Marando Kuhamia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marando Kuhamia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyunyu, Aug 5, 2010.

 1. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Toka nilivyosikia kuwa mwanasiasa na mwanasheria mkongwe nchini Mabere Marando kahamia CHADEMA, nimekuwa katika upembuzi yakinifu kutokana na historia yan nyuma ya mheshimiwa huyu.

  Mabere Marando; kama wote tufahamuvyo aliwahi kuajiriwa serikalini kule kwa wale wanaojiita "Usalama wa Taifa" Wakati wa vugu vugu la vyama vingi, pamoja na wengine ikiwamo Mrema, ni mmoja wa watu walioutangazia umma kuhama CCM na kujiunga upinzani. Wakati huo NCCR-Mageuzi ilikuwa juu. Wakahamia huko na Mrema. Wakahamasisha watu wote tukaamini mageuzi yanakuja TZ katika uchaguzi huo wa 1995. Wote tunajua yaliyotokea. Marando baada ya kuivuruga NCCR-M akahama chama na kutokomea anakokujua; he stayed low profiled.

  Iweje leo CHADEMA, "chuma kimeshika kasi" anatangaza tena kutoka huko anakokujua na kujiunga nacho? Maswali yanayonitatiza ni haya;

  Je haiwezi kuwa, kutokana na historia ya kazi yake Mabere Marando "yuko kazini" CHADEMA?

  Kuwavuruga na kisha aondoke akilalamika wakati amekimaliza chama chetu?

  Ndugu zangu, naomba luwakilisha hoja yangu.

  Go Dr. Slaa go...
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sote twajua kama Marando anawatetea mafisadi katika kesi zao mahakamani -- Jitu Tapeli na Basil Mramba among them na hili Chadema wanalijua fika. Lakini nilivyoambiwa (msiniulize na nani) ni kwamba alikubali kuwatetea ili kupata ushaidi wa ndani kabisa wa utapeli wao -- kama vile vile 'vimemo' baina ya viongozi wa CCM na hao wezi wa EPA ili auanike hadharani.

  Ameshaupata huo ushahidi wa ndani na alikuwa anangojea mtu wa kuumwaga hadharani. Sasa kisha ampata mtu muafaka na credible kwa kazi hiyo -- Dr W. Slaa na tutegemee makombora yake, kasema tayari anayo 20.

  Safari hii CCM WATAJIBEBAAAAAA!!!!
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  We better be sure he is for real!!!
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wewe nawe si tumeshakuzoea. Unaumwa wewe, lakini hujui tu.

  MS haikubaliki mkuu. Tiba ipo!!!
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Nadhani makombora yan[paswa kwenda sambamba na ilani inayoeleza wakiingia watafanya nini? Kwa mfano wanaweza sema yote waliyonayo na.... watabadili katiba. Just an example!
   
 6. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Mimi nadhani wana mageuzi tuache woga. Kwani Marando ni raia wa wapi? hivi mnafikiri huko usalama wa taifa wana mageuzi hawapo? Ilimradi tu Marando hatugeuki majukwaani na kuisifia ccm kama Mrema. Endelea Marando, songa mbele, tangaza habari za ukombozi wa mtanzania, achana na waoga na wakatishaji tamaa, na hakika tutashinda kwani Mungu yupo upande wetu.
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Masikini Nyunyu ama umetumwa au una lako jambo ! Yaani hata hujui vugu vugu la mageuzi lilivyoanza au hata NCCR-Mageuzi ilianza vipi hadi kwa akili yako unathubutu kuropoka kwa madai ya uwongo - eti Mabere Marando pamoja na Mrema ni mmoja wa watu walioutangazia umma kuhama CCM na kujiunga NCCR-Mageuzi ambayo wakati huo ilikuwa juu ! Pole Nyunyu, Watanzania wameamka na hawako tayari kudanganyika kwa jambo la kipuuzi na kijinga kama hili lako.

  Unajidai ni shabiki wa Dr. Slaa na hapo hapo unamponda moja wa askari wake, mwanzilishi na shujaa wa mageuzi nchini aliyeonja joto la jiwe mikononi mwa pandikizi la CCM kwa jina Augustino Lyatonga Mrema ! Hapana, Nyunyu, rudi huko huko shimoni ulikotoka na umwache mkombozi wetu Dr, Slaa na jeshi lake lililokamilika liendeleze libeneke tuling'oe hili dude lililotuadhiri na kutudumaza kwa miaka karibia hamsini. Kama unamkubali Dr. Slaa, uwe tayari kuwakubali na maluteni wake.
   
 8. K

  Keil JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Nyunyu,

  Huyo Mh. Marando naona amejieleza mwenyewe kwenye hiyo mikutano ya kumtambulisha Dr. Slaa. Nimesoma kwenye gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa. Naomba nivute yale aliyoyasema kwenye huo mkutano mjini Morogoro, para za mwisho kabisa kwenye hii quote:

  Mwenye kutaka habari kamili aende kwenye gazeti husika:

  Marando apasua bomu

  Wakati mwingine ni rahisi kumtuhumu mtu kwa hisia, lakini mpeni nafasi muone kama kweli ana malengo ya kukibomoa chama. Kwa sasa hapo alipo hana nafasi yoyote inayogusa maamuzi magumu ya chama, labda aalikwe kwenye vikao ambako hana nafasi hata ya kupiga kura zaidi ya kuchangia tu. Mpeni benefit of doubt.
   
 9. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ninavyokumbuka mimi ni kwamba Marando hakuwa chanzo cha vurugu NCCR Mageuzi wakati ule, Mrema ndiye aliyekuwa chanzo. Marando alijitahidi sana kukipigania Chama ili kirudi mikononi kwake baada ya kubaini hila za Mrema, bahati mbaya alishindwa. kama mchangiaji hapo juu, naweza kusema Marando alikutana na Ajali ya Kisiasa, lakini ukweli utabakia kwamba Marando ni mmoja wa Waasisi wa Mageuzi nchini.
   
 10. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #10
  Aug 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Marando ni moto wa kuotea mbali, NCCR iliharibiwa na mrema ikawa basi tena. Ninafurahia mtu anapoongea akiwa na ushahid mikononi kama huyu jamaa ambaye anajua sana maana ya ushahidi. Wizi wa EPA ndio uliompeleka Kikwete Ikulu, ndiyo maana serikali haiweiz kufanya lolote kuhusiana na wizi huo.
   
Loading...