Corticopontine
JF-Expert Member
- Sep 20, 2019
- 665
- 1,277
Marekani yaikataza IMF kutoa mkopo kwa Iran kukabiliana na COVID-19
Marekani imelizuia Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kutoa mkopo wa dharura wa dola bilioni 5 za kimarekani kwa Iran, kutokana na kile ilichosema kuwa Iran itatumia pesa hizo katika shughuli za kijeshi badala ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Akizungumzia suala hilo, rais Hassan Rouhani wa Iran amesema kitendo hicho si haki wala haikubaliki, na ni kitendo cha ubaguzi dhidi ya Iran. Kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika jana, rais Rouhani alisema ikiwa nchi mwanachama wa IMF, Iran inalipa ada yake, na haijawahi kutoa ombi lolote kwa shirika hilo katika miaka 50 iliyopita.
Tarehe 4 mwezi uliopita, IMF ilisema itatoa mkopo wa dola bilioni 50 kwa nchi zenye uwezo mdogo zilizotoa maombi ya msaada, ili kuchangia juhudi za kukabiliana na virusi vya Corona. Benki Kuu ya Iran pia ilitoa ombi la mkopo wa dola bilioni 5 tarehe 12 Machi.