Marefa wa ngumi Tanzania tuna safari ndefu

Gumilapua

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
833
565
Naangalia hapa mapambano ya ngumi yanayoendelea lakini maamuzi ya marefa yanaharibu mchezo.

Pambano la Richard na Julius Indongo, mwamuzi kamaliza mchezo prematurely, ili kumpa ushindi Mtanzania na hata pambano la mkenya Kimario na Ibrahim Mafia pia refa amemaliza mchezo na kumpa ushindi Mtanzania.

Hizi mbeleko ndiyo zinawalemaza mabondia wetu na kutegemea kubebwa!

Ngoja nisubirie main bout nione nini kitatokea.
 
Sikubahatika kuyaona mapambano yote ila la uyu Mtanzania anaye tokea Kenya Ndugu Kimaro dhidi ya Mtanzania wa hapa Ibrahim Mafia ni dhulma katika mchezo wa Ngumi.
Kwanza Ndugu Kimaro hakupigwa Ngumi aliteleza lakini refa ka hesabu mpaka 9 wakati Kimaro alishakua amesimama kuendelea na pambano refa akawahi kumaliza na kumpatia Mtanzania wa hapa nyumbani ushindi kwa TKO.

Azam wasikubali kukumbatia upuuzi wa kupanga matokeo, Brand Yao ni kubwa katika michezo na hata wasipo shirikiana na waandaji uchwara Bado hawata athirika.
Wasiruhusu Tena kutuonyesha Ngumi ambazo tayari mshindi alishapangwa.
Azam wakatae kushirikiana na Mapromota uchwara ili kulinda viwango vya Ngumi Nchini na kusimamia fair play.
 
Aisee pambano la Indonga ilibidi nibadili chaneli niangalie Afcon tu

Sijajua alitumia kigezo gani kumaliza pambano wakati jamaa alikua physically fit kabisa kuendelea
 
Back
Top Bottom