Marekani kuondoa wanajeshi wake Syria

Ila Trump hii sera yake ya America first Sasa inapoendea sio pazuri,unaondokaje Syria wakati una Urusi,una Iran una Hezbollah wamejizatiti na bado wanaendelea kujichimbia mizizi kule(Syria). INAHUZUNISHA!!!
Mkuu mbona USA yupo syria illegal? Russia yupo Miaka na miaka
 
sidhani Trump ni sawa na jiwe naamini anavyombo vya intelijensia vinamshauri hivyo nadhabi hili swala lilioangwa mda mrefu na sasa ndio wakati wa utekelezaji wake
 
hii naona kama ni moto wa putin ndo unawatoa huko. Yaani kweli dunia inadanganywa. IS hiyo hiyo ndo inasapotiwa na USA, sasa eti wamewatoa. Na utaingiaje kwenye nchi ya mtu kupigana na watu ambao hawakuhusu? haya mapicha picha baadaye kitaeleweka tu.
 
Mmmh,US wanaondoka tu bila kuwa na Alternative plan?..Sidhani
 
sioni kama ni busara kuanza kuingiza haya masuala na uhasama.Wanajeshi wanafamilia zao marekani sasa kama IS hawapo warudi nyumbani tu.Halafu kitendo cha kuiingiza urusi pia ni upuuzi tu maana hakuna kitu kama hicho maana sion kwamba ni msingi upi unaotumia russia kumtisha US.Hayo ni maamuzi tu ya Trump basi.Na IS wakipewa nguvu basi majeshi yatarudi.
 
Tujali maisha ya ndugu zetu syria.Wamechoka na vita miaka 8.Ninyi mnaangalia matimu US,mara Urusi afu manasahau maisha ya raia wasio na hatia wa Syria.Mtu yeyote mwenye ubinadamu lazima asupport alichofanya Trumpa maana hata wakibaki bado Syria itaendelea kuwepo na choko zilizokuwepo hazipo.Mission complete.Warudi makwao.
Kwa mfano Baada ya M23 kumalizwq mbona wanajeshi wetu waliondolewa congo?saiz wamebaki wachache tu.
Tuwaache wasyria wajenge nchi yao.
 
Mattis anasepa
Sijajua kina Bolton na Haspel
 
SAFI SANA PUTIN KUISAMBARATISHA MAREKANI NA ULAYA [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapa nahisi kuna mchezo unachezwa.
Wasiojua Analysis ya haya mambo tayari wameshaanza kupuliza matarumbeta kushangilia. Kwenye haya mambo ni heri hawa jamaa wangeendelea kuwepo kuliko wakiondoka. Binafsi nahisi hivi sasa hali itakuwa mbaya zaidi. Syria huenda ikatawakiwa na mabwana wa kivita kama ilivyo Somalia. Muda wote wa zile harakati nahisi ndiyo Syria ilikua inamegwa kwa kuwaandaa hawa mabwana wa Kivita ili ikifika wakati muafaka wakabidhiwe vitendea kazi na kupewa maeneo ya kutawala.
Ngoja tuone yajayo.
 
Mkuu kwa nn unataka waendelee kuwepo?? Huoni kama watazidi kuuwa watu wasiokuwa na hatia ??
 
Nakubaliana na wewe
Kiboko ya erdogan ni Trump kwa sababu wote hao ni watu wa kakurupuka[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…