Marekani kufanya mashambulio ya ndege Somalia

Marekani kufanya mashambulio ya ndege Somalia

Mwanakili90

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,568
Reaction score
246
Marekani imeanza kufanyia majaribio ndege zake
za kivita zisizo na rubani nchini Ethiopia katika
maandalizi ya kuanza mashambulio dhidi ya
ngome za wapiganaji wa Al Shabaab katika nchi
jirani ya Somalia. Ndege hizo ambazo zinaweza kubeba
makombora na mabomu yanayoelekezwa kwa
kutumia mtambo wa satelite zitaruka kutoka
kituo cha jeshi la Marekani katika mji wa kusini
mwa Ethiopia wa Arba Minch. Marekani hata hivyo imeihakikishia serikali ya
Ethiopia kwamba ndege hizo hazina silaha kwa
hivi sasa na zinatumika tu kuchunguza hali ya
usalama. Marekani imekuwa ikitumia ndege hizi nchini
Djibouti ambako majeshi yake yana ngome yake
ya kudumu ya kipekee barani Afrika.

Source:BBC
 
Hawa wamarekani hawachoki vita?? Wao kila siku ni mipango ya kushambulia tu!!
 
Mimi si support nguvu za kijeshi zinazotumiwa na marekani lakini kwa hili nawaunga mkono asilimia 100. Al Shabaab wamwkua tishio kwa amani na uchumi wa bara la Africa ikiwemo Tanzania. Aluta continua!!!!!!
 
Kwaajili ya amani ya na maendeleo ya Somalia, Afrika na Dunia nzima, ni lazima Dunia nzima, watu wote tushirikiane kuumaliza ushenzi wa Al-Shabab. Wasomalia ni binadamu wanaotakiwa kuishi kwa furaha, amani, upendo na kuifurahia Dunia waliyopewa na Mungu lakini Al-Shabab wameondoa matumaini yote. Mimi nawalaumu Marekani, mataifa yote makubwa Duniani pamoja na AU kwa kutokushiriki kikamilifu katika jitihada za kuwaangamiza Al-Shabab. Hata kama kungekuwa na sumu au vijimelea vinavyoweza kuwaangamiza Al-Shabab pekee, mimi ningeunga mkono.
 
It is good sometimes to help your relatives by blood.
 
Mimi si support nguvu za kijeshi zinazotumiwa na marekani lakini kwa hili nawaunga mkono asilimia 100. Al Shabaab wamwkua tishio kwa amani na uchumi wa bara la Africa ikiwemo Tanzania. Aluta continua!!!!!!

Inaonekana huwaelewi wamarekani, mlimbwende.

Utawaelewa karibuni mabomu yatakapodondoshwa Dar, Arusha.
Hawa US ndio wafadhili wa vikundi vya ugaidi.

Google utapata habazi za CIA na mikakati ya kuitawala dunia. Soma habari za AFRICOM na vipi US wamepanga kuzifurusha kutoka Afrika nchi za China na India.

BBC News - US flies drones from Ethiopia to fight Somali militants
 
obama anajitahidi kumaliza tatizo la 'ugaidi' dunia nzima..kama foreign policy yake muhimu. baada ya kushindwa kwa strategy ya Bill Clinto Somalia miaka ile, Obama ameamua kupambana kwa remote control...kuwatumia wakenya na kutumia ndege zisizo na askari...lengo ni kupunguza majeruhi kwa wamarekani lkn kuondoa kero zote za magaidi...kuhusu somalia naunga hoja...al-shabbab ni tishio sana kwenye pwani yetu ya E.A. tayari bidhaa zinapanda kwa ajili ya uharamia kwenye coastaline yetu...kisa al-shabbab. wapigwe wateketee, turejee kwenye smooth sea transportation maeneo haya
 
Back
Top Bottom