Marando ajaribu kete nyingine kwa Babu Seya

Marando ajaribu kete nyingine kwa Babu Seya

yegella

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Posts
3,113
Reaction score
1,104
na Happiness Katabazi

MWANAMUKIZI wa muziki wa dansi nchini,Nguza Vicking ‘Babu Seya' na mwanaye Papi Kocha ‘Mtoto wa Mfalme', wameiomba Mahakama ya Rufaa nchini iipitie upya hukumu yake iliyoitoa Februari mwaka 2010 ambayo iliwahukumu kifungo cha maisha kwa sababu hukumu hiyo ina utetezi wa wazi wa kisheria.

Ombi hilo Na.5/2010 liliwasilishwa kwa niaba yao na wakili wao, Mabere Marando, jana mbele ya jopo lile lile lililotoa hukumu ya awali ya Februari 2010, ambalo linaongozwa na Jaji Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk.

Marando alidai kuwa kwa mujibu wa kanuni ya 66 ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009, inatoa mamlaka kwa Mahakama ya Rufaa kufanya mapitio ya hukumu inazozitoa, hivyo wateja wake wamewasilisha ombi hilo la mapitio kwa sababu wanaamini mahakama yake ilikosea wazi wazi kisheria katika hukumu yake.

Alidai kuwa kanuni hiyo inatoa mamlaka kwa mahakama hiyo kufanya mapitio ya hukumu yake.

Marando alieleza kuwa ombi lake amelileta chini ya kifungu cha 3 aya A ya Kanuni ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009, ikisomwa pamoja na Ibara 13 (3) (6)(a) ya Katiba ya nchi.

Alidai kuwa katika hukumu hiyo kuna baadhi ya aya inasomeka kuwa majaji hao walikubaliana na hoja yake iliyodai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakati inasikiliza kesi hiyo, ilikosea kufuata utaratibu wa kurekodi ushahidi wa watoto walioutoa katika kesi.

Kwamba Mahakama ya Rufaa nayo ikasema licha ya taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto kukiukwa, mahakama yake iliona kuna ushahidi unaounga mkono na kwamba mahakama ya rufaa ilitumia ushahidi wa kuunga mkono kuwatia hatiani waomba rufaa
kwa adhabu ya kifungo cha maisha.

"Waheshimiwa majaji kwa sababu jopo lenu katika hukumu yake lilikiri wazi wazi kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi wa watoto wadogo ambao walidai walitendewa vibaya na waomba rufaa, na sheria za nchi zipo wazi kabisa.

"Nafahamu ni kazi ngumu sana kuwashawishi nyie majaji kubadili uamuzi wenu mlioutoa katika hukumu ya Februari 2010 ambapo mliwatia hatiani wateja wangu, ila kwa utetezi huo wa kisheria niliouainisha unaonyesha katika hukumu yenu mlikubaliana na hoja yangu, naamini mtatumia busara zenu na kufuata sheria," alidai.

Mawakili wa upande wa mjibu maombi (DPP),Angaza Mwipopo, Jackson Mlati,Imaculata Banzi na Joseph Pande, waliomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi hilo kwa kuwa sababu zote alizozitoa jana ni zile ambazo alizitoa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamuliwa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februari mwaka 2010.

Jackson alidai kama Marando anaona hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari, basi angeomba mahakama hiyo impangie jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na siyo ombi lake kuja kusikilizwa na jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu ile ambayo anadai ina dosari.

Jaji Kimaro alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili akaamuru waomba rufaa warejeshwe gerezani na kwamba mahakama itatoa tarehe ya kutoa uamuzi wake kuhusu maombi hayo kwa pande zote mbili.
 
Ombi hilo Na.5/2010 liliwasilishwa kwa niaba
yao na wakili wao, Mabere Marando, jana
mbele ya jopo lile lile lililotoa hukumu ya awali
ya Februari 2010
, ambalo linaongozwa na Jaji
Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk
Mbarouk.

He ain't got a prayer!
 
Kwa nini majaji walewale? Watafanya vilevile kama mwanzo, masikini Nguza na Papii, hivi hao 'watoto' waliofanyiwa vile uwa ni kama 'never existed'!. Story yenyewe ni kama zile za Aesop, Abunuwas au Alifrela ulela. Tunawaombea majaji wawe na maono tofauti juu ya hili.
 
haki na itendeke, how comes mahakama ikakosa kurekodi ushahidi unaotolewa mahakamani?? obvious record keeping yao itakua na dosari tu, na kwa maana hiyo ile hukumu haikua ya haki bali ni ya ki njama!!
 
ndani ya utawala huu tutaona mengi; nadhani iko siku kitatokea kizazi kinachohoji juu ya mambo haya ambayo yako wazi lakini yanafumbiwa macho:- mtu natekwa, anasema nilitekwa na fulani, mamlaka zinamnyamanzisha: mkutano wa wazi wenye ulinzi unarushiwa gruneti, mamlaka hazina majibu, watu wanamwagiwa tindikali mchana kweupe.... mamlaka hazina majibu...., naneno ya Bob: you can fool somepeople sometimes, buta you cant fool all the people all the time.... nadhani iko siku yatatimia
 
God is great! aliyeandaa kiinimacho hiki akumbuke kuna mungu, iko siku atalipa ghali kwa dhulma hii ya waziwazi, mungu simamia waja wako, wote tuseme aamen.
 
God is great! aliyeandaa kiinimacho hiki akumbuke kuna mungu, iko siku atalipa ghali kwa dhulma hii ya waziwazi, mungu simamia waja wako, wote tuseme aamen.
Miaka 4 mbele Mungu kackia kilio chako
 
Back
Top Bottom