Marekani Kutuma Ndege za Nyukilia Korea Kusini

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,856
ImageUploadedByJamiiForums1455639355.521385.jpg

Marekani itatuma ndege zake za kivita aina ya F-22 stealth kuelekea nchini Korea ya Kusini ambazo zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia ili kuonyesha nguvu zake za kijeshi kwa serikali ya Korea ya Kaskazini , shirika la habari la Yonhap lilisema.

Ndege za F-22 stealth zina uwezo wa kuepuka kugunduliwa na rada, na pia uwezo wa kubeba makombora ya nyuklia na mabomu.
 
Sasa mkuu hizi silaha za nyuklia lazima ziwe chini ya mtu makini, wewe mtu akinyoa tu style kama ya rais ni kosa kubwa!!!?? Hiyo si hatari.
Haha asingekua Makini Mkuu korea kusini ingeshakua majivu siku nyingi
 
Halafu wanamgombeza akifanya majaribio ya kurusha makombora yanayoweza kufika marekani wakati wao wachokozi.
Kinachoshangaza sio makombora tu hadi jamaa kupeleka satellite kwenye orbit wanapiga kelele wakati wao walipeleka miaka karibia sitini iliyopita
 
Sasa mkuu hizi silaha za nyuklia lazima ziwe chini ya mtu makini, wewe mtu akinyoa tu style kama ya rais ni kosa kubwa!!!?? Hiyo si hatari.

Kama angekuwa makini kwa nini alitumia hizo Nuclear kule Japan wakati wa WW II?
 
Ukijiuliza sana haya mambo ya "Kwanini iwe halali kwa huyu na Haramu kwa yule" unaweza ukajikuta una "wehuka" hivi hivi!
Ni kweli mkuu ,hakuna mwanadamu anayependa kumtendea mwenzake kama anavyo tendewa yeye na kama wapo basi ni wachache sana ,(GOLDEN RULE )
 
Huyo dogo wa Korea Kaskazini anahitaji kuthibitiwa, ana kichaa na itakua hatari akimiliki mabomu ya nyuklia. Apigwe mapema mwehu tu, utaamrisha vipi eti raia wote lazima wanyoe mtindo wako kichwani halafu uruhusiwe kumiliki vifaa vya maafa makubwa.
 
Anamchokonoa Korea kaskazini Akita vita sababu ameona vikwazo havimtishi Kim Hong un na hana mpango wa kuacha uundaji wa silaha za nyuklia
 
Huyo dogo wa Korea Kaskazini anahitaji kuthibitiwa, ana kichaa na itakua hatari akimiliki mabomu ya nyuklia. Apigwe mapema mwehu tu, utaamrisha vipi eti raia wote lazima wanyoe mtindo wako kichwani halafu uruhusiwe kumiliki vifaa vya maafa makubwa.

Unaposema adhibitiwe kabla hajamiliki bomu la nyukilia Una maana gani? Kwa kuwa jamaa tayari anamiliki na ndiyo maana marekani anarukaruka Tu hamgusi
 
Back
Top Bottom