkubwa na tech kubwa duniani. China pamoja na population kubwa kuliko US bado bajeti take inachechemea kwa US.

Tusubiri huko mbeleni tutaona kama China ataweza kukuza tech yake pamoja na uchumi wake vya kutosha ndo tuanze kumjadili kama next super power. And I bet huenda asiibuke mwingine zaidi ya U.S.
 
marekani ya miaka 10 iliyopita,sio marekani ya leo,
last time nilicheki mchina alikuwa ana mu overtake kiuchumi,
kwa mfano china ndo nchi inayoongoza kwa kuwa na foreign reserve kuzidi nchi yeyote,
china ina dolar trilion 3 hazina,
sasa imagine hata marekani wanaozichapa hizo dola hawanazo za kuizidi,we hushangai kwanini china anaweza kutoa mkopo hadi dola bilioni 50 kwa mkupuo mmoja,wakati record ya marekani hajawahi kuvuka dola bilion 5 kutoa iwe msaada ama mkopo,

sina data kwa sasa ila mchina anamu overtake mmarekani kwa speed kali mno,
saa hizi china anafungua silk roads,
yaani train inaweza toka china mpaka pakstani na ikatoka china mpaka india,russia,middle east etc
 
Mbona sasa kila siku Urusi anahangaika akiomba aondolewe vikwazo?!
Marekani itaanguka ila sio leo wala kesho utakufa utaiacha ikiwa na nguvu hivhiv, China yenyewe ukuaji wa uchumi ushaanza kushuka, bado ana migogoro na majirani zake India, Vietnam, nk.
 
China hii hii inayotegemea export kwa kiasi kikubwa kuendesha uchumi wake ndo impiku Marekani?!. Hapo nyuma kuna India soon viwanda vingi vitahamia huko kwa sababu ya cheap labor na hapo China ndo atakua hana chake tena.
China leo hii mpaka injini ya ndege mpaka amtegemee mrusi ndo useme ina teknolojia, imenunua Su-35 za mrusi wapate injini zake wazimodify wazichomeke kwenye ndege zao mpya za J-20 na J-31.China kwa Marekani bado sanaaaaa.
 
jirani yako anapokuwekea uzio hakuna kuingia kwake kiungwana ni lazima ulalamike tu ila haina maana kua huwezi kuishi bila yeye,vipi kuhusu EU wamesema nn kuhusu hivi vikwazo. EU wamengua ujinga wa US
 
China hii hii inayotegemea export kwa kiasi kikubwa kuendesha uchumi wake ndo impiku Marekani?!. Hapo nyuma kuna India soon viwanda vingi vitahamia huko kwa sababu ya cheap labor na hapo China ndo atakua hana chake tena.
China leo hii mpaka injini ya ndege mpaka amtegemee mrusi ndo useme ina teknolojia, imenunua Su-35 za mrusi wapate injini zake wazimodify wazichomeke kwenye ndege zao mpya za J-20 na J-31.China kwa Marekani bado sanaaaaa.
Mkuu umeelewa point ya Elungata lakini..?Source za kiuchumi kati ya US na China zinasemaje..?maana naona ww umetoa mawazo yako binafsi kabisa,unawaza silaha za kivita tu
 
Marekani wanahangaika mno hapa duniani...

Hivi nani anafanya biashara na marekani bado,kila kitu ni china sikuhizi,
ufalme wa marekani siku zake zinahesabika,
uchumi umekufa,unapumlia mashine ili hawaishi kukuruka waonekane bado wamo,
Unaposema Marekani siku zake zinaesabika inadhihirisha ulivyo na upeo finyu juu ya huyo Matekani,pia unaposema kila kitu ni china,unadhani kwa kuwa unaona bidhaa za kichina huku ndo unadhani anauza sana? Umebugi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna nchi duniani inayoweza kustahimili vikwazo. Angalia Russia inavyolalamikia vikwazo na hiyo ndiyo chanzo cha wao kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Kitendo cha Wairan kushangilia usiku kucha pale walipoondolewa vikwazo na Marekani, ni uthibitisho tosha wa jinsi gani haya mataifa yanavyoumia pale yanapowekewa vikwazo.

Mbinyo wa vikwazo ndo chanzo cha umasikini wa Korea Kz, kama isingekuwa vikwazo, nchi hii ingekuwa ngoma droo na mwenzake wa kusini, au hata kuizidi.

Hivyo kusema eti vikwazo havitikisi haya mataifa ni uongo uliyofuzu. Hakuna nchi inafurahia vikwazo. Haya mataifa bila vikwazo yangekuwa mbali sana.
Oke turud hapo Korea kaskazin mm tangu mdogo hyo nchi iliwekewa vikwazo lakin mpaka leo wananchi wake wanakula wanaishi wanasoma na mpaka leo wana technolojia za kutisha mpaka Marekan anashangaa wamewezaje..ko kwingine labda ila Kwa kiduku mmarekan anapoteza muda na kuchosha mdomo kuongea
.
.
.
kyenekyaka nkighanile une

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna nchi duniani inayoweza kustahimili vikwazo. Angalia Russia inavyolalamikia vikwazo na hiyo ndiyo chanzo cha wao kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Kitendo cha Wairan kushangilia usiku kucha pale walipoondolewa vikwazo na Marekani, ni uthibitisho tosha wa jinsi gani haya mataifa yanavyoumia pale yanapowekewa vikwazo.

Mbinyo wa vikwazo ndo chanzo cha umasikini wa Korea Kz, kama isingekuwa vikwazo, nchi hii ingekuwa ngoma droo na mwenzake wa kusini, au hata kuizidi.

Hivyo kusema eti vikwazo havitikisi haya mataifa ni uongo uliyofuzu. Hakuna nchi inafurahia vikwazo. Haya mataifa bila vikwazo yangekuwa mbali sana.
inategemea na utegemezi wa nchi mfano urusi soko lake kubwa ni ulaya,ulaya inamuhitaji zaidi urusi kuliko yeye anavyowahitaji-kwa sababu ana abundunt resources kuliko nchi nyingi za ulaya ndio maana vikwazo kwake havina effect sana.Ukija kwa irani vikwazo sawa na kutwanga maji kwenye kinu sababu ni moja ya nchi inazalisha mafuta mengi duniani na bidhaa kama mafuta ni uatake usitake lazima utanunua.
Kuhusu kora kasikazini hizi habari kuwa ni masikini huwa siziamini kutokana na unyeti wa Taifa lenyewe hizo takwimu walipata wapi?? na nchi masikini inawezaje kuwa na satellite yake mwenyewe kitu ambacho kuna nchi karibu zate za ulaya hazijaweza
 
Back
Top Bottom